DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni kweli kaka, ila kumbuka mimba inaingia kwa ushirikiano wa mwanaume na mwanamke. Kwa hiyo ushirikiano huu ukiendelea baada ya mimba kutungwa, ni ngumu kwa mwanamke kuwaza kutoa mimba.
Hakuna sababu yoyote ile ya kuua. Abortion ni kuua kiumbe hai. Sasa uue kisa limwanaume halieleweki, uue?
 
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana hapa, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu maarufu vya hapa Mwanza (sitaki kuvitaja) na wake za watu waliopata mimba za michepuko.

Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika. Pia, wale wanaokuja kupima mimba wakipatikana kuwa wana mimba na wakaonyesha hali ya kutofurahia au kushtuka, huwa mara nyingi wanauziwa wazo la kuichoropoa.

Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.

Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.

Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.

Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.

Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria.

Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua.

Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini.

Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.

Asante.
Mungu wa Mbinguni akupe ulinzi
 
Jambo la kwanza wanaotoa mimba hawana kosa nadhani ni muda sasa sheria itungwe iruhusiwe kama Marekani tayari kutoa mimba sio kosa maana ata wewe unayetumia kondom unaenda kuzuia mimba kumbe kuna muda sahihi wa kupata mtoto.
Angalizo wadada wengi mmeishia kwa manabii na waganga wa jadi kutafuta watoto mliowaharibu mngali wadogo uko mtapewa mimba na ao waganga hewa na ao watoto watawatesa maisha yenu yote.
Mimba zinatolewa sio kila anayetoa mimba anadhamira mbaya wengi zinatolewa kuokoa uhai wa mama.
 
Jambo la kwanza wanaotoa mimba hawana kosa nadhani ni muda sasa sheria itungwe iruhusiwe kama Marekani tayari kutoa mimba sio kosa maana ata wewe unayetumia kondom unaenda kuzuia mimba kumbe kuna muda sahihi wa kupata mtoto.
Angalizo wadada wengi mmeishia kwa manabii na waganga wa jadi kutafuta watoto mliowaharibu mngali wadogo uko mtapewa mimba na ao waganga hewa na ao watoto watawatesa maisha yenu yote.
Mimba zinatolewa sio kila anayetoa mimba anadhamira mbaya wengi zinatolewa kuokoa uhai wa mama.
Kwa kuokoa maisha ya mama inajulikana, na madaktari ndo huamua hilo. Ila hawa wanazozitoa ni zile za mtu kuamua tu, hakuna medical indication.
Ishawishini serikali kupitia wizara ya Afya na wizara ya sheria wabadilishe sheria na kuruhusu abortion, sio sasa hivi kufanya hivyo wakati sheria za nchi zinakataza.
 
Kwa hiyo hakuna haja ya kuripoti huu uvunjaji wa sheria?
hakuna haja ya kuripoti, sio kesi.

Aliyejiripoti mwenyewe kwamba anajuta katoa mimba tatu za Kanumba na sasa hazai tena hakukamatwa.

Unenforced laws. Hata Marekani zipo. Kuna wa Mexico kila asubuhi wanajipanga barabarani nje ya maduka ya hardware wanasubiri waokotwe na mafundi wakapige day waka, na wanajulikana wamebinjuka border, lakini hawakamatwi. Sio kesi.
 
Halafu wafanyakazi wao wengi wanauza vifaa vya mastabation
 
Abortion (kutoa mimba) ni MAUAJI sawa na kumnyonga mtu mzima.

Abortion sio tu kuvunja sheria ya nchi bali ni DHAMBI mbele ya Mungu.

Mungu ana kanuni zake. Ukipanda maharage, utavuna maharage. Ndio kanuni ya "KARMA"- yaani kila unachofanya ujue UTALIPWA TU. Hapo ni Mungu mwenyewe anajua atakulipaje.

Kama ni binti uliyetoa mimba, unaweza kujikuta utakapoolewa mimba hazishiki, au zinatoka. Au ukampata mume wa kukutesa vibaya - utafikiri ni roho yake mbaya kumbe ni malipizi ya uliyofanya kabla.

Umaweza kuzaa watoto wakakua, wakamaliza chuo, lakini kabla hujaonja "matunda" ya kuwasomesha, mwingine anakufa. Mwingine anakuwa shoga, na mwingine anakuwa mlevi wa madawa ya kulevya na pombe juu. Kumbe:- KARMA !!

Hii ni kweli
 
Back
Top Bottom