DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Abortion (kutoa mimba) ni MAUAJI sawa na kumnyonga mtu mzima.

Abortion sio tu kuvunja sheria ya nchi bali ni DHAMBI mbele ya Mungu.

Mungu ana kanuni zake. Ukipanda maharage, utavuna maharage. Ndio kanuni ya "KARMA"- yaani kila unachofanya ujue UTALIPWA TU. Hapo ni Mungu mwenyewe anajua atakulipaje.

Kama ni binti uliyetoa mimba, unaweza kujikuta utakapoolewa mimba hazishiki, au zinatoka. Au ukampata mume wa kukutesa vibaya - utafikiri ni roho yake mbaya kumbe ni malipizi ya uliyofanya kabla.

Umaweza kuzaa watoto wakakua, wakamaliza chuo, lakini kabla hujaonja "matunda" ya kuwasomesha, mwingine anakufa. Mwingine anakuwa shoga, na mwingine anakuwa mlevi wa madawa ya kulevya na pombe juu. Kumbe:- KARMA !!
 
Kutoa mimba gharama zake Ni sh ngapi ?

Hizo njaa zako ulizozisema zinashibishwakwa hela za hao wanaofanya abortion !

Usiharibu biashara ya watu wengine, kituo kikifungwa/wakinyang'anywa leseni utakula mawe ?

Kistaarabu ulitakiwa uondoke hapo ukatafute maisha sehemu nyingine !
Kuwasagia kunguni sio suluhisho!

Mkuu nikuambie hii dunia haina huruma hata kidogo,,, , ,,, wewe fanya Mambo yako yanayokuhusu tu,,, dunia imejaa kila Aina ya ushetani, Kuna watu wanakula mpaka nyama za binadam wenzao ,,, !
Hii haiwez kuwa biashara bali uuwaji
 
Nasema njaa kwa sababu nilikubali kufanya kazi hapa nikijua kabisa kinachoendelea, na nimekua nikishiriki hiyo dhambi, ila imefika wakati naona sasa hapana, nimeona niseme tu ili mamlaka husika zichukue hatua. Wewe unajali wao kunyang'anywa leseni ila haujali uuaji wanaoufanya kila siku?
Simply ondoka hapo katafute maisha sehemu nyingine? Wewe si umesoma? Ni competent? Jiamini na vyeti vyako, maisha sio sehemu moja tu!

Wanaotoa si wameamua wenyewe? Inakuhusu?

Sheria? Ndo kitu gani? Zimewekwa ili zivunjwe!
 
Simply ondoka hapo katafute maisha sehemu nyingine ? Wewe si umesoma ? Ni competent ? Jiamini na vyeti vyako, maisha sio sehemu moja tu !

Wanaotoa si wameamua wenyewe ? Inakuhusu ?

Sheria ? Ndo kitu gani ? Zimewekwa ili zivunjwe !
Hata wanaoiba ni wao wenyewe wameamua kuiba, na wanavunja sheria pia (ambazo umesema zimewekwa ili zivunjwe), kwa hiyo pia tusiwaingilie, tuwaache tu waibe?
 
Back
Top Bottom