Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 12,001
- 27,175
Mkuu acha apoteze kazi jamii ipone,siamini kama hajui hilo,maana hata kazi yenyewe inaonekana haifurahii tena kutokana na kulazimika kufanya kitu ambacho anajua wazi ni kosa.Si njaa zake ndo zinamfanya aendelee kuwa kwenye hiyo taasisi Kama alivyobainisha si ndio ?
Swali, hiyo taasisi ikifungiwa ama kunyang'anywa leseni si atapoteza kazi ???
Mambo mengine unaachana nayo tu ! Hi dunia imejaa kila ushetani ! Watu wanafanya mpaka biashara za viungo vya binadamu sembuse abortion ??
Ukiona Jambo fulani halikufai kimaadili au kulingana na Sheria za nchi achana nalo ! Hii dunia haina huruma na mtu, watu wanaangalia pesa tu !
Tunajua kwamba wanaotoa mimba hapo ni watu walioamua wenyewe lakini kufanywa na taasisi ambayo imeaminiwa Kitaifa kutoa huduma na watumishi wake kukiuka viapo vya maadili haikubaliki,likiachwa hili litaibuka lingine watoto watatekwa huko mitaani wataenda kunyofolewa viungo hapohapo halafu tutasema tena hayatuhusu huku watu wakipotea.
Lazima pawepo wa kujitoa mhanga,Leo hii Nyeyere angelambishwa asali na wakoloni tusingekuwa hapa,kuna watu walikufa Ili wengine tupone,ndivyo dunia ilivyo,uovu hautakoma na wema hautakoma pia.