DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nasema njaa kwa sababu nilikubali kufanya kazi hapa nikijua kabisa kinachoendelea, na nimekua nikishiriki hiyo dhambi, ila imefika wakati naona sasa hapana, nimeona niseme tu ili mamlaka husika zichukue hatua. Wewe unajali wao kunyang'anywa leseni ila haujali uuaji wanaoufanya kila siku?
Yule akibaki na mimba ikaleta mtoto akimshindwa kumlea kwa ugumu wa maisha kukimbiwa na mwanaume aliemtia mimba akaamua amfukie ardhini au akamtupa jalalani ikabainika amefanya hivyo anaeenda jela ni nani?

Sasa kipi bora uende jela ukasotee miaka kwa sababu ya tumbo lako lililobeba mimba au utoe mimba ambayo imeingia bila kutarajia ukaendelea na maisha mengine?

Sometimes uwe unafikiria nje ya box mkuu dunia imejaa ushetani huo wa kutoa mimba cha mtoto,
 
Simply ondoka hapo katafute maisha sehemu nyingine ? Wewe si umesoma ? Ni competent ? Jiamini na vyeti vyako, maisha sio sehemu moja tu !

Wanaotoa si wameamua wenyewe ? Inakuhusu ?

Sheria ? Ndo kitu gani ? Zimewekwa ili zivunjwe !
Acha afichue uovu,kusoma na kujiamini ni pamoja na kuisaidia jamii yake,sasa kama umesoma na husaidii jamii elimu yako yafaa nini?

Inamhusu kwa sababu jamii inayoathirika ni jamii ambayo nae anaishi.
 
Yule akibaki na mimba ikaleta mtoto akimshindwa kumlea kwa ugumu wa maisha kukimbiwa na mwanaume aliemtia mimba akaamua amfukie ardhini au akamtupa jalalani ikabainika amefanya hivyo anaeenda jela ni nani? Sasa kipi bora uende jela ukasotee miaka kwa sababu ya tumbo lako au utoe mimba ambayo imeingia bila kutarajia ukaendelea na maisha mengine?

Sometimes uwe unafikiria nje ya box mkuu dunia imejaa ushetani huo wa kutoa mimba cha mtoto,
Mbona unaanzia katikati mkuu? Mimba inaingiaje bila kutarajia? Maana mimba kuingia sio sawa na mtu kudondokea mtaroni wakati anatembea.
 
Mbona unaanzia katikati mkuu? Mimba inaingiaje bila kutarajia? Maana mimba kuingia sio sawa na mtu kudondokea mtaroni wakati anatembea.
Mkuu wengine hawajui mpangilio wa mzunguko wa siku zao wengine siku hua zinavurugika kwa hio anajikuta tu kamwagiwa Dejan wawili baada ya mwezi kitu kinasoma
 
Mkuu wengine hawajui mpangilio wa mzunguko wa siku zao wengine siku hua zinavurugika kwa hio anajikuta tu kamwagiwa Dejan wawili baada ya mwezi kitu kinasoma
Kwa hiyo suluhisho ya hayo ni kufumbia macho utoaji wa mimba kinyume cha sheria?
 
Yule akibaki na mimba ikaleta mtoto akimshindwa kumlea kwa ugumu wa maisha kukimbiwa na mwanaume aliemtia mimba akaamua amfukie ardhini au akamtupa jalalani ikabainika amefanya hivyo anaeenda jela ni nani?

Sasa kipi bora uende jela ukasotee miaka kwa sababu ya tumbo lako lililobeba mimba au utoe mimba ambayo imeingia bila kutarajia ukaendelea na maisha mengine?

Sometimes uwe unafikiria nje ya box mkuu dunia imejaa ushetani huo wa kutoa mimba cha mtoto,
Pigania utoaji mimba uruhusiwe sasa,kwa sasa ni kosa la jinai kwahio wanachofanya Marie stopes ni kuihujumu nchi.
 
Mkuu sheria pekee zinazoheshimiwa zipo kwenye vitabu vya dini hizi zingine zinapindishwa kila siku tena na watunga sheria wenyewe, sasa wewe ni nani usipindishe sheria?
Unajua kuwa hata mwizi anapindisha sheria pia?
 
Pigania utoaji mimba uruhusiwe sasa,kwa sasa ni kosa la jinai kwahio wanachofanya Marie stopes ni kuihujumu nchi.
Sijasema iruhusiwe nimesema angalia huyo anaeamua kutoa mimba ana hali gani, unajua binadamu mnajua kulaumu tu hamjui kuangalia upande wa pili nini kimepelekea atoe mimba?
 
Acha afichue uovu,kusoma na kujiamini ni pamoja na kuisaidia jamii yake,sasa kama umesoma na husaidii jamii elimu yako yafaa nini?

Inamhusu kwa sababu jamii inayoathirika ni jamii ambayo nae anaishi.
Si njaa zake ndo zinamfanya aendelee kuwa kwenye hiyo taasisi Kama alivyobainisha si ndio ?

Swali, hiyo taasisi ikifungiwa ama kunyang'anywa leseni si atapoteza kazi ???

Mambo mengine unaachana nayo tu ! Hi dunia imejaa kila ushetani ! Watu wanafanya mpaka biashara za viungo vya binadamu sembuse abortion ??

Ukiona Jambo fulani halikufai kimaadili au kulingana na Sheria za nchi achana nalo ! Hii dunia haina huruma na mtu, watu wanaangalia pesa tu !
 
Na wanafuata nini huko ilihali kuna Dokta Kuria kibao mtaani wanafaulsha hizo mbaga?.
 
Wewe ndo unajua leo. Hiyo ni taasis ya kimarekani ambayo lengo lake kuu ni kuadvocate depopulation duniani. Wanatumia kigezo cha family planning ili kuhalalisha agenda yao.

Wapo duniani kote na wala hawana gharama kubwa sometimes wana ngo zao zinafanya abortion bure kabisa
 
Back
Top Bottom