DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana pale, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu. Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika.

Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.

Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.

Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.

Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.

Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria za nchi.

Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua.

Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini.

Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.

Asante.
Acha watoe watajua hawajui karma revolves around.
 
Mkuu wengine hawajui mpangilio wa mzunguko wa siku zao wengine siku hua zinavurugika kwa hio anajikuta tu kamwagiwa Dejan wawili baada ya mwezi kitu kinasoma
Excuses za kitoto sana hizi , kama mtu hataki mimba atafanya kila liwezeknalo asishike ujauzito.. people just don't care wanaona the easy way out ni kutoa mimba...maajabu sana
 
kwa kuwa ni kinyume na sheria za nchi, basi ahsante na mamlaka husika wamekuskia watalishughulikia. Ila sheria ya utoaji mimba serikali inabidi waitazame sana kwa jicho pevu.
Sawa kabisa, wanachotakiwa kufanya ni kushawishi serikali ya Tanzania (kupitia wizara ya afya na wizara ya sheria) waweze kuruhusu abortion nchini, na sio kufanya utoaji mimba kinyume cha sheria.
 
Excuses za kitoto sana hizi , kama mtu hataki mimba atafanya kila liwezeknalo asishike ujauzito.. people just don't care wanaona the easy way out ni kutoa mimba...maajabu sana
Exactly on point.
Mtu anaona ni rahisi zaidi kuchoropoa tu mimba. Hii term ya "mimba isiyotarajiwa" ibaki kwa wale tu ambao wameshika mimba kwa kubakwa, kinyume na hapo aisee hakuna mimba isiyotarajiwa.
 
Suluhisho ni kufumbia macho uvunjaji wa sheria za nchi ambazo zinakataza utoaji wa mimba?
Kwa hiyo unaona ni bora wafe kisa kasikia ukinywa jiki mimba itatoka . We kama unaona huwezi hiyo kazi acha wengine watafanya na sio kuleta unafiki wako hapa.kama unajiamini sio mnafiki wafate hao maboss zako waambie mbona wanavunja sheria za nchi.😏
 
Kwa hiyo ni bora mamlaka za nchi ziendelee kufumbia macho huu uvunjaji wa sheria ya kukataza utoaji mimba?
Bora unafiki kuliko uuaji.
 
Hapana, lengo langu ni kupaza sauti ili angalau mamlaka za nchi zifahamu na zifanye uchunguzi juu ya hili na kuchukua hatua stahiki.
Sasa unafikiri nani asiyejua jua shughuli ya hiyo taasisi, halafu nchi inapokubali misaada na mikopo ya mabeberu ndo inakuja na masharti kama hayo kuziacha hizo taasisi zifanye kazi zake kwa uhuru.
 
Sasa unafikiri nani asiyejua jua shughuli ya hiyo taasisi, halafu nchi inapokubali misaada na mikopo ya mabeberu ndo inakuja na masharti kama hayo kuziacha hizo taasisi zifanye kazi zake kwa uhuru.
Sasa kama ndo hivyo basi kwa nini hao mabeberu kupitia hiyo hiyo misaada wasishawishi nchi ikubali tu sheria ya utoaji mimba? Hiyo si ingekua rahisi zaidi?
 
Marie Stopes ndo kazi yao inajulikana kwa miaka mingi sana. Na sio Mwanza tu ni kila unapoona bango la Marie Stopes Tanzania nzima. Wana uzoefu wa miaka mingi kwenye huo ushetani wa kutoa mimba. Mwaka 2009 nikiwa chuo niliwahi kupendwa na mdada mmoja alikuwa mkubwa kidogo kwangu sasa kabla hata ya kupeana papuchi akawa analalamika mara kwa mara tumbo linamuuma.. akasema nimsindikize Marie Stopes Sinza Afrikasana... tulipofika ndo niligundua alitoa mimba na kinachomsumbua sababu ni hiyo. Nikakata mawasiliano.
 
Hao waliniokoa sana zama za ubaharia, Mungu nisamehe tu maana ingekuwa balaa zito endapo ningeonekana nimemtunisha mwanafunzi 🤣🤣🤣
 
Marie Stopes ndo kazi yao inajulikana kwa miaka mingi sana. Na sio Mwanza tu ni kila unapoona bango la Marie Stopes Tanzania nzima. Wana uzoefu wa miaka mingi kwenye huo ushetani wa kutoa mimba. Mwaka 2009 nikiwa chuo niliwahi kupendwa na mdada mmoja alikuwa mkubwa kidogo kwangu sasa kabla hata ya kupeana papuchi akawa analalamika mara kwa mara tumbo linamuuma.. akasema nimsindikize Marie Stopes Sinza Afrikasana... tulipofika ndo niligundua alitoa mimba na kinachomsumbua sababu ni hiyo. Nikakata mawasiliano.
Aisee. Kwa hiyo hakuna tunachoweza kufanya?
 
Back
Top Bottom