DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Uzuri wao wana vifaa vya kisasa wala mtolewaji hasikii maumivu kabisa 🤣🤣🤣 hawatumii machuma kama wale wa hospitali za kata!
Sheria ya jela miaka 30 haijakaa poa aisee. Kama umempa mwanafunzi mimba ikashindikana kusuluhisha nje ya mahakama bora kuitoa tu maana miaka 30 jela ni kuharibu maisha mazima wakati kitanda hakizai haramu. Pia sheria ya ndoa inaruhusu mtoto wa miaka 16 kuolewa na utakuta uliyempa ni miaka 19 ila mwanafunzi.
 
Ili umkamate red handed, na kumfukuza kazi mara moja!! Sema tu na yeye amejiachia mno. Hivi hao waajiri wake wakifanya uchunguzi mdogo tu kwa wahudumu wao wa afya hapo kituoni, watamkamata kirahisi sana.

Na kama watashindwa, waniite mara moja ili niwakabidhi mhusika wao( just kidding 🤗)
Hadi nimekuja kulisema hapa, najua wazi kabisa kuwa uwezekano wa mimi kujulikana na kufukuzwa kazi upo, ila kwa hatua niliyofikia ni bora tu nifukuzwe kazi kuliko kuendelea kushiriki huu uuaji na uvunjaji wa sheria za nchi.
 
Sasa wewe bila pesa utakubali kuwa mke wangu na mimba nikikupa hutatoa?
Ukinipa mimba siwezi kuitoa, nitalea mwanangu kwa jua na mvua.
Hahahaha..!! Kuhusu kuwa mkeo, ukijieleza vizuri hata bila pesa mbona naweza tu kukubali? Labda uwe domo zege😂😂
 
Ukinipa mimba siwezi kuitoa, nitalea mwanangu kwa jua na mvua.
Hahahaha..!! Kuhusu kuwa mkeo, ukijieleza vizuri hata bila pesa mbona naweza tu kukubali? Labda uwe domo zege[emoji23][emoji23]
Mkuu vipi .. naomba nikutongoze basi?
 
Mfadhili mkuu wa marie stopes kifedha ni nani? Pesa ya hawa wazungu inakuja na masharti
Wafadhili wao wakubwa hawa ni serikali ya Uingereza, kupitia shirika lao la misaada la UKAID, pia kuna Bill & Melinda Gates foundation, shirika la misaada la Australia, Shirika la misaada la Ufaransa,UNFPA, na wengine wengi tu. Hawa wana funders kibao.
 
Sheria ya jela miaka 30 haijakaa poa aisee. Kama umempa mwanafunzi mimba ikashindikana kusuluhisha nje ya mahakama bora kuitoa tu maana miaka 30 jela ni kuharibu maisha mazima wakati kitanda hakizai haramu. Pia sheria ya ndoa inaruhusu mtoto wa miaka 16 kuolewa na utakuta uliyempa ni miaka 19 ila mwanafunzi.
Ni kweli unalosema kuhusu adhabu ya miaka 30 jela.
 
Ukinipa mimba siwezi kuitoa, nitalea mwanangu kwa jua na mvua.
Hahahaha..!! Kuhusu kuwa mkeo, ukijieleza vizuri hata bila pesa mbona naweza tu kukubali? Labda uwe domo zege😂😂
Nimefurahi sana kuona kumbe wanawake mnaojielewa bado mpo. Tafadhali nipatie namba, venue na tarehe ya interview ili tuweke mambo sawa 😀
 
Wafadhili wao wakubwa hawa ni serikali ya Uingereza, kupitia shirika lao la misaada la UKAID, pia kuna Bill & Melinda Gates foundation, shirika la misaada la Australia, Shirika la misaada la Ufaransa,UNFPA, na wengine wengi tu. Hawa wana funders kibao.
Unafikiri kwa nini mnapata customers wengi?
 
Ila kwa Tanzania haturuhusu utoaji mimba, labda tu ikiwa maisha ya mama yako hatarini. Sasa wao wanapata wapi nguvu ya kuyafanya hayo nchini, je mamlaka hazilijui hili?
Wewe unaonekana huijui hii nchi kwa undani. Marie Stope wapo Bongo kitambo sana. Na moja ya shughuli zao kuu, ni hiyo isiyo rasmi ya utoaji mimba.
 
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana pale, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu. Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika.

Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.

Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.

Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.

Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.

Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria za nchi.

Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua.

Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini.

Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.

Asante.
Nipe namba zao
 
Unafikiri kwa nini mnapata customers wengi?
Sababu ziko nyingi:
1.Uelewa mdogo wa vijana kuhusiana na miili yao na jinsi ya kujilinda na mimba
2.Tamaa za maisha ya juu kwa watoto wa kike zinazopelekea wao kujiingiza kwenye mahusiano ili kukidhi tamaa zao kifedha, hivyo kuishia kupata mimba bila kujipanga
3.Uelewa hafifu wa vijana kuhusu upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango
4.Vijana kutopenda kutumia njia za uzazi wa mpango ambazo zipo, kwa sababu mbalimbali kama imani potofu, uelewa hafifu, na kadhalika.
5.Vijana wa kike kutokua na "power" kwenye masuala ya ngono (hawawezi kulazimisha kutumia condom kama mwanaume hataki, hata kama yeye anataka).
 
Wafadhili wao wakubwa hawa ni serikali ya Uingereza, kupitia shirika lao la misaada la UKAID, pia kuna Bill & Melinda Gates foundation, shirika la misaada la Australia, Shirika la misaada la Ufaransa,UNFPA, na wengine wengi tu. Hawa wana funders kibao.
Kama ni hao ondoa matumaini kwamba serikali yako inaweza kufanya lolote.

Ndio maana wanataka kujua msimamo wako kabla hujaajiriwa.
 
Back
Top Bottom