DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa hiyo najisumbua bure tu, haiwezi kusaidia kitu?
Serikali ikiingilia wafadhili wenu nao watazuia funding. Umejiuliza ajira zenu zinahudumia idadi ya watu wangapi nchini kiuchumi?

Hakuna lisilojulikana serikalini, lakini ukishakuwa tegemezi ndio hivyo tena.

Kutoa mimba ni jinai kama ilivyo kwa vitendo vya ushoga. Hujasikia kuna watu wamepewa fedha kuja kuhamasisha ushoga nchini?! 😆😆😆
 
Ilianzishwa kwa ajili ya utoaji Mimba huko UK. Hii ndo kazi yake ya kwanza kabisa kwenye katiba yao

Asante mkuu
Kuna watu hawajui hasa majukumu ya msingi ya hii taasisi; mojawapo mi kusaidia watu wenye complications za masuala ya uzazi
Lingine ni kutoa elimu/ushauri na huduma za uzazi wa mpango ikiwa ni njia za muda mrefu na muda mfupi.

Kama mtu hajui kazi za Marie Stopes aende ku gugu ataziona![emoji3]
 
Serikali ikiingilia wafadhili wenu nao watazuia funding. Umejiuliza ajira zenu zinahudumia idadi ya watu wangapi nchini kiuchumi?

Hakuna lisilojulikana serikalini, lakini ukishakuwa tegemezi ndio hivyo tena.

Kutoa mimba ni jinai kama ilivyo kwa vitendo vya ushoga. Hujasikia kuna watu wamepewa fedha kuja kuhamasisha ushoga nchini?! 😆😆😆
Daaahhh...!! Ngoja nione nini kitafuata baada ya hii taarifa yangu, kama mambo yataendelea kama kawaida basi nitaamini kuwa mamlaka zimebariki hili.
 
Asante mkuu
Kuna watu hawajui hasa majukumu ya msingi ya hii taasisi; mojawapo mi kusaidia watu wenye complications za masuala ya uzazi
Lingine ni kutoa elimu/ushauri na huduma za uzazi wa mpango ikiwa ni njia za muda mrefu na muda mfupi.

Kama mtu hajui kazi za Marie Stopes aende ku gugu ataziona![emoji3]
Lakini kwa Tanzania hawajapewa usajili kwa ajili ya kutoa huduma za abortion, kasome hata website yao ya Marie stopes Tanzania.
Kwa sababu abortion kwa Tanzania ni illegal.
 
Asante mkuu
Kuna watu hawajui hasa majukumu ya msingi ya hii taasisi; mojawapo mi kusaidia watu wenye complications za masuala ya uzazi
Lingine ni kutoa elimu/ushauri na huduma za uzazi wa mpango ikiwa ni njia za muda mrefu na muda mfupi.

Kama mtu hajui kazi za Marie Stopes aende ku gugu ataziona![emoji3]
Yes Katiba yao inasema : Iwapo mwanamke anamimba labda kabakwa au akuwa Tayari kuzaa(mfano yupo JKT(kwa Tanzania) ni mfano tu! Au yupo Chuo etc - Yaani ana sababu ya msingi kama yeye- Rukhusa Kutoa MIMBA! Ata yeye Mwanzilishi alianzisha hii Marie Stopies kwa sababu alikuwa ataki tena zaa na mume wake wa Ndoa😭Yes Marie Stopies aliamuwa ataki tena zaa na mumewe wa Ndoa- na Leo hii UK ambako ndo asili ya Marie Stopies Mkeo wa Ndoa kama amesema ataki usex nae- ukiforce Ni Kesi ya KUBAKA- na anaweza enda akaitoa mimba na ana kosa kisheria
 
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana hapa, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu. Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika.

Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.

Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.

Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.

Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.

Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria za nchi.

Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua.

Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini.

Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.

Asante.
Ni Watoa Mimba walioizinishwa na Serikali ya Uingereza! Na kwa sasa wapo Duniani kwenye nchi zaid ya nchi 30!. Once nikutana na boss wao pale Sinza opp na ilipokuwa Ongera Bar- wapo mpaka leo ndo alinipa hii history yao na majukumu yao
 
Attachments

  • D7D491A9-73CF-4ED2-81D7-0E496666710D.jpeg
    D7D491A9-73CF-4ED2-81D7-0E496666710D.jpeg
    6.5 KB · Views: 10
  • A2530949-A4FE-41B7-9833-9D7175371D88.png
    A2530949-A4FE-41B7-9833-9D7175371D88.png
    80.9 KB · Views: 10
  • 98F168E2-16ED-4590-90AE-1639B6D65489.png
    98F168E2-16ED-4590-90AE-1639B6D65489.png
    93.8 KB · Views: 9
  • 9CC004C5-AD68-42CF-B760-BEA4C1001FC5.png
    9CC004C5-AD68-42CF-B760-BEA4C1001FC5.png
    247.7 KB · Views: 10
Yes Katiba yao inasema : Iwapo mwanamke anamimba labda kabakwa au akuwa Tayari kuzaa(mfano yupo JKT(kwa Tanzania) ni mfano tu! Au yupo Chuo etc - Yaani ana sababu ya msingi kama yeye- Rukhusa Kutoa MIMBA! Ata yeye Mwanzilishi alianzisha hii Marie Stopies kwa sababu alikuwa ataki tena zaa na mume wake wa Ndoa😭Yes Marie Stopies aliamuwa ataki tena zaa na mumewe wa Ndoa- na Leo hii UK ambako ndo asili ya Marie Stopies Mkeo wa Ndoa kama amesema ataki usex nae- ukiforce Ni Kesi ya KUBAKA- na anaweza enda akaitoa mimba na ana kosa kisheria
Ni sawa, ila angalia website yao kwa Tanzania hapa What we do. hakuna sehemu wamesema wanatoa huduma za abortion, kwa sababu wanajua ni kinyume cha sheria, na walipoomba usajili Tz, hawakuomba kwa ajili ya kutoa huduma za kutoa mimba (cheki screenshot niliyo attach)
 
Attachments

  • Screenshot_2023-01-05-19-02-04-521_com.android.chrome.jpg
    Screenshot_2023-01-05-19-02-04-521_com.android.chrome.jpg
    126.7 KB · Views: 11
Back
Top Bottom