Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Hizo sheria zilipokuwa zinatungwa walijua zitatumika kwa nani. Watu walizipigia kelele sana lakini walioneka wehu. Ndio dawa yake.
 
Na bado wanavipindi vya hovyo hovyo vingi kuna kile cha diva anaongelea upuuzi upuuzi muda wote tu
 
Sam Sasali kwa kujipendekeza na kutojua mipaka yake ya kazi kaiponza taasisi nzima....Utangazaji ni taaluma za watu hizo si kitu cha kuvamia tu....Kifupi nyundo kajisahau kabisa anawaza teuzi tu....Teuzi zipo tu fanya kazi nzuri utaonwa tu na teuzi itakuhusu
 
Mnaweza kuishi bila taarifa za uchaguzi, ishini namna hiyo, hilo ni funzo!!
 
Hakuna professionalism.
Mbona vyombo vya serikali vikichukua hatua dhidi ya chama chako pendwa huoni kama chama pendwa kimekosea, kwanini unahisi tcra iko sawa kosa la kipindi kimoja imfungie vipindi vyote vya tv pamoja na redio.
 
Ilikuwa station pendwa ya akina jiwe na genge lake, leo hii kibao kimewageukia.

Cloudz wajue kuwa kile chama ni cha kuzimu, hakina urafiki wa kudumu na mtu.
 
Yani kosa la kipindi kimoja wamefungia TV na redio naona muda wote wanaomba msamaha na kupiga mziki tu. Kama kosa lilitokea clouds 360 kwanini wamefungia vipindi vyote?
Hii siyo sawa kabisa.

Si sawa kwa kanuni zipi?
 
Safi Sana ..Bdozen alisoma nyakati na kusepa zake.

Wasije wakasema TL hakuwaambia lakini.
 
Si sawa kwa kanuni zipi?
Unafungia chombo cha habari kwa kosa la watangazajiwa kipindi kimoja tena kwa siku saba, wangefungia basi kipindi maana kuna vipindi vingi ambavyo havifanya hilo kosa.

Uzuri lungu linashuka taratibu kila mtu litamgusa, tutaelewna tu.
 
Unafungia chombo cha habari kwa kosa la watangazajiwa kipindi kimoja tena kwa siku saba, wangefungia basi kipindi maana kuna vipindi vingi ambavyo havifanya hilo kosa.
Uzuri lungu linashuka taratibu kila mtu litamgusa, tutaelewna tu.

Hawa ni kati ya vituo vilivyofaidika sana na CCM, hasa kupindi cha Kikwete.

Acha na wao waisome namba.
 
CCM haina rafiki wa kudumu.
Mataga wote jifunzeni kwa kilichowapata Clouds, IPO SIKU NA NYIE YATAWAKUTA.
 
Mbona vyombo vya serikali vikichukua hatua dhidi ya chama chako pendwa huoni kama chama pendwa kimekosea, kwanini unahisi tcra iko sawa kosa la kipindi kimoja imfungie vipindi vyote vya tv pamoja na redio.
Sina chama, tuanzie hapo kwanza.
 
Naangalia TV station ya clouds TV muda huu linapita tangazo la kuomba radhi kwa watanzania kuwa wamekosea kurusha maudhui yaliyokosea kanuni za CCM. Huu ni zaidi ya uhuni.

Nataka niwaambie mambo kama haya yakifumbiwa macho tutanyamazishwa nchi nzima na watakua na uwezo wa kutupangia maisha kwa namna wanavyotaka wao.

Hii ni issue inayohusu uhuru wa vyombo vya habari. Mnatakiwa kupinga kwa nguvu zote uminyaji na ukandamizaji wa uhuru wa vya habari.

Msikate tamaa.mapambano yanaendelea.
 
Ingetosha wapewe adhabu ya kuomba radhi hata kwa mwezi mzima huku matangazo yao yakiendelea kuwa hewani,onyo ilikuwa ni adhabu kubwa sana kwao.

Kwa sasa uchumi wa sekta binafsi hata ukiyumba kwa siku mbili ni hatari sana kwa hali ya waajiriwa wake. Wakati mwingine itoshe kupeana adhabuza onyo, watanzania tungeelewa tu kuwa Clouds walitoa kitu kisicho sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…