Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

WATAFUNGULIWA KABLA YA SIKU SABA KUISHA.

KAMA KUNA MTU ANABISHA ASEME.
NINA UHAKIKA 100% MAGUFULI HAWEZI KUWAACHA WATOTO PENDWA WASISIKIKE HEWANI 7 DAYS. NEVER!

KUNA AMRI ITATOKA JUU MUDA SI MREFU!.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la watangazaji wa clouds Ni kujifanya wao wajuaji wa Kila kitu. Kujifanya watoto wa mjini wao, kujifanya wao Kila mtu tajiri au kiongozi wao ndo wanamjua Zaid wao.
 
And then it started.., or rather it continues? 🤔
 
Wewe mwaka 2015 ulikuwa jela ? Mwaka 2015 ndo ulikuwa mwaka mgumu sana ktk chaguzi walizowai kushiriki CCM sidhani kama uchaguzi huu unawaumiza kichwa CCM ndo maana toka Chadema waanze kupiga kelele umeona nani wa CCM anajibu kwa maana ya kudharau ingekuwa wanayosema Chadema yana inpact au damage kwa Chama na serikali bhasi kila siku ungemuona Polepole au Msemaji wa serikali Mr Hassan mbele ya waandishi wa habari kujibu hzo ngonjera za Lissu na chadema

Clouds fm wamefanya kosa na adhabu ipo kisheria kabisa kama unakumbuka Channel ten walishawai kufanya hvyo kwa matokeo ya uchaguzi wa zanzbar ukiacha kila TV au Radio kutangaza matokeo wakt mwenye mamlaka hayo ni NEC utakuwa umeleta Contradiction kwa walaji wa habari kwani kila chombo kitamtangaza mtu ambae wanadhani wao ameshinda

Kuhusu clouds kuongozwa kwa kusikilizwa sijui takwimu hzo umezotoa wapi ukizungumzia Radio inayosikika nchi nzima mpk bibi yako kijijini anaisikia ni TBC taifa haya kwani Serikali inashindwa kuwambia Clouds wasirushe mkutano wenu mpk waifunge? Hv unajua hasara wakatayoipata Clouds kwa siku 7 unajua ni matangazo mangapi itabidi wa warudishe pesa kwa vile hayakuruka muda maalumu uliopangwa ? Acheni ramli za kipuuzi wenzenu wanapewa likizo ya siku 7 bila malipo nyumbani nyinyi mnaleta siasa zenu hapa
 
Ung'amuzi wako hauna mantiki kwasababu Lissu hategemei vyombo vya habari, Lissu ni habari usikilize radio usisikilize utamsikia tu
 
Watashindwa tu na nguvu ya Umma, waache warumie vibaya madaraka walio nayo.
 
Nonsense. Vipi hao Wakurugenzi ambao walitangaza? Nilimsikia Msimamizi wa Jimbo la Ruangwa akitangaza tena kwa mbwembwe kuwa Majaliwa amepita bila kupingwa. Yeye anachukuliwa hatua gani?
 
Waifungie tu Great Thinkers huwa hawasikilizi Clouds FM... alisikika mwanaJF mmoja akisema.
Mara ya mwisho kusikiliza Clouds FM ilikuwa wakati madogo wangu M.L. Chris na Seba (Deo) Maganga walipokuwa wakitangaza.
 
Umeona sasa!!! only smart people will understand this.........hivi lini chadema wanakuja na chombo chao??
Tanzania daima liko wapi? kama Clouds inafanyiwa hivyo je Chadema itafanyiwaje? Watawezana na hizo faini za kila siku?

Tukubali tu kwamba nchi imeharibiwa na sisi tukikenua meno na kuishia kulalama tu humu mitandaoni!

Unakumbuka vyombo vya habari wakati wa Kikwete? vilikua huru na watu walipenda hata kusikiliza taarifa za habari..siku hizi ni TBC tu tena matukio ya kuapishana au kufungua makongamano na habari za SGR au tazama anga!

Nchi imekua familia ya mtu mmoja hii analotaka yeye ndio linalokua.. shame!
 

When will NEC approve and publish any statistics, if at all? They are scheming along with their CCM counterparts to see how they can cook the data and lie to the public in favour of Magufuli?

We know everything they are doing, it's just a matter of time before the mask is finally lifted for the world to see who is behind all the pain this country bhas been going through.

Just a matter of months.
 
Wafungiwe maisha ni wapuuzi sana
Mimi Clouds huwa siwasikilizi hata siku moja na siwapendi kwani ni vibaraka.

Ile Clouds ya mwanzoni kabisa ndiyo ilikuwa pure entertainment studio na hata siku moja walikuwa hawaweki mambo ya siasa. Ila natoa tahadhari.

Hata kama adui yako akipatilizwa na hizi sheria za kikandamizaji zilizobuniwa na hawa watawala waoga, usifurahie.

Hao wamefungiwa siku saba tu, lakini target yao ni kufanya media ziogope na inaonekana kuna maandalizi ya kuja kufungia chombo huru tena kwa muda mrefu.
 
Hapa nakuunga mkono kufungia siku 7 redio na tv inayotazamwa na namba 1 sio rahisi.

Hilo sio gazeti la tanzania daima wala mwanahalisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…