CNN and Coronavirus: Africa in existential threat

CNN and Coronavirus: Africa in existential threat

Wako sahihi sana hao maana mpaka sasa haileti mantiki kwanini hatujafa milioni 10 Afrika, na hatuendelei kufa kwa laki tano kila siku.
Huu ugonjwa unawatesa mataifa yenye uwezo mara 1,000 zaidi yetu Afrika, na ukweli hamna kikubwa tunachokifanya kuzuia, Waafrika tupo tupo siku zinaenda, Corona yenyewe inatupapasa wala haijaonyesha makucha huku mpaka sasa.
Ukitembea mtaani uone tunavyoishi, hata kwa wale ambao wamechukua tahadhari ya hali ya juu Afrika, bado hawajafikia hata robo ya wanachokifanya wale wenye kufa Ulaya.
Hiki kitu jameni wazungu wagundue dawa mapema kabla hakijapata sababu za kutukondolea macho Afrika, maana sisi wenyewe hatuna uwezo hata wa kutengeneza dawa za aina ya panadol.
Barikiwa sana.
 
Hiyo chanjo wanayoitengeneza ndio hatari zaidi ya huu ugonjwa wenyewe kwa maana hii itakayoletwa huku kwenye Continent itachanganya na depopulation agents
Halafu Serikali zetu uchwara zitalazimisha kila mmoja wetu adungwe.

Halafu wanaume kwa wanawake tunajikuta hatuna tena uwezo wa kuzaa Think man
Acha kuwa na negativity ?Wewe haujawahi kuchanjwa chanjo yeyote ?Bila chanjo wewe ungekufa kwa surua au ungeshaugua polio. Kwenye chanjo kuna protocols bwana.Acheni kupayuka payuka ujinga.
 
Mabeberu wameshaongea mara kadhaa.

Kifupi hawafurahishwi na uwepo wa bara hili. Watafanya kila wanaloona linafaa kutupoteza then watasingizia Corona.

Tujihadhari sana..

Bill G kashaongea several times.. Africans will die in billions.. They don't like our presence in this planet. Aarssholes
Lakini hata wakitumaliza watagundua hawajamaliza matatizo. Mwisho watagundua wao ndiyo tatizo. Kama ndivyo ujinga wao hauna kifani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama una Bima lakini ventilators hazitoshi
Look sisi tunajiingiza kwenye Mega projects lakini hospitali zetu utasema ni machinjio ya wagonjwa
Maji safi na salama hakuna ila tunaenda kununua Ndege kubwa na ghali sana kwa cash
Sijui jamaa anayatafakari haya huko Chattle aliko
..!????
 
Binadamu ana mucus kwenye njia ya hewa, hii ni sehemu ya kinga ya mwili. Hewa ikiingia na uchafu unakamatwa na mucus na uchafu ule unautoa kama kohozi.

Mucus goblets zikishambuliwa na virus ndiyo mafua yanachuruzika na huweza kukohoa. Maambukizi yakitokea kwenye mucus membrane husababisha kikohozi. Ndiyo maana unatumwa kikohozi ili wataalamu wagundue ni maambukizi gani.

Covid-19 hushambulia njia ya hewa na maambukizi huleta joto mpaka centi grade 38-39. Mucus goblets zinashambuliwa kwa kasi na Hutoa makohozi. Mapafu hukosa oxygen.

Afrika maisha yetu ni ya kufanya maoezi muda wote. Si kwa kupenda ni lazima utembee kwakuwa huna nauli ya basi na Gari huna. Mapafu yanakuwa imara. Pia vyakula tunavyokula ni organic.
Ok kiongozi umeeleweka,lakini sio kutumwa kikohozi bali kupimwa kikohozi!!

Hehehehehe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aina ya hatari kufuta uhai wa aina fulani ya binadamu au wanyama.
Kwa mfano itokee aina fulani ya swara wamebaki kama mia na wanaishi kaeneo kadogo wote kwa pamoja, halafu kundi la simba lizingire hao swara, hapo ndio tunasema aina hiyo ya swara wapo kwenye "existential threat", maana watauawa wote, ifahamike simba hawatakua wakiua tu wawafanye msosi, ila wataua kila swara atakayepatikana hai.

Mfano mwingine ni ule uvamizi wa taifa la Israel kutoka kwa mataifa ya kiarabu, wale Waarabu hawakua wanakwenda kupigana na Israeli kijeshi, nia ilikua ni kuchinja chochote na yeyote mwenye damu ya Kiyahudi kama alivyofanya Hitler. Yaani chochote chenye hatari ya kufutwa kwenye ramani ya dunia ndio huwa tunasema kipo kwenya hatari ya "existential threat".

Kwa kifupi, Corona ina uwezo wa kutufuta Afrika maana inachofanya wenye uwezo zaidi yetu, unajiuliza hivi nini tunacho cha maana hadi ikatukwepa.
Kama ni kunawa mikono, wale wananawa mpaka basi, ilhali huku bado kuna vijiji na mitaa haina hata maji. Kama ni kuepuka misongamano, wale wamejifungia ndani kabisa, Afrika bado tunasongamana kwenye madaladala na madhehebu. Yaani tahadhari kwa wale zinachukuliwa za hali ya juu ila bado wanadondoka kwa maelfu, huku sisi tupo tupo tu, lakini anakufa mmoja baada ya mwezi.
Hiki ndio hata mimi najiuliza. Kwasababu tangu tupate wagonjwa Africa rate ya kufa sio kama Wao walivyopata wagonjwa w akwanza
 
Acha kuwa na negativity ?Wewe haujawahi kuchanjwa chanjo yeyote ?Bila chanjo wewe ungekufa kwa surua au ungeshaugua polio. Kwenye chanjo kuna protocols bwana.Acheni kupayuka payuka ujinga.
Mimi niliugua Surua,Tete kuwanga,mshipa wa ngiri,Kipindupindu,
Chanjo niliyopigwa ilikuwa ni ya Ndui na polio tu
Wakati huo dunia ilkuwa natu wachache na walikuwa serious katika kujilinda na maradhi ila hii dunia ya sasa ni vita ya kumalizana haswa kwetu yaani black race
Inasemekana tumekalia madini na utajiri ambao kuna watu wanautaka.
 
Sijui jamaa anayatafakari haya huko Chattle aliko
..!????
Kama ugali uko mezani kwake na kapewa nguvu na majeshi yote yanamtii hawezi kusikiliza mpaka atoke hapo aje uraiani
 
Tunavyovingapi kweli hivi? Twafaaaaaa
Ndo hicho hicho tu. Hapa kama ulikuwa haujui kusali inabidi uanze kusali. Mungu aingilie kati. Maana Alveolis zikishambuliwa ujue kwa heri
Ventilator moja mpo mia moja mnahitaji. Mungu ingilia kati.
 
Binadamu ana mucus kwenye njia ya hewa, hii ni sehemu ya kinga ya mwili. Hewa ikiingia na uchafu unakamatwa na mucus na uchafu ule unautoa kama kohozi.

Mucus goblets zikishambuliwa na virus ndiyo mafua yanachuruzika na huweza kukohoa. Maambukizi yakitokea kwenye mucus membrane husababisha kikohozi. Ndiyo maana unatumwa kikohozi ili wataalamu wagundue ni maambukizi gani.

Covid-19 hushambulia njia ya hewa na maambukizi huleta joto mpaka centi grade 38-39. Mucus goblets zinashambuliwa kwa kasi na Hutoa makohozi. Mapafu hukosa oxygen.

Afrika maisha yetu ni ya kufanya maoezi muda wote. Si kwa kupenda ni lazima utembee kwakuwa huna nauli ya basi na Gari huna. Mapafu yanakuwa imara. Pia vyakula tunavyokula ni organic.
Your theory might hold water but let's not get too excited on the African immunity. Tunahitaji kufanya tests zaidi for a conclusive interpretation of the results.
 
Mimi niliugua Surua,Tete kuwanga,mshipa wa ngiri,Kipindupindu,
Chanjo niliyopigwa ilikuwa ni ya Ndui na polio tu
Wakati huo dunia ilkuwa natu wachache na walikuwa serious katika kujilinda na maradhi ila hii dunia ya sasa ni vita ya kumalizana haswa kwetu yaani black race
Inasemekana tumekalia madini na utajiri ambao kuna watu wanautaka.
Tetekuwanga hata watoto mpaka leo wanaugua,uzuri hiyo sio fatal.Na ukiugua unakunywa panadol tu kupunguza homa wiki mbili unapona na hauugui tena. Ila kipindupindu umeniogopesha. Mimi Surua,tb,polio,menengitis,Hepatit B zote nimechanjwa. Ndui wakati nazaliwa walikuwa hawachanji tena. Ila mliochanjwa ndui mna maalama makubwa begani. Mweh 🤣🤣🤣
 
Chloroquine kama inatibu kwanini ifanyiwe utafiti ni tamaa tu ya makampuni ya dawa
 
Tetekuwanga hata watoto mpaka leo wanaugua,uzuri hiyo sio fatal.Na ukiugua unakunywa panadol tu kupunguza homa wiki mbili unapona na hauugui tena. Ila kipindupindu umeniogopesha. Mimi Surua,tb,polio,menengitis,Hepatit B zote nimechanjwa. Ndui wakati nazaliwa walikuwa hawachanji tena. Ila mliochanjwa ndui mna maalama makubwa begani. Mweh [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
duuh mkuu una miaka mingapi!?
hujachanjwa kwa bega?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo sahihi. Waafrica ni Mungu tu ndyo anatusaidia. Ila ukiangalia mazingira yetu, huu ugonjwa ungekuwa na nguvu kama ebola, bac tungeisha wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom