CNN: 'Don't use birth control,' Tanzania's President tells women in the country

Watoto huwa wanakuja na bahati zao wewe!!
 
Kaka huna cha kuwalisha basi usizae kabisa. Ila yeye kasema zaa tu ila uwalishe. Kama vipi kahasiwe kabisa.
 
Trump sio muungwana. Hajawahi kukiri uchizi wake ahdharani
 
Ukiangalia comments ndo unaelewa jinsi ambavyo kuna watu zero brain
 
Upuuzi gani kama mtu anakuambia chapa kazi na endelea kufyatua?Au humo kichwani mwako ni sifuri?Kama unapiga kazi it means utapata kipato kitakachoweza kuendesha maisha yako vizur,sasa kwanini usizae?Au unamattz ya uzaz hii kauli ya kuzaa imekukera?
 
Kwa huu utaratibu wa kuwekeza kwenye ndege badala ya kuwekeza kwenye uchumi na maisha ya watu wengi ili kuwepo na unafuu wa maisha, ni bora angekaa kimya kuhusu hilo swala maana hakuna mpango wowote wa ku handle hiyo population growth
 
Kaka huna cha kuwalisha basi usizae kabisa. Ila yeye kasema zaa tu ila uwalishe. Kama vipi kahasiwe kabisa.
Muombe sana Mungu akupe akili, unless unataka uwaziri.

Watoto hawahitaji kula tu. Japo chakula, malazi na mavazi ndio basic, lkn jamii yako inahitaji zaidi ya hayo. Usiwe na akili za kuku, kwamba ukizaa utalisha yataisha...kuna malezi pia. Huyu anayeadvocate watu wafyatue watoto tuuuuuu, ndio huyo huyo aliyeagiza binti zetu wakipata ujauzito wafukuzwe shuleni. Mimba za umri mdogo huchangiwa na ukosefu wa malezi pia.
 
Achana na sera ya Marekani unajua lkn sera yetu ya taifa ni ya uzazi wa mpango ambayo rais wake anaipinga, hata kama ana mawazo tofauti ilikuwa busara kutosema mbele ya kamera.
Kakuambia kama unachapa kazi kwann usizae?Hii kauli haieleweki?Jaman team kupinga kila kitu tafuteni hoja za mcng
 
This a shame to our nation, yoyote angesema lkn asingekua Raisi wetu, inaonyesha Raisi kwamba hana international exposure.
Mwenzio anakwambia kaishi kote Ulaya, Japan, Uchina na Marekani hakuna wa kumwambia kitu...na alipokuwa akiishi Canada alichaguliwa kuwa Co-chair wa Mawaziri wa Ardhi duniani, sasa jiulize iliwezekanaje hii, na hatujawahi kusikia alipokuwa Waziri aliishi Canada...Shock, horror!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kaka huna cha kuwalisha basi usizae kabisa. Ila yeye kasema zaa tu ila uwalishe. Kama vipi kahasiwe kabisa.
Thumbs up Mkuu. Kuna watu humu JF huwa wanachangia mada wakiwa hawajaelewa au hata kujisumbua kupata full story behind mada iliyoanzishwa. Kama mtu una akili timamu na umemsikiliza Mheshimiwa alichokisema mwanzo mwisho sidhani kama mtu anaweza kuwa na mawazo mgando kama yanayojionyesha hapa.

Kwa jinsi watu wanavyowahusudu wazungu miaka ijayo ukoloni unaweza kurudi tena tena Africa, maana ni kama kila kitu anachokisema mtu mweupe bila hata kukipima mtu anaruka nacho kama ndio standard of life. Wachina kwa sasa wana mpango wa kuachana na one child policy, mbona hatuwasikii wazungu wakiwakosoa! Ila kwa kua wanajua akili za kiafrika zilivyo jambo lolote likitoka kwetu wanaaamini wakiweka neno tu lazima wenyewe kwa wenyewe tugeukane bila hata kulitafakari.

Na haya maneno aliyoyasema Mh. Rais, kama yangesemwa na kiongozi mwingine wa taifa la ulaya au marekani hawa wanaosema tumeabishwa yamkini ndio wangekua wapiga debe wakuu kisa tu ngozi nyeupe imesema.

"kama unajimudu, na una uwezo wa kutunza na kuihudumia familia yako zaa kadiri uwezavyo" In Mr. President voice.
 
Tanzania na watanzania tuko huru na hatupangiwi na kiumbe yeyeto katika mambo tuliyopewa bure na Mwentezi Mungu. Trump kawakamata pabaya bado wanapata nguvu za kuikemea nchi yetu eti
 
Mna uwezo wa kuwatunza? hawa tulionao hata mkopo ya wanafunzi tumeshindwa kuwatimizia tumeanza kuwabagua kwa vigezo vya kozi.
Ukipitia vyuo vikuu siku hizi hadi huruma watoto wasio na mikopo wanapata shida kweli wanaishi maisha ya dhiki, mlo mmoja halafu ndiyo wengi sana zaidi ya nusu. Watoto wa kike ahueni yao ni kudanga na kujiuza, jaribu kupitia huko mavyuoni utashangaa. Tunakoelekea na watoto wa kiume soon wataanza kudanga kwa mashugar mami au kwa mabasha. Hivi tunajenga taifa la watu wa aina gani?

Tunaangalia tu idadi hatuangalii ubora? Hivi ukiwa na watoto kumi umeshindwa kuwalea wameishia kwenye ushoga,usagaji na kujiuza hapo umepata au umepatikana? Ndiyo pa kujilaumu bora ungekuwa na mmoja au wawili upunguze hasara na stress.
 
Hili la kuzaa ninaunga mkono hoja ya JPM.Russia na baadhi ya nchi za ulaya sasa hivi wapo katika kampeni ya kuongeza idaidi ya watu.Mwenye uwezo na azae kwa hata mungu alisema tuje kuijaza dunia.
 
Serikali imejipanga kiasi gani kuhandle hiyo population growth au ni ili mradi kufyatua tu. Kama asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 wamedumaa unajua implication yake kuhusu ukuaji wa hao watoto na uwezo wao wa kiakili wanapokuwa watu wazima? Serikali ina mpango wowote ku address haya maswala, au ni bora liende?
 
Wewe ndo umeona Mungu kakupa akili?

Unachanganya mada.. Hapa tunaongelea kuzaa Watoto kadili unavyoweza kuwalea.. Rais katoa maoni yake mi naona yanafaa kabisa. Kama unaweza kuwatunza zaa tu. Unataka nini Tena?

JPM hataki mimba za utotoni kwa hiyo wanao takiwa kuzaa ni kwenye umri sahihi? Usichanganye mambo kwa kujiona una akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…