CNN: 'Don't use birth control,' Tanzania's President tells women in the country

CNN: 'Don't use birth control,' Tanzania's President tells women in the country

Katika makala zote za nje hili neno uwa halisahauliki "bull dozer"
 
Kweli wewe ni kilaza kweli; what is intl exposure for without considering own nation's interest? Ninakushauri uwaulize wajapan na waswizi juu ya sera yao wa sasa ya kuongeza watu (kuzaliana). Waswahili mnasoma kwa kukariri, mnaishi kwa kukariri (intl exposure!) na kisha maisha yenu yanakuwa tainted na uwakala/kuwa vibaraka.
Haya JPM atasema anataka nguvu kazi haya wewe kajamba nani inakusaidia nini kuwa na watoto kumi? Au ile kuitwa baba kila upande ndiyo raha yako? Huyo JPM au serikali itakusaidia kuwasomesha wakati siku hizi mpaka wanafunzi wa udaktari wanakosa mikopo?
 
Lakini amesema kama unaweza kuzaa zaa maana hospitali na vituo vya afya vipo kwa ajili ya kutoa huduma ila kama huna uwezo kiuchumi punguza speed. Tatizo tu labda kuzungumzia issue ya uzazi wa mpango kwamba afagilii otherwise alichokisema ni moja ya msingi wa uzazi wa mpango ambao unasisitiza kuwa na familia ambayo unaimudu japokuwa watanzania wengi wanaamini kuwa na watoto wawili ama watatu ndio uzazi wa mpango kumbe hata mwenye watoto 6 kama ni maamuzi ya wazazi na wameona wana uwezo wa kumudu kuwahudumia bado ni uzazi wa mpango pia
Ewaaaaaa....ww unajua sana.....yaan baada ya watu kuambiwa uzazi wa mpango basi wanaona MTU akizaa watoto kumi na wote akawa na uwezo wa kuwapa huduma zote bhc wanahs hajatumia uzazi wa mpango!!! HV hakuna familia ambazo zina mtoto mmoja au wawili lkn wameshindwa kuwasomesha watoto hao?? Ilihali zpo pia familia zenye watoto sita na wamewapa mahtaj yao yote ya msng kama ipasavyo!!!
Inatakiwa ieleweke kuwa uzazi wa mpango sio kuzaa mtoto mmoja au wawili au kumi Bali n kuzaa idadi ya watoto utakaoweza kuwapa huduma zote za msng kama watoto ikiwemo chakula,mavazi,makazi,elimu ,afya na hata ajira ikiwezekana.
 
Swala jingine amezingatia uwezo wa mtu binafsi pekee, lakini hajaeleza mikakati ya serikali kuboresha huduma muhimu kama maji, afya, elimu, umeme, upatikanaji wa chakula na lishe bora, miundombinu kama barabara ambazo toka uhuru bado ziko katika kiwango cha chini kabisa huku kukiwa hakuna mipango inayoeleweka zaidi ya siasa za majitaka na upigaji wa hapa na pale kupewa kipaumbele
 
Harafu kitu kingine wasichokijua watu ni kuwa,Magu alisema kama huna uwezo wa kuwatunza na unaiona kabisa hali yako hairuhusu fanya uzazi wa mpango ila kama unauwezo wa kuwalea we zaa tu hata 100 kikubwa tu ni kuweka interval nzuri kati ya mtoto na mtoto
Magu anachokikataa ni kuwa sisi tunapewa uzazi wa mpango na tuko watu wachache wao wako wengi na idadi kubwa ya watu ni tool muhimu sana kwenye maendeleo hasa soko na nguvu kazi.......leo hii wanawake wengi wana kansa sababu ya madawa yao hayo ni bora hata wangesisitiza kwenye uzazi wa mpango wa asili usiotumia dawa
Sasa kama hali yako haikuruhusu kuwa na watoto wengi utatumia nini kama siyo kufuata uzazi wa mpango? Hivi mnajua mnachokipinga lakini au mnasapoti tu kwa kuwa aliyeongea ni Rais?

Mimi nilimfuatilia alisema hasapoti uzazi wa mpango hapo hapo anasema Kama una uwezo zaa tu it means usipokuwa na uwezo usizae sasa huo si ndiyo uzazi wa mpango wenyewe? Sasa akiambiwa hajielewi atasema anatukanwa?
 
Siyo mimi sikumsikiliza yeye bali yeye ndiyo hajataka kusikiliza kampeni ya uzazi wa mpango inataka nini. Uzazi wa mpango nia yake ni kila mtu azae watoto anaoweza kuwatunza kama una uwezo wa kutunza watoto 20 vizuri zaa tu. Sasa yeye anasema chapeni kazi na mfyatue watoto tu huu ni upuuzi, utazaaje bila kujipima na kujua uwezo wako wa kulea upoje? Na kwa mfano ukajua unauwezo wa watoto saba utazaaje saba bila usaidizi wa uzazi wa mpango je ukizidisha?

Tatizo hamjaelewa hata kampeni ya uzazi wa mpango ni nini, hatuwezi kuishi kwa kubahatisha tuenende kama mang'ombe sisi ni binadamu. Mungu ametupa utashi na Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu lazima tuwe na mpango mkakati katika kila jambo. We have to plan everything maisha yetu lazima yaende kwa mpangilio mimi nilishakataa watoto wa bahati mbaya na wa kushitukizwa najua lini napata mtoto na nani. Siyo umekutana na mwanamke huko hata haeleweki mimba tayari.
Kwani we hukumsikia alivyosema kuwa kama huna uwezo wa kuwatunza fanya uzazi wa mpango? Mkuu mbona unaongea kishabiki? Maana unayoyasema ndio aliyosema hata yeye,mi nakushangaa sana aisee!!
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

ELIMU ELIMU ELIMU. KNOWLEDGE IS POWER
Knowledge IS NOT Power. It is potential power. Effective application ya hiyo knowledge ndo power sasa. Jiwe ana PhD lakini sometimes ana behave kama akina Prof. Majimarefu
 
Mkuu waache wazae tutawaanzishia tuzo ya uzaaji bora.

Huwa najiuliza mtu mmoja watoto kumi ili iweje? Kwani ni sifa? Ukiuliza utaambiwa ooh wazazi wangu wasingezaa wengi nisingekuwepo so what? Usingekuwepo ungepungukiwa nini? Ushajiuliza wasiokuwepo wanashida ipi?

Tuacheni fujo zaa mtoto mmoja wawili au watatu wahudumie vizuri, enjoy maisha yako.
Kwa mtazamo wako nadhani uko sahihi na nakuunga mkono
 
Lakini amesema kama unaweza kuzaa zaa maana hospitali na vituo vya afya vipo kwa ajili ya kutoa huduma ila kama huna uwezo kiuchumi punguza speed. Tatizo tu labda kuzungumzia issue ya uzazi wa mpango kwamba afagilii otherwise alichokisema ni moja ya msingi wa uzazi wa mpango ambao unasisitiza kuwa na familia ambayo unaimudu japokuwa watanzania wengi wanaamini kuwa na watoto wawili ama watatu ndio uzazi wa mpango kumbe hata mwenye watoto 6 kama ni maamuzi ya wazazi na wameona wana uwezo wa kumudu kuwahudumia bado ni uzazi wa mpango pia
Ndiyo maana tunasema alijicontradict alichokiongea kwamba kama unauwezo zaa huo ndiyo msingi wa uzazi wa mpango mtu azae anaoweza kuwahudumia. Sasa nilishangaa hapo hapo anaongea hivyo halafu anasema hasapoti uzazi wa mpango hii inaonyesha jamaa hajajipa muda wa kuifahamu elimu ya uzazi hata kidogo anatumia commonsense kwenye vitu vya kitaalamu.
 
Hakuna baya lolote alilosema JPM maana hamna MTU atakayepangiwa azae watoto wangapi ila JPM alitoa tu maoni yake tatizo lenu nyie wakosoaji mligeuza Ile hotuba ajenda yenu ya kisiasa badala ya kuangalia uhalisia wa hotuba yenyewe.
Mimi huwa nampinga Jiwe mambo mengi sana karibu yote lkn akiongea vitu vya maana kama hivi lazima nimuunge mkono........jingine ambalo nishawahi muunga mkono ni la wanafunzi kuzaa wakiwa shule
 
Kwa hili niko na Magu kwasababu ukuangalia population yetu na eneo letu, nchi ina hitaji watu zaidi.
Chukua nchi kama Nigeria kieneo ni ndogo kwetu lkn ina idadi zaidi ya million 180 halafu sisi tuko million 55 tu.
NB: Mipango thabiti hitajika kwenye maeneo haya: Aridhi, elimu, afya. Na kulinda vyazo vya maji.
 
Sasa kama hali yako haikuruhusu kuwa na watoto wengi utatumia nini kama siyo kufuata uzazi wa mpango? Hivi mnajua mnachokipinga lakini au mnasapoti tu kwa kuwa aliyeongea ni Rais?

Mimi nilimfuatilia alisema hasapoti uzazi wa mpango hapo hapo anasema Kama una uwezo zaa tu it means usipokuwa na uwezo usizae sasa huo si ndiyo uzazi wa mpango wenyewe? Sasa akiambiwa hajielewi atasema anatukanwa?
Ndugu,mi huwa sio mshabikia wa kushabikia kila kitu ila suala lenye tija kwangu lazima niliunge mkono......unaposema eti huwezi kujua uzar au usizae maana we una shida pahala,uzazi wa mpango sio lazima mtu atumie vile vidonge au vipandikizi kuna njia nyingi tu za asilia zisizohitaji dawa za kemikali we kama hujui uliza usaidiwe au ukae kimya
Najua humu kuna wengi wenu mnapinga tu kwa sababu kasema Jiwe mwenyekiti wa ccm,hili ni tatizo kubwa sana kama nchi.
 
Wamezaa kumi ndiyo hawa watoto wao wanakimbilia mjini kuwa mahouse girl na mahouse boy, wengine ndiyo hawa ombaomba. Sasa mtu kama huyu anayeombaomba na watoto watano alikuwa na ulazima gani wa kuzaa? Angefunga kizazi akatulia zake angeonekana hajakamilika? Kama mtu huna uwezo wa kutunza na kuhudumia its better ufe bila mtoto kuzaa its not mandatory. Hata biblia inaposema enendeni duniani mkazaliane haimaanishi kila mtu lazima azae, ndiyo maana kuna manabii na mitume wengi tu walikufa bila watoto

Haya ni mambo ya sera ya nchi ambayo yanatakiwa yajadiliwe na serikali kwa pamoja na kupata makubaliano; badala ya haya tunayoyaona ambapo wizara inatekeleza sera ya mpango wa uzazi halafu Rais mbele ya waziri wa Afya, kwenye mkutano wa hadhara anatoa tamko kupinga sera inayotekelezwa na serikali yake! Matamko kama haya yanawapa wakati mgumu mawaziri kutimiza majukumu yao simply because JPM is seeking popularity!!!

Mimi sipingi uzazi wa mpango ila napinga jinsi unavyotekelezwa hapa nchini kwa kutumia madawa [ chemicals from pharmaceuticals] ambayo yana madhara makubwa kwa afya za wakina mama. Wananchi wahimizwe kutumia njia za asili ambazo hazina side effects.
 
Mimi ni mwafrika lkn nasema Afrika litabaki kuwa bara la giza kwa muda mrefu ujao unless tu change mentality thinking ya viongozi wetu kwamba wao ni kama miungu watu untouchables wanapokuwa madarakani.

Tutawalaumu tu wazungu lkn wenye matatizo ni sisi ngozi nyeusi. Hebu msome Trump uniambie anamekosea wapi kuhusu viongozi wetu wa Afrika.

=========!​
American President - Donald Trump explains his statement against Africans:

"If after 50 years of independence you have not built the necessary infrastructure for your people, are you humans?

"If you sit on gold, diamond, oil, manganese, uranium... and your people don't have food, are you humans?

"If to stay in power, you buy weapons from strangers to kill your own citizens, are you humans?

"If your only social project is to stay in power for life, are you being human?

"If you despise and shoot your own citizens like game, who will respect them?"

"if you take all resources meant for development of your country for personal property are you humans?

" if you leave your country healthcare unattended and treat yourself abroad are you humans?

"Until your leaders think less of themselves and more about your people. You are not human but animal.

"Mentality" itabadilika ingawa itachukua muda na ntafurahi ikiwa siku moja ikiwa wewe nawe utafurahia uafrika wako na kuanza kuona bara letu linapata nuru ya kuona kwamba maendeleo ni jambo muhimu kwa kila kaya.

Hawa viongozi ni binadamu kama wewe na mimi hivyo wana kasoro zao, lakini tupime zaidi KPI (key performance index) zao khasa kuhusu maendeleo kwa vitendo.

Lakini umewahi kumsikia Trump akimzungumzia raisi Magufuli tokea (yeye Trump) aingie madarakani?

Na unadhani hajaambiwa habari za Magufuli na majasusi wa Marekani?

Ni kwamba bado anachukulia kila kitu kiujumla bila kutathmini kila nchi na hatua zake za kimaendeleo kwa sababu Marekani bado ni taifa kubwa duniani na bado wanatupatia misaada.

Lakini siku akiulizwa kuhusu raisi Magufuli nna uhakika utamsikia Trump akimuelezea kwa fikra chanya kabisa kuliko alivyomwelezea Mugabe.

Hivyo vyombo vya habari vina uwezo wa kulisha habari zozote zile zikiwemo zile za kuhusu mabaya tu ya Afrika na hadhira yao ikaona ni kweli.

Vyenyewe bado vyaendeleza hiyo kasumba yao ya kuitazama Afrika kwa fikra zisizo za kuisifia kwa hata mazuri kidogo ambayo yanafaywa bali kuiponda kwa kutumia hata kauli moja tu ambayo wanaichukua na kuitengeneza kwa uzuri kabisa..

Wakiweka vichwa vyao vya habari ndani ya eneo la 18 ndo unaona sisi tunashambulia na kuchambua tutakavyo huku wengine wamevaa sanamu bila kufikiria kwa undani.
 
"Mentality" ibabadilika ingawa itachukua muda na ntafurahi ikiwa siku moja ikiwa wewe nawe utafurahia uafrika wako na kuanza kuona bara letu linapata nuru ya kuona kwamba maendeleo ni jambo muhimu kwa kila kaya.

Hawa viongozi ni binadamu kama wewe na mimi hivyo wana kasoro zao, lakini tupime zaidi KPI (key performance index) zao khasa kuhusu maendeleo kwa vitendo.

Lakini umewahi kumsikia Trump akimzungumzia raisi Magufuli tokea (yeye Trump) aingie madarakani?

Na unadhani hajaambiwa habari za Magufuli na majasusi wa Marekani?

Ni kwamba bado anachukulia kila kitu kiujumla bila kutathmini kila nchi na hatua zake za kimaendeleo kwa sababu Marekani bado ni taifa kubwa duniani na bado wanatupatia misaada.

Lakini siku akiulizwa kuhusu raisi Magufuli nna uhakika utamsikia Trump akimuelezea kwa fikra chanya kabisa kuliko alivyomwelezea Mugabe.

Hivyo vyombo vya habari vina uwezo wa kulisha habari zozote zile zikiwemo zile za kuhusu mabaya tu ya Afrika na hadhira yao ikaona ni kweli.

Vyenyewe bado vyaendeleza hiyo kasumba yao ya kuitazama Afrika kwa fikra zisizo za kuisifia kwa hata mazuri kidogo ambayo yanafaywa bali kuiponda kwa kutumia hata kauli moja tu ambayo wanaichukua na kuitengeneza kwa uzuri kabisa..

Wakiweka vichwa vyao vya habari ndani ya eneo la 18 ndo unaona sisi tunashambulia na kuchambua tutakavyo huku wengine wamevaa sanamu bila kufikiria kwa undani.
Sawa, kama tunajua wazungu wanatuangalia negatively kwanini sisi wenyewe tusiwe na tahadhari ya kuongea vitu controversial,

bado narudi kule kule rais asingeongea vile CNN wangeandika nini.
 
Sawa, kama tunajua wazungu wanatuangalia negatively kwanini sisi wenyewe tusiwe na tahadhari ya kuongeza vitu controversial,

bado narudi kule kule rais asingeongea vile CNN wangeandika nini.

Mimi nimeishi na kufanya kazi na wazungu miaka mingi sana Afrika na huko majuu na nawafahamu kwa uzuri kabisa.

Mwafrika kwa mzungu kila kitu unachofanya kwake yeye ni lazima kiwe ni 100/100.

Ukikosea siku moja hata kakosa kidogo tu, basi hiyo 100/100 wanaifuta na unakuwa yuleyule mwafrika wa kule porini wanakoamini siku zote hakuna waafrika wenye vipaji na akili.

Kwahio kinachofanyika hivi sasa ni kwamba hata kama KPI ya raisi Magufuli iko juu, wao wanachofanya ni kutafuta vikosa vidogovidogo na kuvikuuza kwa minajili ya kumshusha zile alama zake za nguvu anazoendelea kuzipata kwa mambo anayoifanyia Tanzania.

Hivyo tuwe tunaelewa hilo.
 
Watetezi wa Jiwe mtapata tabu sana kila siku kufanya damage control, tafuteni utaratibu wa kumuwahi kabla hajaropoka, ni jambo la kawaida maadui zake na vyombo vya habari vya nje vinachukulia hiyo loop hole kufanya propaganda.

Awali ya yote ni vema uwe na lugha ya heshima kwa Head of State...Acha kutumia lugha ya 'jiwe', 'kuropoka' dhidi ya Mkuu wa nchi...jenga hoja yako vizuri bila kutumia lugha ya udhalilishaji kwa kiongozi wa nchi....Hiyo ni moja na jambo la pili ni vizuri ujiongeze katika masuala ya uelewa wa issues wa namna dunia inavyokwenda...Birth control ina athari zake...na wazungu wana maana kubwa kupigania birth control kwa third world countries ukiacha 'kilio' chao cha kudhibiti umasikini...wana ajenda yao kubwa zaidi...
 
Back
Top Bottom