CNN, Sky news, Aljezeera, BBC, New York Times, Daily Mail, CBS, DW, Finacial Times vyaunga mkono hotuba ya Magufuli kuhusu Test kits

Kama sisi wote ni wanachama wa IMF kwanini tunabaguliwa? inamaana hadi tuwafurahishe ndio watusaidie? kwanza tuwafurahishe wao kama akina nani pumbaf hao, wabaki na hela zao kama wanadhani watazikwa nazo, shwain kabisa.
 
Mkuu wewe ni mtaalam wa maabara?


Sent from my iPhone using Tapatalk
Kiongozi mbona unahoji ikiwa mimi ni mtaalamu wa maabara wakati hoja yangu aihusiani na suala la maabara?! Unaonaje ukienda to the point?!
 
Wakati Wa Hotuba,rais Magufuri alidai mashine za kupimia virusi vya Corona zimehujumiwa na mabeberu katika kutoa majibu .Sio kwamba mabeberu hawamsikii wanamsikia matokeo yake ndio haya sasa.
Mkuu Chifu Kabi, hizo fedha za IMF na WB, japo zinatajwa kama assistance, sio grants,hizo ni mkopo na zimeombwa kama mkopo, zitalipwa na riba!. Sisi kwetu rais Magufuli amegoma kukopa, amewataka mabeberu kama wana nia njema, watusamehe riba au wasitishe marejesho ya mikopo hadi janga la Corona lipite.

Hii fursa ya IMF na WB kukopa tuliisema humu jukwaani kitambo

P
 
Ngoja nafasi tufatilie hivyo vyomb vya habari visemavyo na jinsi wanavyojadoli..

Sent using Jamii Forums mobile app
Short and clear, HAKUNA media yoyote kati ya hizo iliyomuunga mkono JPM! Zote zimeripoti alichoongea JPM; na pekee kilichoongozewa mbali na liyoongea JPM ni jinsi watu wanavyo-criticize suala zima la ufichaji takwimu, na jinsi Afrika ilivyo na maambukizi madogo huku waki-conclude vile vile kuna low testing level

Na kingine ni jinsi inavyoonekana tusivyo serious kulinganisha na majirani! In short, ukisoma katikati ya mstari utaona kilichopo ni kejeli kwa JPM kuliko kumuunga mkono!
 
Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake!
Tuache utani jamani hata Mungu anaona Mungu jeshi kubwa la wajinga lipo Chadema....kama unabisha muulize Silinde.
 
Ujinga ni kipaji pia!!


Pole kwa kujitambua, alkadhalika, wewe si mjinga kama unavyojihisi maana mjinga hajijuwi...yeye hubisha tu hata kama hajuwi anachobishia ni nini. Ipo siku utakuwa. By the way, hivi ulisikiliza ile hotuba ya Magufuli na kuielewa?
 
Tuache utani jamani hata Mungu anaona Mungu jeshi kubwa la wajinga lipo Chadema....kama unabisha muulize Silinde.
Subiri Magu zichemke halafu aibuke tena na kutangaza kinyesi cha nguruwe kinatibu corona; kisha subiri mwitikio na tafakari mwenyewe ni nani ana Jeshi Kubwa la Wajinga!!

Watu wataibuka hapa "ukila kitimoto hata mashetani hayakufuati..."! Ku-justify hoja ya Magu wataleta habari za kufikirika za kitimoto na majini wakati Magu kaongelea kinyesi cha kitimoto!
 
Hilo akilisikia hata shehe mkuu wa dalisalamu ataunga mkono.
Atatafuta hadi aya za kusapoti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu hiyo habari ya Nyerere kuandikwa na hao waandishi wa Kimagharibi, ingawa siijui na wala sijaiona na kuisoma, yawezekeana Mzee Sozigwa yeye ndivyo alivyoitafsiri ama kuipokea, wakati hao waandishi wala hawakuwa na nia ya kutoa ‘backhanded compliment’.

Kama hao waliomhoji Nyerere walikuwa ni waandishi wa habari [journalists] na si watu wa kuandika ma op-eds, walichotakiwa kukifanya ni kuandika kile walichokiona na kile alichokisema mhojiwa.

Zaidi ya hapo, kama nia yao ilikuwa ni kutoa ‘backhanded compliment’, basi hawakuwa ni waandishi wa habari kwa sababu kuingiza hisia, maoni, na mitazamo yao katika andiko lao ni kukiuka miiko ya taaluma ya uanahabari.

Sasa habari inapoandikwa, wasomaji wanaweza wakaipokea kwa mitazamo tofauti sana. Si ajabu Mzee Sozigwa aliipokea vile alivyoipokea kwa sababu hao waandishi walitoka Magharibi. Na enzi za Nyerere sisi tulikuwa wajamaa. Kuna uwezekano Sozigwa aliisoma hiyo habari huku akiwa na preconceived notions zake dhidi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi. Habari hiyo hiyo ingeandikwa na waandishi toka ITAR-TASS au Xinhua, si ajabu angeweza kuisoma kupitia prism tofauti kabisa.

Kama sijakosea, nakumbuka umewahi kutoa stori moja humu enzi bado ukiwa shule ya upili. Stori inahusu wewe kuagana na mshikaji na kumwambia kwamba utampigia baadaye ukifika nyumbani.

Wakati unasema hivyo, waliokuwepo karibu yako wakakusikia. Mmoja wao akaona kama vile unajidai eti kwenu kuna simu. Kwa maelezo yako, wewe lengo lako wala halikuwa kufanya ubishoo wa kuwa mna simu nyumbani kwa sababu kwako simu haikuwa big deal kivile na wala hukuwa na lengo kujionyesha. Wewe ulisema tu utampigia simu mshikaji ukifika nyumbani.

Unadhani ni kwa nini mmoja wao [unaweza kunisahihisha kama nimekosea] alikumaindi ilhali wewe wala hukuwa na nia mbaya [kwa mujibu wako]?

Binadamu huwa tuna tabia ya kupokea kwa namna tofauti mambo yanayotuhusu kutegemea na hayo mambo yamesemwa au kuandikwa na nani.

Mimi hapa mara moja moja huwa napenda kuandika ‘USA baby’ kiutani. Ila kuna watu huwa wanaona kuwa eti nawaringishia. Wewe ukisema upo Gotham unabeba boksi Wall Street, mimi wala sioni kama unafanya mashauzi. Naona kawaida. Lakini wanaokereka na kuona kuwa unajidai, wapo!!

Kwa hiyo inawezekana kabisa labda Mzee Sozigwa aliitafsiri vibaya tu hiyo habari.....
 
Umenikumbusha mbali sana na hiyo stori ya mchizi wangu, ni yeye mwenyewe niliyemwambia nitampigia simu alinifuata akaniambia "we mbona unaharibu, oale kuna watu kwao wanaona simu kitu cha fahari sana halafu wewe unaongea kama utanipigia tu tupige story?

Kuhusu Sozigwa na backhanded compliment, inawezekana ali politicize, inawezekana alibaini mambo muhimu.

Lakini, kuhusu Magufuli, sidhani kwamba rahisi kujigamba kapima mapapai na mafenesi kwenye kipimo cha Covid-19 ni jambo la kusifia.

Kwanza kawavuruga watu kichizi, rais unaposema hizi tests mbovu, unatakiwa kuwapa watu alternative ya hizi test nzuri tumieni. Au tunaweka wanamaabara wazuri zaidi. Yeye kavuruga tu.

Mpaka kawapa sababu Wakenya wanakataa kuingiza ng'ombe wa Tanzania Kenya, wanasema mifugo ya Tanzania imepimwa na Magufuli na kukutwa na Covid-19. By the way kuna domestic cats wanepimwa wamekuwa wana hivi virusi.

Rais hata kama ana fanya uhakiki wa hizi testing procedures, anatakiwa kufanya methodically, kwa njia ambayo haitaleta mtafaruku, ananyata polepole, anaweka mtego, anagundua udhaifu, anauindoa udhaifu, anatangaza habari wakati kashamaliza kazi.

Siyo huyu anabwatuka tu, mara mabeberu, mara vipimo vibovu, mara kaugonjwa, anaonekana anataka ku confuse watu tu kwa kuwa hana mpango thabiti wa kukabiliana na janga hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…