Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi mbona unahoji ikiwa mimi ni mtaalamu wa maabara wakati hoja yangu aihusiani na suala la maabara?! Unaonaje ukienda to the point?!Mkuu wewe ni mtaalam wa maabara?
Sent from my iPhone using Tapatalk
Mkuu Chifu Kabi, hizo fedha za IMF na WB, japo zinatajwa kama assistance, sio grants,hizo ni mkopo na zimeombwa kama mkopo, zitalipwa na riba!. Sisi kwetu rais Magufuli amegoma kukopa, amewataka mabeberu kama wana nia njema, watusamehe riba au wasitishe marejesho ya mikopo hadi janga la Corona lipite.Wakati Wa Hotuba,rais Magufuri alidai mashine za kupimia virusi vya Corona zimehujumiwa na mabeberu katika kutoa majibu .Sio kwamba mabeberu hawamsikii wanamsikia matokeo yake ndio haya sasa.
Short and clear, HAKUNA media yoyote kati ya hizo iliyomuunga mkono JPM! Zote zimeripoti alichoongea JPM; na pekee kilichoongozewa mbali na liyoongea JPM ni jinsi watu wanavyo-criticize suala zima la ufichaji takwimu, na jinsi Afrika ilivyo na maambukizi madogo huku waki-conclude vile vile kuna low testing levelNgoja nafasi tufatilie hivyo vyomb vya habari visemavyo na jinsi wanavyojadoli..
Sent using Jamii Forums mobile app
Tuache utani jamani hata Mungu anaona Mungu jeshi kubwa la wajinga lipo Chadema....kama unabisha muulize Silinde.Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake!
Ujinga ni kipaji pia!!
Subiri Magu zichemke halafu aibuke tena na kutangaza kinyesi cha nguruwe kinatibu corona; kisha subiri mwitikio na tafakari mwenyewe ni nani ana Jeshi Kubwa la Wajinga!!Tuache utani jamani hata Mungu anaona Mungu jeshi kubwa la wajinga lipo Chadema....kama unabisha muulize Silinde.
Hilo akilisikia hata shehe mkuu wa dalisalamu ataunga mkono.Subiri Magu zichemke halafu aibuke tena na kutangaza kinyesi cha nguruwe kinatibu corona; kisha subiri mwitikio na tafakari mwenyewe ni nani ana Jeshi Kubwa la Wajinga!!
Watu wataibuka hapa "ukila kitimoto hata mashetani hayakufuati..."! Ku-justify hoja ya Magu wataleta habari za kufikirika za kitimoto na majini wakati Magu kaongelea kinyesi cha kitimoto!
Ujinga ni kipaji pia!!
Kuhusu hiyo habari ya Nyerere kuandikwa na hao waandishi wa Kimagharibi, ingawa siijui na wala sijaiona na kuisoma, yawezekeana Mzee Sozigwa yeye ndivyo alivyoitafsiri ama kuipokea, wakati hao waandishi wala hawakuwa na nia ya kutoa ‘backhanded compliment’.Kuna kipindi, wakati wa utawala wa Nyerere, rais Nyerere alifanyiwa mahojiano na gazeti moja la magharibi.
Waandishi walikaribishwa Msasani, wakapewa juisi, wakakaa na Mwalimu Nyerere, wakamuhoji.
Basi wakarudi kwao, wakaandika mahojiano.
Kama kawaida yao wenzetu, wakiandika habari hawaandiki alichosema waliyemuhoji tu, wanaandika mpaka jinsi alivyokuwa amekaa, mazingira ya mahojiano, wanakupa picha unaona kama upo kwenye mahojiano.
Basi wakandika kwamba Mwalimu Nyerere ni mtu wa watu sana, anaishi maisha ya kawaida sana, hata wafanyakazi wake wanavaa kawaida sana, na hata juisi waliyokaribishwa ilikuwa ya kawaida sana, haikuwa hata ya baridi.Kweli Nyerere ni kiongozi asiye na makuu.
Watu wakawa wameifurahia sana ile habari, wakasema Nyerere kasifiwa sana na gazeti hili la Magharibi.
Akaja mtu mwenye jicho la tatu, Mzee wangu Paulo Sozigwa, mtaalamu wa mambo ya habari. Akawakuta watu wanaifurahia ile habari.
Marehemu Mzee Paulo Sozigwa alikuwa mbobezi wa mambo ya habari, na muandishi wa habari wa rais siku hizo. Akaisoma ile habari, akawaamsha waliofurahi.
Akasema mnafurahia nini? Nyerere katukanwa kwa style inaitwa "tongue-in-cheek" hapa.
Wakamuuliza, hiyo style ya "tongue-in-cheek" ndiyo ikoje?
Akawaambia ni style ambayo mtu anakupa "backhanded compliment".
Vijana wakamwambia, sasa Mzee unatuchanganya zaidi, hiyo "backhanded compliment" ndiyo ikoje?
Akasema hiyo style ni pale mtu anapoonekana kama anakusifia, kwa kumsoma kijuujuu, lakini ukimsoma kwa undani unaona kakutukana.Hawa watu wamemsema rais wetu hajui hata kupokea wageni, watumishi wake hawajui kuvaa, na juisi ya nyumbani kwake hata haina ubaridi, kwamba sisi hatuna ustaarabu hata wa kupokea wageni, mpaka nyumbani kwa rais.
Watu wakasema "kweeeeeliiii Mzee Sozigwa".
Sasa, na leo tusije kufurahia habari za "backhanded compliment" inayotolewa "tongue-in-cheek".
Tests za Covid-19 zina matatizo dunia nzima, vipimo vinapima virus mpya.Kuna kipimo cha Mchina India wanakilalamikia kinatoa majibu feki 95%. So vipimo vina matatizo.
Lakini.
Magufuli anaweza kuwa anakejeliwa kwa kupima mapapai kwenye kipimo cha Covid-19, halafu washabiki wake wakawa wanachekelea.
Nataka kuwakumbusha kusoma kwa makini kama alivyotukumbusha Mzee Paulo Sozigwa.
Umenikumbusha mbali sana na hiyo stori ya mchizi wangu, ni yeye mwenyewe niliyemwambia nitampigia simu alinifuata akaniambia "we mbona unaharibu, oale kuna watu kwao wanaona simu kitu cha fahari sana halafu wewe unaongea kama utanipigia tu tupige story?Kuhusu hiyo habari ya Nyerere kuandikwa na hao waandishi wa Kimagharibi, ingawa siijui na wala sijaiona na kuisoma, yawezekeana Mzee Sozigwa yeye ndivyo alivyoitafsiri ama kuipokea, wakati hao waandishi wala hawakuwa na nia ya kutoa ‘backhanded compliment’.
Kama hao waliomhoji Nyerere walikuwa ni waandishi wa habari [journalists] na si watu wa kuandika ma op-eds, walichotakiwa kukifanya ni kuandika kile walichokiona na kile alichokisema mhojiwa.
Zaidi ya hapo, kama nia yao ilikuwa ni kutoa ‘backhanded compliment’, basi hawakuwa ni waandishi wa habari kwa sababu kuingiza hisia, maoni, na mitazamo yao katika andiko lao ni kukiuka miiko ya taaluma ya uanahabari.
Sasa habari inapoandikwa, wasomaji wanaweza wakaipokea kwa mitazamo tofauti sana. Si ajabu Mzee Sozigwa aliipokea vile alivyoipokea kwa sababu hao waandishi walitoka Magharibi. Na enzi za Nyerere sisi tulikuwa wajamaa. Kuna uwezekano Sozigwa aliisoma hiyo habari huku akiwa na preconceived notions zake dhidi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi. Habari hiyo hiyo ingeandikwa na waandishi toka ITAR-TASS au Xinhua, si ajabu angeweza kuisoma katika prism tofauti kabisa.
Kama sijakosea, nakumbuka umewahi kutoa stori moja humu enzi bado ukiwa shule ya upili. Stori inahusu wewe kuagana na mshikaji na kumwambia kwamba utampigia baadaye ukifika nyumbani.
Wakati unasema hivyo, waliokuwepo karibu yako wakakusikia. Mmoja wao akaona kama vile unajidai eti kwenu kuna simu. Kwa maelezo yako, wewe lengo lako wala halikuwa kufanya ubishoo wa kuwa mna simu nyumbani kwa sababu kwako simu haikuwa big deal kivile na wala hukuwa na lengo kujionyesha. Wewe ulisema tu utampigia simu mshikaji ukifika nyumbani.
Unadhani ni kwa nini mmoja wao [unaweza kunisahihisha kama nimekosea] alikumaindi ilhali wewe wala hukuwa na nia mbaya [kwa mujibu wako]?
Binadamu huwa tuna tabia ya kupokea kwa namna tofauti mambo yanayotuhusu kutegemea na hayo mambo yamesemwa au kuandikwa na nani.
Mimi hapa mara moja moja huwa napenda kuandika ‘USA baby’ kiutani. Ila kuna watu huwa wanaona kuwa eti nawaringishia. Wewe ukisema upo Gotham unabeba boksi Wall Street, mimi wala sioni kama unafanya mashauzi. Naona kawaida. Lakini wanaokereka na kuona kuwa unajidai, wapo!!
Kwa hiyo inawezekana kabisa labda Mzee Sozigwa aliitafsiri vibaya tu hiyo habari.....
Sema angalia pia usije ukawa wewe ndio mjinga maana....Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake!