Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Zero ni kwako wewe na huo ni uhuru wako wa kikatiba. Wapo wanaona mengi ya maana anayoyafanya.Na ni hao ndio wanaosema "hana uwezo wa kuaongoza"; lakini badala ya kuwaruhusu wamwonyeshe kuwa hana uwezo, badala yake kila njia zinatumika kulazimisha yeye kuendelea kuwepo kwenye uongozi bila ya ridhaa yao.
Wewe hili hulioni?
Nimekwisha kueleza mara kadhaa sasa kuhusu hili: hicho "kipande cha mkate" kina manufaa gani kama uhai wenyewe upo mashakani?
Hiyo miradi unayo kimbilia kila mara, yeye hana lolote huko. Awepo, asiwepo, bado miradi inge endelea tu; tena pengine kwa ufanisi zaidi.
Ni kama umezaliwa jana, kwamba hukumbuki haya maswala ya kilimo yanako tokea? Au unadhani watu wote hawajui/hawafuatilii yanayotokea hapa nchini miaka yote?
Kwa ufupi, Samia tokea aingie ni zero; na mbaya zaidi ni kuzidisha hali ya kunadisha nchi hovyo hovyo; kama alivyo fanya na Bandari; na sasa anaelekea kwenye Gesi na mali asili nyinginezo.
Kazi ya kuwageuza waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao, hilo ndilo atapaswa kulijibu tokea sasa na kuendelea.
Huwezi ukasema kisa mauaji ya Kibao ndio SSH hana uwezo. Wakati wa JPM walikufa wengi sana huko MKIRU na Coco Beach, maiti zilikuwa zikiokotwa kila kukicha, nani aliyesema kuwa JPM hana uwezo wa kuongoza nchi kisa vifo vilionekana kuizidi nguvu mamlaka ya nchi?.
Tatizo lako mengi huyajui na wanaoyajua wanaujua uwezo wake kwa kina upo vipi.
Suala la bandari ndio hujui lolote masikini ya Mungu, tafuta taarifa za utendaji wa TPA kwa mwaka huu halafu linganisha na miaka iliyopita, kwa taarifa yako TPA ndio bandari inayoongoza kwa ufanisi hivi sasa Afrika Mashariki.
Chuki inausumbua ubongo wako na hayupo wa kukusaidia. Ulianza kipindi kile kwa kurusha hewani kile kipindi na yule mwanasheria wako uchwara wa Kenya ukiupinga uwekezaji bila ya kujua kwa kina hiyo TPA inafanya vipi kazi, bila ya kujua kwa kina hizo sheria za kimataifa zilizosainiwa kwenye huo mkataba zinafanya vipi kazi, kisa ni roho mbaya tu inakusumbua.
Samia Mungu akipenda tunae mpaka 2030.