Code zinaanza kufunguka

Code zinaanza kufunguka

Na ni hao ndio wanaosema "hana uwezo wa kuaongoza"; lakini badala ya kuwaruhusu wamwonyeshe kuwa hana uwezo, badala yake kila njia zinatumika kulazimisha yeye kuendelea kuwepo kwenye uongozi bila ya ridhaa yao.
Wewe hili hulioni?
Nimekwisha kueleza mara kadhaa sasa kuhusu hili: hicho "kipande cha mkate" kina manufaa gani kama uhai wenyewe upo mashakani?
Hiyo miradi unayo kimbilia kila mara, yeye hana lolote huko. Awepo, asiwepo, bado miradi inge endelea tu; tena pengine kwa ufanisi zaidi.
Ni kama umezaliwa jana, kwamba hukumbuki haya maswala ya kilimo yanako tokea? Au unadhani watu wote hawajui/hawafuatilii yanayotokea hapa nchini miaka yote?

Kwa ufupi, Samia tokea aingie ni zero; na mbaya zaidi ni kuzidisha hali ya kunadisha nchi hovyo hovyo; kama alivyo fanya na Bandari; na sasa anaelekea kwenye Gesi na mali asili nyinginezo.
Kazi ya kuwageuza waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao, hilo ndilo atapaswa kulijibu tokea sasa na kuendelea.
Zero ni kwako wewe na huo ni uhuru wako wa kikatiba. Wapo wanaona mengi ya maana anayoyafanya.

Huwezi ukasema kisa mauaji ya Kibao ndio SSH hana uwezo. Wakati wa JPM walikufa wengi sana huko MKIRU na Coco Beach, maiti zilikuwa zikiokotwa kila kukicha, nani aliyesema kuwa JPM hana uwezo wa kuongoza nchi kisa vifo vilionekana kuizidi nguvu mamlaka ya nchi?.

Tatizo lako mengi huyajui na wanaoyajua wanaujua uwezo wake kwa kina upo vipi.

Suala la bandari ndio hujui lolote masikini ya Mungu, tafuta taarifa za utendaji wa TPA kwa mwaka huu halafu linganisha na miaka iliyopita, kwa taarifa yako TPA ndio bandari inayoongoza kwa ufanisi hivi sasa Afrika Mashariki.

Chuki inausumbua ubongo wako na hayupo wa kukusaidia. Ulianza kipindi kile kwa kurusha hewani kile kipindi na yule mwanasheria wako uchwara wa Kenya ukiupinga uwekezaji bila ya kujua kwa kina hiyo TPA inafanya vipi kazi, bila ya kujua kwa kina hizo sheria za kimataifa zilizosainiwa kwenye huo mkataba zinafanya vipi kazi, kisa ni roho mbaya tu inakusumbua.

Samia Mungu akipenda tunae mpaka 2030.
 
Samia Mungu akipenda tunae mpaka 2030.
Huo utakuwa muujiza wa kishetani; na sina hakika kama kweli Mungu anaweza kuliadhibu taifa hili kwa namna hiyo.

Samia siyo kiongozi, ni kinyago tu kilichowekwa hapo na watu wanaofaidika kwa uwepo wa kinyago hicho, watu wa aina yako. Lakini pamoja na ubovu iliofikia CCM sasa hivi; baadhi ya watu waliomo ndani ya chama hicho ambao wanaona taifa linavyo didimizwa na huyu mwanamke, hata wao wameanza kustuka. Kwa hiyo hiyo 2030 sahau kabisa. Mkilazimisha huko, kutakuwa na njia zingine za kumzuia huyu kuendelea kulinajisi taifa hili.

Hapa hakuna swala la kumchukia Samia kama binaadam. Kinacho chukiwa ni udhaifu wake, ukosefu wa kuwa na sifa za uongozi. Nchi inayumba tu, hakuna msimamo thabiti ya mwelekeo unaojenga imani za watu kwake.
Ulianza kipindi kile kwa kurusha hewani kile kipindi na yule mwanasheria wako uchwara wa Kenya ukiupinga uwekezaji bila ya kujua kwa kina hiyo TPA inafanya vipi kazi, bila ya kujua kwa kina hizo sheria za kimataifa zilizosainiwa kwenye huo mkataba zinafanya vipi kazi, kisa ni roho mbaya tu inakusumbua.
Huyu unaye mzungumzia hapa simjui, na wala hicho "kipindi" sijui ni kitu gani unakizungumzia wewe. Msije mkaenda kumteka mtu wa watu bure asiye husika na chochote. Kama una tatizo lingine naye huyo mtu, mweleze moja kwa moja, kwa vile unamfahamu. Usije ukachukuwa ya huku JF na kumsingizia yeye.

Ni hivi: uwepo wa Samia katika nafasi hiyo ya uongozi tayari ni balaa kwa Tanzania; kamwe haiwezekani kuendelea na balaa lile lile kwa zaidi ya 2025. Haiwezekani.
 
Huo utakuwa muujiza wa kishetani; na sina hakika kama kweli Mungu anaweza kuliadhibu taifa hili kwa namna hiyo.

Samia siyo kiongozi, ni kinyago tu kilichowekwa hapo na watu wanaofaidika kwa uwepo wa kinyago hicho, watu wa aina yako. Lakini pamoja na ubovu iliofikia CCM sasa hivi; baadhi ya watu waliomo ndani ya chama hicho ambao wanaona taifa linavyo didimizwa na huyu mwanamke, hata wao wameanza kustuka. Kwa hiyo hiyo 2030 sahau kabisa. Mkilazimisha huko, kutakuwa na njia zingine za kumzuia huyu kuendelea kulinajisi taifa hili.

Hapa hakuna swala la kumchukia Samia kama binaadam. Kinacho chukiwa ni udhaifu wake, ukosefu wa kuwa na sifa za uongozi. Nchi inayumba tu, hakuna msimamo thabiti ya mwelekeo unaojenga imani za watu kwake.
Huyu unaye mzungumzia hapa simjui, na wala hicho "kipindi" sijui ni kitu gani unakizungumzia wewe. Msije mkaenda kumteka mtu wa watu bure asiye husika na chochote. Kama una tatizo lingine naye huyo mtu, mweleze moja kwa moja, kwa vile unamfahamu. Usije ukachukuwa ya huku JF na kumsingizia yeye.

Ni hivi: uwepo wa Samia katika nafasi hiyo ya uongozi tayari ni balaa kwa Tanzania; kamwe haiwezekani kuendelea na balaa lile lile kwa zaidi ya 2025. Haiwezekani.
Uwepo wa mtu yoyote ni balaa kwa taifa kama hufanyi kazi, huna elimu na huna ubunifu wowote ule kichwani.

Naamini yoyote atakayekuwepo pale ikulu kwako na wa aina yako ni lazima watamuona ni balaa na hafai, ndio watanzania wengi tulivyo, tumechanganyikiwa, misingi yetu ya kielimu ni duni na haraka sana tunakimbilia kudhania kwamba aliyepo ikulu ndio tatizo.

Tatizo lipo ndani ya misingi yetu ya kitaifa, ukikosa maandalizi ya elimu yenye kuhusisha ubunifu ni lazima kila Rais aonekane ni mbaya tu kumbe ubaya ni vichwa vyetu wenyewe.

Kumbuka pia kwamba Samia amekuwa Rais kwa sababu ya kifo cha JPM, lakini wasaidizi wote wa hayati na misingi ya kisera aliyoiacha bado inaiongoza TZ, hivyo kulialia kwako na wengine wa aina yako ni tabia ambayo imekuwepo tangu awamu zilizotangulia.

Kwa wenye hekima na busara, hawawezi kunyimwa usingizi kwa namna yoyote ile na fikra kama hizi za kwako.
 
Naamini yoyote atakayekuwepo pale ikulu kwako na wa aina yako ni lazima watamuona ni balaa na hafai, ndio watanzania wengi tulivyo, tumechanganyikiwa, misingi yetu ya kielimu ni duni na haraka sana tunakimbilia kudhania kwamba aliyepo ikulu ndio tatizo.
Kama wewe kipimo chako ni Samia; sina shaka yoyote viongozi hao watakuwa ni balaa kwa nchi yetu; na Mungu apishie mbali kabisa tusije tukampata kiongozi mwingine mbovu kama huyu. Sio ubovu wa kutokuwa na sifa ya uongozi pekee, lakini Samia ni hatari kubwa kwa nchi kwa mwelekeo wa uwafubaza waTanzania wajione kuwa hawafai, hawana uwezo mbele za watu wengine.
Kiongozi wa aina hiii ni balaa kubwa kwa nchi yoyote; ndizo nchi kama Haiti kwa mfano.

Na unapozungumzia elimu ya baadhi ya waTanzania, na hasa wengi sasa wanao ongoza CCM, Samia ni Sampuli nzuri sana ya kuwaelezea watu hao. Elimu aliyo nayo kiongozi huyu, kama kweli anayo, na aliipata alipokuwa huko vyuoni, ni kielelezo tosha kabisa cha ubovu huo.
Katika hili la "elimu" inanilazimu kabisa nikubaliane na wewe kuhusu ubovu wa elimu yetu. Matokeo yake ndiyo haya tunayo yaona kila siku, siyo huko serikalini pekee, ila sasa ni kila sehemu; hadi humu JF. Huhitaji kwenda mbali kujua ubovu huo wa elimu katika nchi hii.
Na hili ni moja ya sababu moja kuu ya kuwapata viongozi wa aina hii ya Samia.
Uwepo wa mtu yoyote ni balaa kwa taifa kama hufanyi kazi, huna elimu na huna ubunifu wowote ule kichwani.
Tanganyika ilipo pata uhuru wake, tatizo hilo la "elimu" lilitambuliwa kuwa adui mkubwa, na ililazimu kupambana na adui huyo kwa nguvu zote. Kama leo hii, na viongozi tulio nao sasa, bado tunakubali kumrudisha adui ambaye kwa kiasi kikubwa tulikuwa tume mshinda, utashindwa vipi kujuwa tatizo linapo anzia, badala ya kuwalaumu waTanzania kiujumla jumla kama unavyo fanya hapa. Ujinga wa waTanzania ndio imekuwa kinga muhimu ya viongozi hawa wabovu. Badala ya kuelekeza lawama kunako husika, unaielekeza kwa wahanga wa ubovu huo?
Kumbuka pia kwamba Samia amekuwa Rais kwa sababu ya kifo cha JPM, lakini wasaidizi wote wa hayati na misingi ya kisera aliyoiacha bado inaiongoza TZ, hivyo kulialia kwako na wengine wa aina yako ni tabia ambayo imekuwepo tangu awamu zilizotangulia.
Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo Samia hastahili kabisa kubaki madarakani baada ya kumaliza hiyo ngwe ya balaa lililo ikumba nchi yetu.
 
Kama wewe kipimo chako ni Samia; sina shaka yoyote viongozi hao watakuwa ni balaa kwa nchi yetu; na Mungu apishie mbali kabisa tusije tukampata kiongozi mwingine mbovu kama huyu. Sio ubovu wa kutokuwa na sifa ya uongozi pekee, lakini Samia ni hatari kubwa kwa nchi kwa mwelekeo wa uwafubaza waTanzania wajione kuwa hawafai, hawana uwezo mbele za watu wengine.
Kiongozi wa aina hiii ni balaa kubwa kwa nchi yoyote; ndizo nchi kama Haiti kwa mfano.

Na unapozungumzia elimu ya baadhi ya waTanzania, na hasa wengi sasa wanao ongoza CCM, Samia ni Sampuli nzuri sana ya kuwaelezea watu hao. Elimu aliyo nayo kiongozi huyu, kama kweli anayo, na aliipata alipokuwa huko vyuoni, ni kielelezo tosha kabisa cha ubovu huo.
Katika hili la "elimu" inanilazimu kabisa nikubaliane na wewe kuhusu ubovu wa elimu yetu. Matokeo yake ndiyo haya tunayo yaona kila siku, siyo huko serikalini pekee, ila sasa ni kila sehemu; hadi humu JF. Huhitaji kwenda mbali kujua ubovu huo wa elimu katika nchi hii.
Na hili ni moja ya sababu moja kuu ya kuwapata viongozi wa aina hii ya Samia.
Tanganyika ilipo pata uhuru wake, tatizo hilo la "elimu" lilitambuliwa kuwa adui mkubwa, na ililazimu kupambana na adui huyo kwa nguvu zote. Kama leo hii, na viongozi tulio nao sasa, bado tunakubali kumrudisha adui ambaye kwa kiasi kikubwa tulikuwa tume mshinda, utashindwa vipi kujuwa tatizo linapo anzia, badala ya kuwalaumu waTanzania kiujumla jumla kama unavyo fanya hapa. Ujinga wa waTanzania ndio imekuwa kinga muhimu ya viongozi hawa wabovu. Badala ya kuelekeza lawama kunako husika, unaielekeza kwa wahanga wa ubovu huo?
Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo Samia hastahili kabisa kubaki madarakani baada ya kumaliza hiyo ngwe ya balaa lililo ikumba nchi yetu.
Magufuli alikuwa na sifa zote za kuitwa mzalendo lakini ni sisi humu jukwaani tuliomletea dharau za kila aina. Hata Malaika wakiletwa na Mungu waje kuongoza Tanzania bado kina Kalamu watawatoa kasoro na kuwatupia lawama nyingi.

Samia anaimalizia SGR muda huu wakati sisi tunajibishana, muda huu kuna watu wanaingia kwenye kilimo cha mbogamboga ili wafaidike na treni kwa kuuza mazao yao Ulaya na kwingineko duniani.

Elimu ni tatizo, haina ubunifu wa aina yoyote kila mtu anataka akishapata shahada akafanye kazi ya kuajiriwa maofisini awe anazungusha kiti chake kwa mbwembwe akiwa kafunga tai nzuri.

Wapo watanzania wenzetu na wageni kutoka mataifa mengine wanaoutumia muda huu kufaidika na rasilimali zetu wakati huo sisi tunaolalamika na kulaumu viongozi hatujakatazwa na mtu yoyote kubadilisha fikra zetu.
 
Magufuli alikuwa na sifa zote za kuitwa mzalendo lakini ni sisi humu jukwaani tuliomletea dharau za kila aina. Hata Malaika wakiletwa na Mungu waje kuongoza Tanzania bado kina Kalamu watawatoa kasoro na kuwatupia lawama nyingi.
Huku ndiko kujichanganya kwako, ambako sasa naelewa unafanya kwa maksudi maalum (kinafiki). Ni "mzalendo" gani anayefanya baadhi ya mambo kama kichaa!

Kwa hiyo huyu wako naye unataka aige ya Magufuli ili na yeye aonekane mzalendo?

Magufuli alionyesha mambo mazuri kwa Tanzania, lakini hapo hapo alifanya mambo maovu ambayo kamwe hata angefanya mazuri vipi asingeweza kufuta huo uovu mkubwa aliokuwa akionyesha.
Huyu Samia wako kadhani akilaghai watu kwa lugha tamu kukataa hayo maovu ya Maghufuli, ataonekana yeye ni kiongozi mzuri na kusifiwa. Alipoona ulaghai ule watu wameutambua, haraka kakimbilia kwenye maovu yale yale ya Magufuli, ambayo ndiyo haya sasa yanayoliliza taifa.
Mbaya zaidi, licha ya kuiga maovu ya Magufuli, yeye Samia anafanya kinyume kabisa na yale mazuri ya Magufuli. Sasa waTanzania na raslimali zao wamekuwa ni bidhaa tu za kupelekwa sokoni.

Mnao faidika na uovu huu, ndio nyinyi mliolazimika kujiunga humu JF nyakati hizo hizo hizo kutetea uongozi usio kuwa na dira yoyote juu ya nchi hii.
 
Wapo watanzania wenzetu na wageni kutoka mataifa mengine wanaoutumia muda huu kufaidika na rasilimali zetu wakati huo sisi tunaolalamika na kulaumu viongozi hatujakatazwa na mtu yoyote kubadilisha fikra zetu
Ni mistari hii miwili ndiyo yenye maana kwako (watanzania wenzenu); na "wageni" mnaowanadisha masi asili zetu na kutufanya wengine wote tuwe watwana zenu/zao, ndiyo hasa inayo waelezea wewe na huyo Samia.

Na ungekuwa kweli umemwona Magufuli kuwa "mzalendo" kama ulivyo andika hapo juu; haya maneno usinge yaandika kabisa hapa.
Tabia zile zile za Ki-Samia (ni tamaduni hizi) ndizo zinazo waunganisha nyinyi, genge linalo mwendesha Samia wakati huu.
 
Unahisi kwamba nchi imeuzwa kwa sababu huna uelewa mpana wa kinachofanyika na una haki kabisa ya kuwa na mtazamo huu kwa sababu ni udhaifu wa serikali kushindwa kuwa na wataalam wenye uwezo wa kutoa ufafanuzi juu ya maamuzi yenye kuhusu miradi mikubwa inayofanyika.

BIashara ya bandari ni matunda ya biashara ambayo mwaka 2017 kulisainiwa mkataba wa kibiashara kati ya DRC na DP World lengo haswa ni kununua madini ya nchi ile.

Mwaka 2019 ukasainiwa mkataba mwingine kati ya serikali ya Rwanda na DPW lengo ni lile lile la kununua mali kwa maana ya madini na kujenga sehemu kubwa ya kutunzia mzigo ukiwa unasubiri kusafirishwa na treni kuja huku Dar bandarini.

Mwaka jana umesainiwa mkataba kati ya DPW na serikali ya Tanzania lengo ni uendelezaji wa bandari ya Dar na usafirishaji wa madini kutoka Rwanda na DRC kuja bandarini kupandishwa melini na kwenda huko nje.

Mkataba uliosainiwa Dar mbele ya Rais SSH ni muendelezo wa kile kilichosainiwa kule DRC na Rwanda mbele ya marais wawili wa mataifa hayo mawili, ukisema Samia anauza nchi pia uwe na vigezo vya kusema Tshisekedi na Kagame pia wameuza nchi zao kwa waarabu.

Haya ni masuala ambayo serikali yetu inakosa wataalam sahihi wa kuyatolea maelezo ya kina matokeo yake wanaacha maswali mengi na kina Kalamu wanakuja na habari za kizushi humu JF.
 
Huku ndiko kujichanganya kwako, ambako sasa naelewa unafanya kwa maksudi maalum (kinafiki). Ni "mzalendo" gani anayefanya baadhi ya mambo kama kichaa!

Kwa hiyo huyu wako naye unataka aige ya Magufuli ili na yeye aonekane mzalendo?

Magufuli alionyesha mambo mazuri kwa Tanzania, lakini hapo hapo alifanya mambo maovu ambayo kamwe hata angefanya mazuri vipi asingeweza kufuta huo uovu mkubwa aliokuwa akionyesha.
Huyu Samia wako kadhani akilaghai watu kwa lugha tamu kukataa hayo maovu ya Maghufuli, ataonekana yeye ni kiongozi mzuri na kusifiwa. Alipoona ulaghai ule watu wameutambua, haraka kakimbilia kwenye maovu yale yale ya Magufuli, ambayo ndiyo haya sasa yanayoliliza taifa.
Mbaya zaidi, licha ya kuiga maovu ya Magufuli, yeye Samia anafanya kinyume kabisa na yale mazuri ya Magufuli. Sasa waTanzania na raslimali zao wamekuwa ni bidhaa tu za kupelekwa sokoni.

Mnao faidika na uovu huu, ndio nyinyi mliolazimika kujiunga humu JF nyakati hizo hizo hizo kutetea uongozi usio kuwa na dira yoyote juu ya nchi hii.
Hakuna maendeleo bila ya kujitoa mhanga, ni sawa na mtoto mdogo anapopigwa sindano hulia na huleta fujo kwa daktari lakini baada ya saa kadhaa atakapokuwa kapona ataanza kucheza na kurukaruka kwa furaha akisahau uchungu wa sindano inapoingia takoni.
 
Mfano unao onyesha ufinyu wa ufahamu wa maeneo yote mawili, upande wa utabibu na hata huko kwenys manufaa ya nchi.
Wewe utakuwa ni tibabu wa hovyo sana kudhani kila sindano inafaa kwa huyo mtoto, bila ya kujali hayo maumivu ni ya kuleta ahueni au maumivu ya kuumiza huyo mtoto. Katika eneo hili ninakuhakikishia utakuwa ni mwanafunzi tu, kwa sababu hujui kitu huku.

Hata huelewi kwamba kuna njia mbali mbali mbadala za kumpa huyo mtoto dawa stahiki bila ya hayo maumivu! Unachojuwa wewe ni kuimba tu hayo "maumivu".

Samia kama huyo daktari wako mwovu, au asiyejua kazi yake, anaishia kuumiza taifa hili; huku nyinyi manesi wake mkishangilia kwa kutojuwa anacho fanya.
Huwezi kuwaburuza wenye nchi katika maswala ya maendeleo yao eti kuna daktari feki atakaye wapa maumivu kabla ya kuwaponyesha maradhi. Samia anaua kabisa moyo wa waTanzania. Hili ni kosa linalostahiri huyu mama kuwekwa hatiani hata akisha ondoka madarakani.. Hakuna kiongozi wa aina hii anaye weza kuvumiliwa.
 
Unahisi kwamba nchi imeuzwa kwa sababu huna uelewa mpana wa kinachofanyika na una haki kabisa ya kuwa na mtazamo huu kwa sababu ni udhaifu wa serikali kushindwa kuwa na wataalam wenye uwezo wa kutoa ufafanuzi juu ya maamuzi yenye kuhusu miradi mikubwa inayofanyika.

BIashara ya bandari ni matunda ya biashara ambayo mwaka 2017 kulisainiwa mkataba wa kibiashara kati ya DRC na DP World lengo haswa ni kununua madini ya nchi ile.

Mwaka 2019 ukasainiwa mkataba mwingine kati ya serikali ya Rwanda na DPW lengo ni lile lile la kununua mali kwa maana ya madini na kujenga sehemu kubwa ya kutunzia mzigo ukiwa unasubiri kusafirishwa na treni kuja huku Dar bandarini.

Mwaka jana umesainiwa mkataba kati ya DPW na serikali ya Tanzania lengo ni uendelezaji wa bandari ya Dar na usafirishaji wa madini kutoka Rwanda na DRC kuja bandarini kupandishwa melini na kwenda huko nje.

Mkataba uliosainiwa Dar mbele ya Rais SSH ni muendelezo wa kile kilichosainiwa kule DRC na Rwanda mbele ya marais wawili wa mataifa hayo mawili, ukisema Samia anauza nchi pia uwe na vigezo vya kusema Tshisekedi na Kagame pia wameuza nchi zao kwa waarabu.

Haya ni masuala ambayo serikali yetu inakosa wataalam sahihi wa kuyatolea maelezo ya kina matokeo yake wanaacha maswali mengi na kina Kalamu wanakuja na habari za kizushi humu JF.
"Wataalam" wenyewe si ndio akina nyinyi, akina Johari Hamza, au siyo! Genge la wapigaji; wezi, akina Kafulila ndio mnao tamba siku hizi!

Usifikiri akina Kalamu wanao upungufu wa uelewa wa mambo haya ya kawaida sana, hata kama siyo maeneo wanayo jishughulisha nayo maishani mwao. Maswala ya maendeleo ya watu hayana ugumu wa kuyaelewa kama fikra pana zipo.
Ndiyo maana, baada ya kujuwa kwamba watu wanafuatilia maswala haya kwa karibu zaidi, mukaamua sasa kuyafanyia gizani, yasionekane. Huku ni kuficha maovu yaliyomo katika mipango yenu ya kulihujumu taifa hili.

haya ndiyo mtatakiwa kuwaeleza waTanzania kwa nini mlikuwa mnafanya siri kubwa wasiyafahamu mlipo kuwa mnaingia kwenye hujuma hizi dhidi yao.
 
Tatizo lako unadhani unajua unachokijadili kumbe ni mbumbumbu mzungu wa reli, zero kabisa.

Masuala ya mikataba ya kimataifa sio wengi wanaoyafahamu, tatizo la watanzania ni kuamini mijadala ya vijiweni mkidhani ndio uelewa sahihi kumbe ni kuzidi kupotezana tu.

Hamza Johari ni mwanasheria wa kimataifa kasomea sheria za kimataifa pale Kiev Ukraine huwezi kumlinganisha na hizi takataka kina Mwabukusi na Madeleka.

Kuna mkataba mwingine wa Adani umempa nafasi ya kufanya kazi pale pale bandarini, umeshawahi kuuona?.

Unachekesha sana Kalamu, ukamtafuta mwanasheria wako Mkenya mkaanza kuwapotosha watu kwenye media za kibongo mkidhani kuwa serikali imepotoka kumbe hamjui chochote mnachokiongea maskini ya Mungu.
 
Mfano unao onyesha ufinyu wa ufahamu wa maeneo yote mawili, upande wa utabibu na hata huko kwenys manufaa ya nchi.
Wewe utakuwa ni tibabu wa hovyo sana kudhani kila sindano inafaa kwa huyo mtoto, bila ya kujali hayo maumivu ni ya kuleta ahueni au maumivu ya kuumiza huyo mtoto. Katika eneo hili ninakuhakikishia utakuwa ni mwanafunzi tu, kwa sababu hujui kitu huku.

Hata huelewi kwamba kuna njia mbali mbali mbadala za kumpa huyo mtoto dawa stahiki bila ya hayo maumivu! Unachojuwa wewe ni kuimba tu hayo "maumivu".

Samia kama huyo daktari wako mwovu, au asiyejua kazi yake, anaishia kuumiza taifa hili; huku nyinyi manesi wake mkishangilia kwa kutojuwa anacho fanya.
Huwezi kuwaburuza wenye nchi katika maswala ya maendeleo yao eti kuna daktari feki atakaye wapa maumivu kabla ya kuwaponyesha maradhi. Samia anaua kabisa moyo wa waTanzania. Hili ni kosa linalostahiri huyu mama kuwekwa hatiani hata akisha ondoka madarakani.. Hakuna kiongozi wa aina hii anaye weza kuvumiliwa.
Tunarudi kule kule kwenye elimu zetu na maamuzi ya makusudi ya kuwapotosha watanzania.

Alicholalamikiwa kufanya JPM ni kubana uchumi wa ndani, Samia kaamua kwenda na njia tofauti na zile za hayati, bado watanzania mnalalamika mkidhani maisha yana njia za mkato!.

Nchi imefunguliwa na fursa ni za kumwaga muda huu, wewe na wa aina yako endeleeni kulialia na kuandika vibonzo vya kuikejeli mamlaka kwenye media mkidhani ni dawa itakayowaondoleeni umaskini.
 
Hata hueleweki unazungumzia kitu gani, bila shaka hujui unacho jaribu kueleza.

Huo mstari wa kwanza, "elimu zenu" na "maamuzi ya maksudi..." yana husiana vipi? Kwamba ufinyu wa elimu zenu, hasa hiyo ya Samia imekuwa tatizo la "kuwapotosha waTanzania"?

Samia hana njia tofauti ya uchumi inayo eleweka. Anacho fanya ni kuruhusu tu bila mpangilio wowote uvurugaji wa mali za waTanzania, kwa kuzitapanya hovyo hovyo, huku akiwafubaza akili waTanzania na kuondoa uthubutu wao kujifanyia maendeleo yao. Juhudi kubwa anayo fanya Samia ni kuwapeleka waTanzania katika utwana. Hili halikubaliki.

Fursa zingekuwa ni za kumwaga, mtuu kama wewe usingkuwa kutwa unashinda hapa kama kupe aliye ng'ang'ania kwenye ngozi ya Samia akinyonya damu. Hayo ndiyo maisha mnayo watengenezea waTanzania; maisha ya utegemezi kwa hao mnao wagawia mali asili na utajiri wa nchi hii.
 
Tatizo lako unadhani unajua unachokijadili kumbe ni mbumbumbu mzungu wa reli, zero kabisa.

Masuala ya mikataba ya kimataifa sio wengi wanaoyafahamu, tatizo la watanzania ni kuamini mijadala ya vijiweni mkidhani ndio uelewa sahihi kumbe ni kuzidi kupotezana tu.

Hamza Johari ni mwanasheria wa kimataifa kasomea sheria za kimataifa pale Kiev Ukraine huwezi kumlinganisha na hizi takataka kina Mwabukusi na Madeleka.

Kuna mkataba mwingine wa Adani umempa nafasi ya kufanya kazi pale pale bandarini, umeshawahi kuuona?.

Unachekesha sana Kalamu, ukamtafuta mwanasheria wako Mkenya mkaanza kuwapotosha watu kwenye media za kibongo mkidhani kuwa serikali imepotoka kumbe hamjui chochote mnachokiongea maskini ya Mungu.
Sijui ni mara ngapi ulisha mtaja Hamza Johari humu kuwa wa kimataifa. Bila shaka ndiye hasa anayekulisha kama siye yeye mwenyewe. Wewe unapo mwona Hamza kuwa wa thamani kubwa sana hiyo ni wazi kwamba wewe mwenyewe umepungukiwa sana kielimu.

Kusoma Kiev nayo imekuwa sifa ya kujivunia?

Kwanza mwandiko wako tu unaonyesha upungufu mkubwa kielimu.
 
Back
Top Bottom