Code zinaanza kufunguka

Code zinaanza kufunguka

China ardhi yao kubwa wameweka viwanda vingi sana na kuna sehemu serikali ililazimika iwauwe wananchi na kuwavunjia nyumba zao ili wasonge mbele kwa kujitanua kiuchumi
Hakufika hapo kwa kucheka
Sasa mashamba hakuna ya kutosha kwa kukidhi mahijaji yao na hata chakula cha mifugo yao
Unajua wanalenga wapi ili wazalishe chakula chao?
Wameanza kuotesha mimea jangwani
 
Samia mweupe sana kwenye masuala ya geopolitics, aendelee kutembelea shows za taarab huko Z'bar... Na kuwapiga mipasho wapinzani...
JPM aliyeamua kubakia humu ndani akishindwa kuvuka hapo mediterannean ndio aliyezijua geopolitics!.

Anafanya mengi sana huko mikoani sisi wa mijini tunachojua ni kukosoa tu.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina

Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
Kumuua Membe lilikuwa kosa kubwa mno sasahivi hawaoni future ya maslahi yao!!

Ameshazengua kitambo Sana kitendo Cha kumu attack Mage kimambi , kumfukuza makamba maagent wa CIA .

Hatokaa atoboe

Marekani imemuandaa January muda mrefu Sana kuja kuwa Rais sasa baada ya kuondolewa wizara ya mambo ya nje

Tegemeeni kuona Kila aina ya rangi ya beberu!!!
 
DPW wapo bandarini mpaka mkataba wao utakapomalizika.

Viwanda vingi vinaanzishwa muda huu wewe huwezi kuvijua kwa sababu unabii wa majanga ni tatizo lako kuu kuliko mengine yote.

Akili finyu unayo wewe mwenye mawazo yale yale ya kuona kazi inafanywa na watu wengi, kuna teknolojia za kisasa zinaondoa nguvu kazi nyingi kwenye ajira muda huu, mitambo ya kisasa inafukuza watu makazini.

Ujerumani wamegundua teknolojia za kujenga nyumba bila ya uwepo wa mafundi kwenye site, ni mitambo tu ipo kazini, maana yake wote wanaosomea vyuoni masuala ya uhandisi wa majengo wanakwenda kukosa kazi siku teknolojia hizo zikifika hapa Tanzania.

Akija mwekezaji kwenye sekta ya uhandisi na mitambo yake ya kujenga, kina Kalamu wenye akili za kizamani watampinga kwa nguvu zote.

Dunia inakwenda kasi sana jitahidi uende nayo kwa kasi hiyo hiyo ili usibakie kuchekesha watu humu kwenye jamvi.
Kwa hiyo hapa unajisikia ume andika jambo la maana sana litakalo wasaidia waTanzania kutoingizwa kwenye utwana? DPW waombe sana na watoe hela nyingi sana za kununua serikali ya genge lenu ili iendelee kuwepo na kuhujumu. Viginevyo uamzi wa wao kuendelea hapo utategemea maslahi ya nchi na siyo ya genge lenu. Si ulizungumzia TICTS mlivyo wanyang'anya mfupa mdomoni; halafu wakati huo huo unashindwa kuona hayo yakiwatokea DPW?

Sasa nikuulize wewe kwa akili hiyo ndogo ya kudhani teknolojia inakuwepo kuwaondoa watu kazini bila ya uwepo wa mbadala watu hao watafanya na kufaidika na nini kutokana na hiyo teknolojia.
Hivi wewe unadhani haya mambo unayo okoteza huko kuwa ni mageni kwangu, au siyo? Umesoma kijarida gani ukaiona habari hiyo leo. Unapo sikia' Artificial Intelligence' (AI), unaelewa maana yake ni nini hasa?

Kwa hiyo achana na kujaribu kunifanya kama mtu asiye na uelewa mpana kuhusu haya mambo. Nipo mbele yako sana kuhusu haya.
Hapa tujadili tu hali ya waTanzania wetu hawa maskini, mnaofanya kila juhudi kuwatumbukiza tena katika enzi za utwana na utumwa. Fahamu kuwa hilo halitawezekana tena.
 
Nenda hazina kaulize mchango wa Bandari kwenye magawio ya serikali mwaka huu ni kiasi gani kimeongezeka.

Hakuna haja ya kuandikia mate, wino upo.
Ninacho kueleza ni kuwa hayo magawiwo unayo yazungumzia hapa ni kabla ya DPW kufanya kazi hapo. Bandari tayari ilikuwa imeanza kufanya kazi vizuri baada ya ukarabati mkubwa ulio fanyika hapo.
Hata hivyo, bado upo nje ya maswala tunayo jadili kama ilivyo kawaida yako. Wewe jambo pekee unalojuwa ni DPW, basi, nje ya hapo huna lingine.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina

Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
Tanzania haijawahi kuwa mbali na wachina tangu tupate uhuru

And that will never change
 
Kusaidia kupunguza joto ma eneo mengi yamekaliwa na watu... Pamoja na kuweka shughuli za kilimo
Safi sana
Ila na sisi sio wabunifu mkuu yaani Halmashauri wanajua kutoza kodi tu na kuzila ila kufanya jema hakuna
Yaani mpaka mchina daa
 
Ninacho kueleza ni kuwa hayo magawiwo unayo yazungumzia hapa ni kabla ya DPW kufanya kazi hapo. Bandari tayari ilikuwa imeanza kufanya kazi vizuri baada ya ukarabati mkubwa ulio fanyika hapo.
Hata hivyo, bado upo nje ya maswala tunayo jadili kama ilivyo kawaida yako. Wewe jambo pekee unalojuwa ni DPW, basi, nje ya hapo huna lingine.
Hujui unaloliongea, bandari licha ya ukarabati mkubwa kuna vitu ambavyo vilikuwa vikiikoseshea ufanisi wake.

DPW wamekuja na ufanisi wenye haraka zaidi, meli moja inahudumiwa haraka zaidi kwa sasa kulinganisha na kipindi kile tulipokuwepo sisi wenyewe.

Pia DPW katika mkataba wake kuna kipengele kinachomtaka awape ujuzi wafanyakazi wa bandari wazalendo. ukizisikiliza nadharia zetu wazalendo ni kwamba tunao uwezo wa kujiendeshea bandari yetu sisi wenyewe ukweli na uhalisia haupo hivyo, bado kiwango chetu cha kupata wataalam wapya ni kidogo sana na hata uwezo wa kukuza maarifa ya wafanyakazi waliokwisha kuajiliwa tayari ni mdogo pia..

Kuboresha bandari kwa mabilioni ya pesa sio hakikisho la kukua kwa uwezo wa ufanisi wa utendaji kazi wetu,. Mimi nipo karibu na sekta ya bandari naelewa zaidi kinachofanyika kule kuliko wewe Kalamu.

Chuki yako wewe ipo kwa Rais Samia na asili yake ya uarabu alionao kwa mbali, tunahisi kwamba DPW wapo pale wakiwa wamebebwa na 'undugu' walionao na SSH, hizi ni habari za kipuuzi kama zile za udaku tunazozisoma kwenye magazeti na mitandaoni.

Hawa DPW wangekuwa wameletwa na Rais Mkristo wala tusingepoteza muda kuwapinga. Wangekuwa ni waingereza au watu wa mataifa ya kizungu tusingepoteza muda na nguvu katika kuupinga uwekezaji wao.
 
Kwa hiyo hapa unajisikia ume andika jambo la maana sana litakalo wasaidia waTanzania kutoingizwa kwenye utwana? DPW waombe sana na watoe hela nyingi sana za kununua serikali ya genge lenu ili iendelee kuwepo na kuhujumu. Viginevyo uamzi wa wao kuendelea hapo utategemea maslahi ya nchi na siyo ya genge lenu. Si ulizungumzia TICTS mlivyo wanyang'anya mfupa mdomoni; halafu wakati huo huo unashindwa kuona hayo yakiwatokea DPW?

Sasa nikuulize wewe kwa akili hiyo ndogo ya kudhani teknolojia inakuwepo kuwaondoa watu kazini bila ya uwepo wa mbadala watu hao watafanya na kufaidika na nini kutokana na hiyo teknolojia.
Hivi wewe unadhani haya mambo unayo okoteza huko kuwa ni mageni kwangu, au siyo? Umesoma kijarida gani ukaiona habari hiyo leo. Unapo sikia' Artificial Intelligence' (AI), unaelewa maana yake ni nini hasa?

Kwa hiyo achana na kujaribu kunifanya kama mtu asiye na uelewa mpana kuhusu haya mambo. Nipo mbele yako sana kuhusu haya.
Hapa tujadili tu hali ya waTanzania wetu hawa maskini, mnaofanya kila juhudi kuwatumbukiza tena katika enzi za utwana na utumwa. Fahamu kuwa hilo halitawezekana tena.
Na DPW sio mwekezaji wa mwisho ndani ya Tanzania, wanakuja wengi tu na teknolojia zao, sisi wazalendo tukiendekeza maneno mengi na ujuaji mwingi bila ya kukuza elimu zetu kwa masuala mbalimbali, tutaishia kuwa na akili sawa na za Kalamu, zenye kupenda kulialia na kulalamika.

Mfumo wa maisha wa sasa ni hauna lelemama hata kidogo. Ukizubaa umeachwa na wenzako wanakimbilia fursa mbalimbali za uwekezaji.

Kuna suala la bandari yetu kuwa ni ya kisasa yenye kuweza kushindana na bandari nyinginezo za ukanda huu. Huko Msumbiji na Afrika ya Kusini wanazidi kuwekeza vilivyo kwenye bandari zao.

Kuna soko la Malawi, Zambia na Zimbabwe, haya ni makubwa sana yenye bidhaa nyingi na hatuwezi kusikiliza kelele za wanaojiita wanaharakati ambao hawajali nchi inapokosa masoko haya ya wateja wa bandari kwa upuuzi tu wa mitandaoni, hakuna mwenye utayari wa kuwasikiliza mawakala hawa wa washindani wetu kibiashara (stooges).

DPW anakwenda kutusaidia sana katika kuifanya bandari yetu iwe na ushindani mkubwa, kusema tutegemee wafanyakazi hawa hawa wazawa wenye ugumu wa kuongeza maarifa na sifa mbaya ya ufisadi wa kila aina, ni kupoteza muda.

Kwa bahati mbaya masoko ya ushoroba wetu hayatusubiri hata kidogo nimemuelewa SSH alipokwenda China na kufufua mazungumzo ya biashara ya TAZARA , ni katika kukuza soko la bandari yetu kwa maana ya kuongeza wingi wa mzigo unaoshughulikiwa mahali pale.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina

Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
Intelegensia ya Tanzania ni kubwa sana, inatumalizia fedha zetu kuihudumia lakini inatudaidia sana kutubakisha salama. Wakati wa ukombozi wa bara la Afrika, azimio la Arusha, na sera ya ujamaa na kujitegemea Tanzania ilikuwa imejioatia maadui wengi sana kutoka nchi za mabeberu na makaburu lakini intelegensia yetu ilitusaidia na kumsaidia mwl Nyerere awe hai.

Intelegensia yetu inajua Magharibi wanashirikiana na chadema kuleta vurugu nchini. China hawana mashariti ya kipuuzi ya kuwekeana vikwazo na kulazimishana ushoga kwa kisingizio cha demokrasia ya kipuuzi. Dominance ya nchi za magharibi duniani inazidi kuporomoka maana hata wao hawana cha kugawa siku hizi, wanapoga miayo pia na kuitegemea china pia. Hata mauzo ya silaha zao yameshuka sana maana hazifui dafu kwa zile za Urusi na Iran.
 
Pia DPW katika mkataba wake kuna kipengele kinachomtaka awape ujuzi wafanyakazi wa bandari wazalendo. ukizisikiliza nadharia zetu wazalendo ni kwamba tunao uwezo wa kujiendeshea bandari yetu sisi wenyewe ukweli na uhalisia haupo hivyo, bado kiwango chetu cha kupata wataalam wapya ni kidogo sana na hata uwezo wa kukuza maarifa ya wafanyakazi waliokwisha kuajiliwa tayari ni mdogo pia..
Miaka 30 ndio kipimo mlicho wawekea waTanzania kuwa watakuwa wamepata ujuzi?
Hizi ni sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Ile bandari pakiwepo na uongozi unaotambua maslahi ya nchi, waTanzania wenyewe wapo hata leo kuiendesha hiyo bandari kwa ufanisi mkubwa.
Tatizo lako na mama yenu ni lile lile,kudharau uwezo wa waTanzania, na kujiona nyinyi na wajomba zenu ndio bora kuliko waTanzania. Sasa sijui nilieleze hili nilieleze vipi ili liweze kuingia akilini mwako.

Lakini najua, hata kama unaelewa huwezi kukubali ukweli huo kwa sababu ya manufaa yenu mnayo yalinda kwa kila njia.
 
Na DPW sio mwekezaji wa mwisho ndani ya Tanzania, wanakuja wengi tu na teknolojia zao, sisi wazalendo tukiendekeza maneno mengi na ujuaji mwingi bila ya kukuza elimu zetu kwa masuala mbalimbali, tutaishia kuwa na akili sawa na za Kalamu, zenye kupenda kulialia na kulalamika.
Sasa angalia upumbavu huu hapa unao uandika bila ya kuutilia maanani. Unataka nani "akuze elimu zetu kwa maswala mbalimbali" wakati ni Samia na genge lenu mnao fanya kila jitihada kudhoofisha kila kitu ili waTanzania wabaki kuwa watwana wenu?
 
Mfumo wa maisha wa sasa ni hauna lelemama hata kidogo. Ukizubaa umeachwa na wenzako wanakimbilia fursa mbalimbali za uwekezaji.
Sasa unamwambia nani haya, badala ya kwenda kwa Samia na kumweleza kuwa anawahujumu waTanzania kwa kudhani kuwa watu wanao weza ni kutoka huko nje na siyo waTanzania walio andaliwa kuchukua jukumu la kuiendeleza nchi yao?

Wajibu wa Samia na serikali yake kwa waTanzania ni upi, kunadi mali asili za nchi yao, au kuhakikisha kwamba wananchi wamewezeshwa kuchukua jukumu la maendeleo ya nchi yao?
Ulisikia mChina akienda kutafuta wawekezaji toka nje na kusahau kuwaandaa wananchi wake. Korea Kusini, walisubiri wawekezaji waingie ndipo makampuni yao makubwa yaanzishwe? Nitajie hata nchi moja ambayo imebweteka tu ikisubiri viongozi wake wakatafute akina DPW wa dunia wakawaletee maendeleo!
 
Samia anajenga mashule na zahanati nchi nzima, anajenga viwanda nchi nzima, miaka michache ijayo ataanza kuifufua reli ya TAZARA, tutakuwa na reli mbili ya SGR inayokwenda huko kanda ya ziwa na huyo reli kongwe.

Hivyo vyote vinaajiri mamilioni ya watanzania, ni juu ya vijana wetu kuchangamka madarqsani ili waweze kuajiriwa, kuna mamia kwa mamia ya fursa za kiuchumi zinaendelea kufanyiwa kazi kwa ajili yetu watanzania ili tusiwe vibarua katika nchi yetu wenyewe.

Huwezi kukwepa uwekezaji, narudia tena kukielimisha kichwa chako kigumu na sitachoka kufanya hivyo.

Hao Wachina na Wakorea walijengewa na wanaendelea kujengewa misingi ya kuwa wamiliki wa rasilimali zao kupitia mashuleni, tusifanye mchezo na elimu.

Huku duniani ni vita inaendelea huko katika misingi ya kielimu ndio maandalizi ya uhakika yanapofanyika.

DPW na Adani wamekuja kuongeza tija hapo bandarini, kumbuka miaka michache ijayo tutakuwa na reli mbili zinazopeleka mzigo hapo bandarini, itakuwa ni sehemu yenye kutegemewa kuzalisha ziada muda wote.

Hatuwezi kulea uzembe kwa kisingizio cha kutowageuza vibarua na watwana vijana wetu. Watu wapige pesa za wizi hapo TPA na serikali ikija na mbinu za kuongeza mzunguko wa faida waibuke wanaharakati kama Kalamu na kuanza kutetea uchafu wa miaka yote.

Wakafie mbele hao wanaharakati.
 
Sasa angalia upumbavu huu hapa unao uandika bila ya kuutilia maanani. Unataka nani "akuze elimu zetu kwa maswala mbalimbali" wakati ni Samia na genge lenu mnao fanya kila jitihada kudhoofisha kila kitu ili waTanzania wabaki kuwa watwana wenu?
Samia anagusa kila sekta muhimu, hata hiyo elimu pia inaguswa kwa kuongeza malipo ya wanavyuo vyetu kwa njia ya mikopo.

Dunia hii haina huruma hata kidogo, hao Korea na China ni superpowers wenye kutambulika na kuheshimika, wana misingi mizuri ya kielimu.

Sisi ujanja wetu ni soga zinazoishia humu JF, huko bandarini bado tupo nyuma kwenye kusomesha wataalam wenye uelewa wa kisasa wa masuala mengi ya shipping, tuwe wakweli tupunguze kupiga siasa.
 
Miaka 30 ndio kipimo mlicho wawekea waTanzania kuwa watakuwa wamepata ujuzi?
Hizi ni sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Ile bandari pakiwepo na uongozi unaotambua maslahi ya nchi, waTanzania wenyewe wapo hata leo kuiendesha hiyo bandari kwa ufanisi mkubwa.
Tatizo lako na mama yenu ni lile lile,kudharau uwezo wa waTanzania, na kujiona nyinyi na wajomba zenu ndio bora kuliko waTanzania. Sasa sijui nilieleze hili nilieleze vipi ili liweze kuingia akilini mwako.

Lakini najua, hata kama unaelewa huwezi kukubali ukweli huo kwa sababu ya manufaa yenu mnayo yalinda kwa kila njia.
Hakuna mtu anayeudharau uwezo wa watanzania, ni sisi wenyewe tunajidharau kwa kuendekeza tabia za ufisadi na wizi wa kila aina.

Tangu awamu ya tatu ya Kikwete kumekuwa na wakaguzi wakuu wa mahasebu ya serikali watatu, Utouh, Assad na Kichere, hakuna mwaka hata mmoja ambapo nchi kwa ujumla imekuwa na mahesabu safi baada ya ukaguzi. kwa awamu tatu za marais kila mwaka ni uchafu mtupu unaorekodiwa na kuwekwa kwenye vitabu vinavyomfikia Mheshimiwa Rais pale ikulu.

Madudu hayo yapo kila mahali hata TPA ulikuwa ni uchafu mtupu, hao ndio watanzania wa kushika bandari inayotarajiwa kupokea mizigo inayoshushwa pale na reli mbili zilizo kazini muda wote!.

SGR na TAZARA zinakwenda kuipandisha sana thamani hiyo bandari, hakuna muda tena wa kuwaendekeza wafanyakazi wazembe, wavivu na wenye kuwazia wizi.

Aina ya watendaji tulionao, bado sana.
 
Hao Wachina na Wakorea walijengewa na wanaendelea kujengewa misingi ya kuwa wamiliki wa rasilimali zao kupitia mashuleni, tusifanye mchezo na elimu.
Ngoja niseme hivi kama kumalizana na wewe: Wewe siyo hawa mapunguani wengi tunao waona humu JF; ila wewe ni fisadi anaye endeshwa tu na maslahi.
Siyo kwamba hujui unacho elezwa, unajuwa na pengine kujutia huko moyoni mwako kwamba laiti isinge kuwa maslahi ya genge, ungekuwa ni tofauti. Ungepigania maslahi ya waTanzania.
Kuna baadhi ya mabandiko yako humu ambayo yalionyesha haya ninayo elezea hapa

Hayo ya ujenzi wa shule na mengineyo yana tofauti gani na ninayo kueleza na kukumbusha hapa kila mara. Ujenge shule huku elimu inayo tolewa humo ni ya kuwawezesha waTanzania kuwa watawana..., elimu hiyo inayo manufaa gani?
Wachina hawatoi elimu ya kuwaandaa watu wao kuwa watumishi/watwana; elimu yao inawaandaa kuwa wamiliki na waendeshaji wa shughuli zao za maendeleo ya nchi yao. Hivyo hivyo na Korea Kusini, Vietnam, na kwingine kote wanakojua ni nini maana ya nchi kuwa na wajibu wa maendeleo yake.
Samia na hili genge lenu, fikra hizi hazimo kabisa akilini mwenu.

Ni hivi: tusizungushane bure. Wewe unajua ninacho zungumzia humu; na mimi kwa hakika kabisa najua unaelewa vyema ninayo andika na hata bila shaka unajutia kuwa huko kwenye upande unakolazimika kuwepo, kwa sababu tu ya maslahi, na ushikamano yenu na Samia kwa mambo mengineyo binafsi; kitamaduni na kiimani.

Sina sababu tena ya kuzungushana na wewe humu.
 
Back
Top Bottom