COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Kwa hiyo kama binadamu ana mwisho wa uwezo wake hilo linathibitisha kuwepo kwa mungu?

Kati ya anayesema kuna mungu ambaye hawezi kumthibitisha na anayekataa uwepo wa mungu huyo mpaka uthibitisho uwepo nani anajifanya mjuaji?

Kujifanya mjuaji kwangu mimi ni kudai unajua kitu usichojua.

Mimi sikubali kuwepo kwa mungu kwa sababu silijui hilo.

Wanaosema mungu yupo bila ya kuwa na uwezo wa kuthibitisha hilo ndio wanaojifanya wajuaji.
 
MwenyezMungu ametuumba na ametupa utashi wa kutambua jambo jema na baya. Na pia ameziacha huru nafsi zetu kutenda tutakacho ili iwe km mtihani siku ya mwisho,waonekane watakaofeli na kufaulu.
 
Toa sababu za kukufanya usikubali kuwa Mungu yupo....
 
MwenyezMungu ametuumba na ametupa utashi wa kutambua jambo jema na baya. Na pia ameziacha huru nafsi zetu kutenda tutakacho ili iwe km mtihani siku ya mwisho,waonekane watakaofeli na kufaulu.

Hajaziachia nafsi zetu kutenda tutakacho.

Angeweza kuruhusu turudi nyuma katika muda, lskini hakutupa uhuru huo.

Pia, angeweza kuturuhusu kuamua kama tunataks kuzaliwa au hatutaki.

Hskutupa uamuzi huu mkubwa sana.

Kwa hiyo hii habari ya kwamba mungu anapenda kitupa uhuru tuamue tutakacho ni uongo.

Halafu mungu mjuxi wa yote na meenye uwezo wote kea nini ahitaji kutupa sisi binadamu mtihani wskati anajua kila kitu?

Mwalimu asiyejua yote anaweza kumpa mwanafunzi mtihani ili ajue mwanafunzi anajua nini.

Mungu anampa mwanadamu mtihani ili iweje?
 
Blah blah miiingi
Huyo Mungu mbona najificha ficha hivi na haelewiki?

Tatizo la mungu kutojidhihirisha kwa njia ya wazi isiyopingika kwa wote nikishaliulizis swali hapa, na mpaka leo sijapewa jibu.
 
MwenyezMungu ametuumba na ametupa utashi wa kutambua jambo jema na baya. Na pia ameziacha huru nafsi zetu kutenda tutakacho ili iwe km mtihani siku ya mwisho,waonekane watakaofeli na kufaulu.
Hawa watu wana ajenda ya siri ya kuchanganya akili za watu, ilihali wao wanapata nafasi ya kufanya mambo yao. Ukisha aminishwa Mungu hayupo ina maana hutakuwa na nguvu ya kukemea hata maovu yanayotendeka mfano ushoga n.k...kwahyo hawa watu wanakuja kwa kasi sana. Tujitahidi kuwaelimisha ili umma usipotoshwe ndugu, tujadili nao tutafika tu..na wataelewa kwa kudra za Mwenyezi-Mungu
 
Toa sababu za kukufanya usikubali kuwa Mungu yupo....

Sababu kubwa ya kutokubali mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo ni uwepo wa mabaya kwenye ulimwengu huu.

Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumbs ulimwengu wowote alioutaka, ukiwamo ule ambao mabaya hayawezekani.

Haiyumkiniki akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
 
Hapana.

Kuna watu wanaamini mungu mpaka wamefika kupewa dhamana za kidini na ni mashoga, wauaji (kwa jina la mungu nonetheless) etc.

Kuna wengine hawaamini mungu lakini wametoa maisha yao kuhudumia jamii kwa moyo wote.

Tatizo unalolionesha wewe katika post yaki ni lack of exposure.

Your frame of reference is probably very small by the looks of how generalized and myopic your conclusions are.
 
Unachanganya uhuru na uwezo.
 
Jaaah...kwahiyo kumbe ni hayo tu..! Mabaya wanaoleta si binadamu wenyewe, kwa mfano ww umetambua vyema kuwa kuna mabaya duniani..je hakuna mambo mema pia duniani?
 
Nimesoma mijadala ya watu pamoja na ya mleta uzi na nimegundua kwamba BINADAMU NDIO AMEMTENGENEZA / AMEMUUMBA MUNGU KUTOKANA NA KUSHINDWA KUPATA MAJAWABU YA VITU MBALIMBALI VILIVYOMZUNGUUKA.
Hayo ni mawazo yako wewe kulingana na uelewa wako ...! Kwani ww unajuaje? Kulingana na wewe je Mungu yupo au hayupo?
 
Tatizo la mungu kutojidhihirisha kwa njia ya wazi isiyopingika kwa wote nikishaliulizis swali hapa, na mpaka leo sijapewa jibu.

Kwani angeamua kufanya hivyo ndiyo ingekuaje?maana unachokiuliza hapo ni maamuzi yake.
 
Hayo ni mawazo yako wewe kulingana na uelewa wako ...! Kwani ww unajuaje? Kulingana na wewe je Mungu yupo au hayupo?
Mie nipo katikati kuna mazingira huwa naamini uwepo wake na kuna mazingira huwa naamini kutokuwepo kwake. Kwa sababu wakati mwingine huwa naona hizi dini ni kama mapokeo flani hivi
 
Naamini Mungu yupo kwa asilimia zote

Swali halikuwa kama unaamini, swali likikutaka uthibitishe kwamba yupo.

Viwili hivi ni tofauti.

Kama hujui tofauti kati ya kuamini na kuthibitisha, nitajuaje kama una basic requirements za kuweza kushiriki mjadala huu?
 
Kwani angeamua kufanya hivyo ndiyo ingekuaje?maana unachokiuliza hapo ni maamuzi yake.

Huwezi jusema maamuzi yake wakati hujaweza kuthibitisha kwamba yupo.

Kama hayupo, hawezi hata kufanya maamuzi.

Unaweza kuthibitisha kwamba yupo?

Hilo ni moja.

Pili, kusema "hayo ni maamuzi yake" bila kiweza kuelezea maamuzi hayo kayafikia kwa logic gani ni kukibali kwamba humuwlewi huyu mungu, unamkubali kwa upofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…