Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Katika suala hili, ni kwamba kuna watu hawajui chochote na ujifanya wajuaji. Hii inanikumbusha wakati nasoma ,,nilipokuwa darasa la kwanza nilijiona mi ndo msomi kuzidi wenzake, halikadhalika kila ninapokuwa level nilijiona kuwa nime elimika sana...ila ukweli sivyo. Katika suala la Mungu ni kwamba binadamu hawezi kulichunguza na kupata majibu anayotaka yeye. Kwa sababu binadamu kuna point ikiwa hawezi fanya jambo fulani....mfano kuna kiwango maalum binadamu anaweza kusikia sauti au mlio wa kitu, hiko kiasi kikizidi au kupungua hawezi sikia huo mlio ( audible range). Na pia kuna visible range ya binadamu, ikiwa kitu kitakuwa nje ya hiyo range hawezi kuona colour yoyote. Pia hata ktk uwezo wetu wa kukimbia pia upo limited, huwezi fananisha kukimbia kwa cheetah na binadamu. Nasuala la kufikiri pia, kuna range yetu ya kufikiri.....ukifika hapo huwezi kuendelea kufikiria tena, ila kifuatacho kitakuwa ni kufur au kuamua kuwaza vitu vingine. Mungu awabariki..
Kwa hiyo kama binadamu ana mwisho wa uwezo wake hilo linathibitisha kuwepo kwa mungu?
Kati ya anayesema kuna mungu ambaye hawezi kumthibitisha na anayekataa uwepo wa mungu huyo mpaka uthibitisho uwepo nani anajifanya mjuaji?
Kujifanya mjuaji kwangu mimi ni kudai unajua kitu usichojua.
Mimi sikubali kuwepo kwa mungu kwa sababu silijui hilo.
Wanaosema mungu yupo bila ya kuwa na uwezo wa kuthibitisha hilo ndio wanaojifanya wajuaji.