COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Zinafeli vibaya mno.

Tatizo watu washakunywa maji ya dini mengi sana hawawezi kukubali ukweli. Na hata wakiujua wana cognitive dissonance inayoweza kutunga sababu zozote za kipuuzi kama "mtihani" ilu kutetea uongo.

Mungu mwenye kujua yote anahitaji mtihani kwa nini?

Na kama matatizo ni mtihani kweli mbona wengine wanakufa tumboni kabla hata ya kupata nafasi ya kutahinuwa, huju wengine wakifa wachanga.

Hata hilo baraza la mitihani lingekuwa linachagua watu randomly na kusema wewe una namba ya mtihani lakini hutafanya mtihani watu wasingeelewa, sembuse mungu mwenye haki zote, uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
 

Kupinga ni jambo rahisi sana.

Nimejaribu kujibu maswali yenu hadi mmefikia na kubaki na maswali ya kwanini imekuwa hivi kwanini isingekuwa vile. Sasa tujielekeze kwn mfano niliyotoa ili wote tuweze kuelezea kile tunachnkiamini na kukielewa,na si mmoja kupinga hoja za mwenzie kwa kumuuliza maswali tu.
 
Papa Francis alishalisema hilo.

Papa Francis asema hajui

Papa Francis kama mwanatheolojia anajua hili swali si la kitoto.

Wamejaribu kujibu tangu enzi za St.Augustine na Anselm, na halijapata jibu mpaka leo.

Mtu yeyote aliyesoma the classic arguments in the nature of god atajua hilo.

Kwa hiyo Papa analojua hilinswali, kasoma theolojua, kajua hakuna jibu la kusleweka kwenye swali hili, kasema ukweli wake kwamba hajui jibu.

Sasa hapa utakutana na watu ambao hata hawamjui Andelm au St. Augustine ni nani, wafajifanya kwamba biblia ina majibu ya swali hili.
 

Naweza kusema mungu wenu hayupo kama ninavyoweza kisema pembetatu duara haipo katika Euclidean geometry.

Vyote viwili vina an inherent contradiction, they require two mutually exclusive conditions to take place at the same time.

Huwezi kuwa na pembetatu duara kwa sababu pembetatu si duara na duara si pembetatu. Ili kitu kiwe pembetatu inabidi kisiwe duara, na ili kitu kiwe duara inabidi kisiwe pembetatu.

Mungu wenu naye ni hivyo hivyo, ypande mmoja ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote (pembetatu) upande mwingine mnasema kaumba ulimwengu huu unaoruhusu kuwepo kwa mabaya (duara).

Mnapotuambia kuna mungu mwenye uwezo wote, unuzi wote na uoendo wote kaumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya kuwepo, ni sawa na mtu anayetuambia kwamba kuna pembetatu duara.

Anaweza kusema na hata kuifikiria pembetatu duara, lakini hilo halimaanishi ipo.

Mnaweza kumsema na kumfikiria huyo mungu, lakini hilo halimaanishi yupo.
 

Kama msingi wa imani yako ni maswali basi mie siwezi kukuzuia endelea. Ila sasa sitajibu tena maswali yenu nje ya huo mfano niliyotoa.

Japo kuna maswali na ambayo hamuwezi kuyajibu na kuna hoja za wazi kabisa, lakini inabaki kuwa suala la Mungu ni la kuamini. Kama mtu anataka akumkubali Mungu kwa kuondoa kabisa suala la imani basi huyo atasubiri sana.
 

Ninachoelewa ni kwamba.

1. Watu bado hatujajua chanzo cha ulimwengu na mwanadamu, tunakitafuta bado.

2. Hata kama hatujajua chanzo cha ulimwengu na tunakitafuta bado, kuna habari fulani tunaweza kuzikataa kwa kutumia akili tu. Mtu akisema ulimwengu uliumbwa na funza aliye kwenye kidole cha babu yake bula uthibitisho wala mantiki tutamuona ana haki ya kuamini hivyo, lakini hiyo habari si kweli.

3. Kutokujua jibu sahihi lakini kujua jibu la uongo ni sawa na kutokujua jibu la square root ya mbili lakini kunua kwamba square root ya mbili ni ndogo kuliko mbili, kwa hiyo mtu akikuambia square root ya mbili ni nane, hata bula kujua square root ya mbili ni nini, utajua hilo jibu la nane si sawa, kwa sababu nane ni kubwa kuliko mbili. Ingawa hujui jibu sahihi, unajua jibu sahihi lipo upande gani wa mbili.

4. Jibu lenu la kwamba kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote aliyeumba ulimwenfu huu na vilivyomo ni sawa na jibu la kusema square root of two is eight. Hata kama sijui ulimwengu ukianzaje na bunadamu katokeaje, hiki jubu lenu najua si sahihi, kwa sababu lipo kwenye the wrong side of logic.

5. Mpaka sasa auo tu hamjajibu maswaki ya logic. Bali hata wasomi wa theolojia wa hiyo dini yenu kama Papa Francis waneshindwa kujibu kama alivyotuonesha Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:

pembetatu haiwezi kua duara ndio,sababu haviingiliani.....je uwezo hauwezi kuingiliana na uumbaji wa dunia yenye mabaya..jaribu kua namantiki please....manake umetoa mfano pembetatu(uwezo) duara(uumbaji wa mabaya)....kwahyo kwaakili yako uwezo hauwezi kuumba mabaya..?
 

Nani mwenye kukitafuta hicho chanzo na amefikia wapi hadi sasa?

Ikiwa unaamini hakuna mungu japo unakubali mapungufu ya kama kutokujua chanzo cha ulimwengu na binadamu lakini bado umeshikilia imani ,sasa mbona imani ya mungu ambayo kwenu mmeona inamapungufu mmeikataa jumlajumja japo kuna mambo ambayo hamuwezi kuyakataa?
 
Last edited by a moderator:

Kuna imani inayopatikana bila maswali?
 

Kwa nini umetaja iwezo peke yake wakati mimi kila nikitaja uwezo nataja na ujuzi na upendo?

Unaelewa maana ya mimi kutaja "uwezo wote, ujuzi wite na upendo wote" kila ninapoandika na nisiseme tu "uwezo wote" ?

Swali langu haliishii kwenye uwezo, nimekuuliza kwa nini mungu mwenye uwezo wote, unuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao unaruhusu mabaya wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?

Wewe umeacha ujuzi wote na upendo wote, unajibu kuhusu uwezo tu.

Hujajibu kwa nini mungu mwenye upendo wote aumbe ulimwengu ambao viumbe wake watateseka wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya na mateso hayawezekani?

Hata baba wa kininadamu tu ambaye ana uwezo na upendo wa kibinadamu wa kuwalisha wanawe akiwaacha na njaa tutamshangaa, sembuse mungu mwenye upendo wote?
 

Swali lako kama unajua kusoma na kufikiri ungeshaona jibu lake katika ulichonukuu.

Tatizo hujui kusoma wala kufikiri.

Unaniuliza kwa nini nimekataa nane si square root ya mbili wakati nishakwambua square root ya mbili ni lazima iwe ndogo kuliko mbili?
 

haya basi MUNGU mwenye uwezo wote,ujuzi wote,upendo wote anashindwa kuumba ulimwengu wenye mabaya?...NDIO au HAPANA....

mfano wa MUNGU kama baba wakibinadamu alishautoa....yule tajiri aliye wapa wanawe malizake..lkn mtoto mmoja alienda nakuzitumia vibaya malizake na kufilisika, baada ya kuishi mtaani kwatabu ilibidi arudi kwa baba yake kuomba msamaha japo awe kijakazi,lkn baba yake alimkaribisha kwa furaha na kumpa matunzo tena kama mwana..

kwa mantiki hiyo,yule mwanae akati anateseka kule mtaani wakati baba yake tajir ilipaswa baba yake kujadiliwa kwann hamjali mwanae.....?

ni baba gani anaye mchekea mwanaye akikosea,ni mtoto gani ataye mshtumu baba yake kumzaa kilema....ni baba gani asiye na maamuzi kiranga...

yy hufanya chochote atakacho,sababu yy ndiye aliyekuumba ana mamlaka kamili juu yako..kama aliruhusu mabaya yawepo duniani,na akakuumba ww kiranga usipate baya hata moja mpka unakufa uwezo huo anao....ulimwengu unavimbunga,mafuriko nakila kitu kibaya lkn sizani kama ushavexperience vngine...na unaweza mpka ukafa yasikuoate hayo...kwann udandie kushtaki kesi za wengine...hayo ndo makusudi take...

unapaswa kuelewa,kuna watakao kufa na ambao hawatakufa...kwahyo unataka kuandamana kwann wengne hawatakufa...au kwann wengine wanapendelewa..je hii sio sifa ya shetani unayo takakufanya....

tafakari kwa umakini kiranga
 

Sawa sijui kufikiri,haya nioneshe hilo jibu mie nisiejua kufikiri.
 

Hiyo tajiri unayemsema alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Mfano wangu wa baba wa kibinadamu umeusoma vizuri au umekurupuka tu?

Bado hujajibu swali.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu wenye kuwezekana vimbunga na matetemeko, vita na njaa, magonjwa na shida nyingi sana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya?
 
I am afraid I am dealing with a very weak kind of reasoning.

Mtu ananiuliza nitadandiaje kesi za wengine wakati hata hanijui na hivyo hana jinsi ya kujua kama nishapatwa na mafuriko au matetemeko etc.
 
Sawa sijui kufikiri,haya nioneshe hilo jibu mie nisiejua kufikiri.

Unauliza kuoneshwa jibu katika post iliyonukuu ulivyooneshwa jibu.

Sio tu hujui kufikiri, hata ukioneshwa ni kwa vipi hujui kufikiri bado huelewi.
 
Unauliza kuoneshwa jibu katika post iliyonukuu ulivyooneshwa jibu.

Sio tu hujui kufikiri, hata ukioneshwa ni kwa vipi hujui kufikiri bado huelewi.

Huyo mzoee tu ndivyo alivyo huwa anauliza asichokijua halafu anasahau kauliza nini na kajibu nn
 
Huyo mzoee tu ndivyo alivyo huwa anauliza asichokijua halafu anasahau kauliza nini na kajibu nn

huyo ni ishmael kaja na ID nyingine mzee wa kujitoa ufaham!!! anabisha tu kama ubishan wa mpira hata timu ikiwa mbovu unaibishia tu ila dawa zinamuingia make no mistake!!!
 
Unauliza kuoneshwa jibu katika post iliyonukuu ulivyooneshwa jibu.

Sio tu hujui kufikiri, hata ukioneshwa ni kwa vipi hujui kufikiri bado huelewi.

Jibu maswali mkuu,tatizo lenu hamtaki kuulizwa maswali mnapenda nyie tu muulize maswali.
 
Jibu maswali mkuu,tatizo lenu hamtaki kuulizwa maswali mnapenda nyie tu muulize maswali.

Nijibu swali gani ambalo sijalijibu?

Suala hapa siyo mimi kujibu maswali, najibu maswali, unanukuu jibu na kunitaka nijibu swali ambalo jibu lake umelinukuu.

Suala hapa ni, nikikujibu maswali una uwezo wa kulielewa jibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…