Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwa nini mungu aruhusu watoto zeruzeru wakatwe viungo vyao vya mwili na kupewa vilema vya maisha huku wengine wakiuliwa kabisa kisa tu eti kuna watu wenye imani ya kwamba vipande vya miili ya hao watu wenye ulemavu wa ngozi sijui huleta utajiri...(halafu, kama hiyo imani ingekuwa ni ya kweli basi hao zeruzeru si ndo wangekuwa matajiri wakubwa sana hapa duniani...?)
Kwanza, kwa nini hata huyo mungu aruhusu kuwepo na watu wenye ulemavu wa ngozi? Kama anajua huo ulemavu wao wa ngozi utawaletea kila aina ya madhila hapa duniani kwa nini asiliepushe hilo tokea mwanzo?
Yeye si ni muweza wa yote? Yeye si ndo muumba wetu? Sasa kwa nini wengine awaumbe na kasoro zitakazokuja kuwaletea shida chungu nzima hapa duniani?
Kwa kweli hizi habari za uwepo wa mungu pamoja na uwezo wake ukizipitisha kwenye jaribio la kimantiki zinafeli vibaya mno!
Zinafeli vibaya mno.
Tatizo watu washakunywa maji ya dini mengi sana hawawezi kukubali ukweli. Na hata wakiujua wana cognitive dissonance inayoweza kutunga sababu zozote za kipuuzi kama "mtihani" ilu kutetea uongo.
Mungu mwenye kujua yote anahitaji mtihani kwa nini?
Na kama matatizo ni mtihani kweli mbona wengine wanakufa tumboni kabla hata ya kupata nafasi ya kutahinuwa, huju wengine wakifa wachanga.
Hata hilo baraza la mitihani lingekuwa linachagua watu randomly na kusema wewe una namba ya mtihani lakini hutafanya mtihani watu wasingeelewa, sembuse mungu mwenye haki zote, uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?