Mkuu
Kiranga kwanza nashangaa kwa mtu mwenye akili tumamu, mwenye afya kutosha ya Mwili na Akili,(kwa kweli chizi hawezi kuandika yote haya) Kupinga uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa hoja kama hizi...!!!
Kwa uelewa wako wewe, kabla ya Mwanadamu wa kwanza kilikuwapo nini? Na nini msingi mkuu wa huyu Mwanadamu wa kwanza? Na huo msingi wa Mwanadamu wa awali ulijengwa/tokana na nini? Mean nini source ya Ulimwengu na vyote vilivyomo? (Naomba majibu Mujarabu kwa hoja hizi tafadhari)
Kwa hoja zako hapo juu, juu ya Mungu kuumba dunia yenye uwezekano wa kutokea ama kufanyika mabaya......, Mimi kwa uelewa wangu (kutokana na mafunzo ya dini yangu ya Kikristu) naweza kukujibu kama ifuatavyo...
Mungu hakuumba mabaya wala uwezekano wa kufanyika hayo ktk ulimwengu huu na ndiomaana ktk maandiko tunasoma "Na tazama kila alichokiumba ni chema sana" Naam kila kilichoumbwa na Mungu ni chema..!!
Kwanini basi ktk wema huo yanatokea mabaya??
Naam ni UASI WA MWANADAMU. Mungu alipomuumba Mwanadamu (Adam) na kumweka ktk bustani ya Eden na kisha kumpatia msaidizi (HAWA) Lengo lilikuwa aishi milele na kuifurahia dunia na vyote vilivyomo..!!! (Hakika asingekutana na Mabaya) Ila kutokana na Uasi alioufanya Adam kupitia kwa Mkewe akidanganywa na Nyoka, Ghadhabu ya Mungu ikawaka juu ya Mwanadamu. Na ndipo Biblia inasema Mungu kwa kutambua kwamba huyu Mwanadamu kasha Asi (Kwa kula tunda alilokatazwa na Mungu) na hivyo kujitambua ndipo sa akampa adhabu ya kwanza (kumtoa nje ya Bustani) Na kisha akamwambia "Kwa jasho utakula na mkewe apewa adhabu kama ilivyo kwa Mumewe akasema kwa uchungu utazaa...!!!
Tangu enzi za Adam mpaka kwa wanae (Kaini na Abel) dunia imekuwa ya uasi uasi Dunia imejaa maovu si kutokana na Kuumbwa na Mungu bali kutokana na Dhambi iliyofanywa tangu mwanzo na wazazi wetu (Uasi) Tinashukuru Mungu mwingi wa rehema baada ya maasi kuzidi duniani akamtuma mwanae wa pekee (Yesu Kristu) aje atukomboe sisi na dhambi zetu (Naam kwa kupigwa kwake sisi tumepona)
Kwahiyo pamoja na kwamba mengi yanayotokea hapa duniani si kwa mapenzi yetu sisi wanadamu, Ila lililowazi ni kwamba UASI KWA MUNGU wetu ndiyo chanzo cha yote haya na si kusindws kwa Mungu kuyazuia haya...!!! Mungu kakuleta duniani ili umtumikie,Umpende na hatimaye uweze kufika kwake Mbinguni. Ni kwa kumpenda na kumtumikia Mungu huwezi Kumwibia Mwenzako,Huwezi kumuua mwenzako,Huwezi kumdanganya kwa hila lengo likiwa kujipatia Mali,afya,ajira na vitu vinavyofanan na hivyo. NI KWASABABU HAYA YOTE MUNGU KATUKATALIA. Ila kutokana na kuendelea kumuasi Mungu wetu ndiomaana mpaka leo unaona Maovu yanaendelea kutokea duniani.
BACK TANGANYIKA