COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

interesting....kwani ni lazima umpime ndipo ujue kuwa yupo....unaamini kuwa una akili au brain?
umeshawahi kuipima akili yako au brain yako?
how hard is it to believe Something you can not see or measure exists if you believe una akili and your head has brain while you have never seen your own brain or measured your own akili?

Nani kakwambia akili haipimwi?

Na kwa nini ufikiri akili haipimwi?

Unaposikia "kupima" unaelewa nini? Unaelewa kupima kwa kutumia tape au mizani?

Umesoma objections zangu za kuwepo kwa mungu? Unaelewa napinga uwepo wa mungu kwa sababu gani?
 
Binadamu hawezi kumpima mungu kwa vipimo vya kibunadamu, wewe unampima mungu jwa vipimo gani?

Na wewe kama binadamu unaweza vipi kuhakikisha kwamba hutumii vipimo vya kibinadamu kumpima huyo mungu hata pale ambapo unafikiri humpimi huyo mungu kwa vipimo vya kibinadamu?

Kwani wewe unamaanisha nini unaposema kumpima mungu?
 
Nimekuuliza wewe swali halafu wewe unaniuliza mimi tena?

Mimi si umesema siwezi kumpima mungu kibinadamu?

Sawa nimekubali.

Nakuuliza wewe, unavyosema mungu yupo, umetumia vipimo gani ambavyo havijachakachuliwa na ubinadamu wako ili kujua kwamba mungu yupo?
 
Kutambua uwepo wa mungu ni tofauti na kumpima mungu kama ambavyo wewe unafanya.

Najua kuwa waislamu na wakristo hutofautiana kwa wakristo kusema Yesu ni mungu na waislamu kusema Yesu si mungu na wote wanaamini uwepo wa mungu, lakini waislamu wanaposema Yesu si mungu, si tu kwa sababu ya kutumia akili ya kawaida(kipimo) bali husema Yesu amekosa sifa za Mungu na ndiyo husema Yesu hakuwa Mungu.

Sasa wewe unapinga hizo sifa za Mungu kabisa,na ndiyo maana nilikwambia hoja yako hiyo utaitumia kwa kumpinga tu mungu ila si hoja ya kutoa ushahidi ya kutokuwepo kwa mungu. Na wala haina athari yeyote mtu ambaye anaamini labda kwa yule ambaye imani yake kwa mungu ni ya mashaka. Hii ni kwa sababu kuna mambo na ishara mbalimbali zenye kumfanya mtu aamini mungu kabla hata ya kuzijua hizo sifa zote za mungu.
 
Utatambuaje uwepo wa mungu bila kumpima?
 
Ndiyo maana nikakuuliza kwani wewe unakusudia nini unaposema kumpima?

Kimsingi kufikiri ni kupima.

Hata ukilifikiria ua tu umeshalipima katika jicho la mawazo yako kama ni jekundu au la hudhurungi.

Sasa utawezaje kumfikiria mungu bila kumpima?

Na kama binadamu hawezi kumpima mungu kwa mawazo yake, wewe umetumia nini kujua mungu yupo?
 
Mie sikumjua mungu kwa kumpima,ila kuna mambo mengi ambayo ukifikiri au kuyapima ndiyo yanafanya watu waamini uwepo wa mungu.

Mfano hilo ua ambalo unalipima na kujua kama ni jekundu au hudhurungi,unafanya hivyo kwa kuwa unalijua lakini kama ungekuwa hulijui ungepimaje!

Kwa kifupi niseme tu kwamba Mungu hatuwezi kumhoji ni kwa nini amefanya hivi na kwanini asifanye vile, ila unaweza ukataka kujua hekima yake ya kufanya hivyo alivyofanya lakini sio kwanini amefanya hivi na hakufanya vile.
 
Kwa nini usiweze kumhoji?

Kama yeye ni mungu yuko sawa, wa haki, kwa nini asihojiwe?

Utawezaje kutaka kujua hekima zake kwa kweli bila kumuhoji?
 
Kujua hekima na kuhoji kwa kuona kama Mungu amekosea hivyo ni vitu viwili tofauti. Ikiwa mtu tu hawezi kumhoji mzazi wake je,vp kwa Mungu ambaye ni mjuzi wa yote?

Hata hivyo mkuu sidhani utaweza kumjua mungu kwa kutaka kujua hekima ktk mambo yake,kwanza ungefanya umjue kwanza ndiyo utake kujua hekima.
 
Nani kakwambia mtu hawezi kumuhoji mzazi wake?

Kwa nini hawezi? Is there a law of nature that takes the words out of your mouth and the thoughts out of your head if you start to question your parent?

Hujathibitisha kwamba mungu yupo, na kabla hujathibitisha hiko, habari zako zote za kuwapo kwa mungu hazina tofauti na hadithi.
 
Mkuu mie nataka unieleze ni vp hakuna Mungu?

Zingatia swali.
 
Hujajibu nilichouliza unataka nikujibu wewe?

Nishaeleza huyo mungu wenu anajipinga kama pembetatu duara katika Euclidean geometry.

Hawezi kuwepo kwa sababu kabla ya kupingwa na yeyote idea yenyewe ya mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu inapingana na ulimwengu tunaouona.

This is an ungodly contradiction.
 
Hujajibu nilichouliza unataka nikunibu wewe?

Nishaeleza huyo mungu wenu anajipinga kama pembetatu duara katika Euclidean geometry.

Hawezi kuwepo kwa sababu kabla ya kupingwa na yeyote idea yenyewe ya mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu inapingana na ulimwengu tunaouona.

This is an ungodly contradiction.

Ndiyo maana nikasema zingatia swali,Ingekuwa hoja za kuonesha uwepo wa mungu zinajipinga labda hapo ndiyo ungeeleweka lakini kuacha kote na kwenda kurukia sifa za mungu na kusema zinajipinga bado haijawa hoja ya kuonesha hakuna Mungu,ukizingatia pia nimeshakuonesha sifa zengine za Mungu zenye kuelezea ukali wake,hivyo hoja yako inakosa maana.

Unachokifanya wewe ni sawa na mfano mie niwe ninasema kuwa nina nyumba na kujisifu kuwa mimi ni msafi. Halafu siku nikakupeleka kwn nyumba na kukwambia hii ndiyo ile nyumba yangu.Lakini nyumba yenyewe ukaikuta ni chafu halafu et kwa sababu umeikuta nyumba chafu ndiyo iwe hoja ya kusema kuwa hiyo nyumba si yangu kwa sababu mie nilisema ni msafi.
 
Mungu anayejipinga na kukosa consistency hawezi kuwapo.

Kama wewe umesema ni msafi, na una nyumba, na umenipeleka kwenye nyumba ambayo ni chafu, ama hiyo nyumba si yako ama wewe si msafi.

Wewe kama "wewe msafi na mwenye nyumba hiyo" huqezi kuwapo, the two are mutually exclusive.

Strictly speaking, hiyo nyumba haiwezi kuwa yako, na wewe ukawa msafi, na nyumba ikawa chafu. That is a contradiction.
 
Kwa kurasa tatu za mwanzo za uzi huu, ambazo Kiranga na stroke walikuwa wanaulizana, nimeshuku kuwa Kiranga anaamini kabisa kwa asilimia mia moja kuwa Mungu yupo. Ila kutokana na msimamo wake ambao aliupata baada ya kusoma kitabu fulani cha wachukia Mungu na kujitangaza hadharani kuwa naye anamchukia Mungu kwa kusema 'Mungu hayupo'; baadaye kupata wafuasi wengi...! sasa imemuwia vigumu kukiri kuwa Mungu yupo kwani anaona atawasaliti wafuasi wake pia atakosa tunu anayoipata kutokana na kuwa na ufuasi huo.

Nimemshuku hivyo, kwa sababu Kiranga huyu, kama kweli anataka kuonyesha kwa kutoa ushahidi ya kile anaochokiamini wala asingichelea kufanya hivyo. Yeye anachokifanya ni kujificha kwenye kivuli cha wale wanaojitahidi kudhibitisha uwepo wa Mungu; kudai kutoa ushahidi wa hicho wanachokiamini. Wakisha kitoa yeye anasema huo siyo ushahidi. Kama alivyofanya kwa Stroke akatumia mbinu ya kuhamisha mjadala, anadai Stroke atofautishe 'proof' na 'evidence'. Naendelea kumshuku Kiranga kwa sababu, kama hakubaliani na ushahidi anaopewa, basi yeye atoa sifa za ushahidi (ambao una 'logic') anaoutaka juu ya Uwepo wa Mungu aletewe kuliko kuendelea kukataa ushahidi. Akisha fanya hivyo na yeye bila blah blah za habari alete ushahidi wake wenye logic juu ya kutokuwepo Mungu. Ushahidi wake usiwe na mizengwe ya matumizi magumu ya lugha ama ya kigeni ama ya kiswahili.

Akifanya hayo hapo juu, Nitakupunguza kumshuku juu ya msimamo wake.
 
Mungu anayejipinga na kukosa consistency hawezi kuwapo.

Kama wewe umesema ni msafi, na una nyumba, na umenipeleka kwenye nyumba ambayo ni chafu, ama hiyo nyumba si yako ama wewe si msafi.

Wewe kama "wewe msafi na mwenye nyumba hiyo" huqezi kuwapo, the two are mutually exclusive.

Strictly speaking, hiyo nyumba haiwezi kuwa yako, na wewe ukawa msafi, na nyumba ikawa chafu. That is a contradiction.

Je,hiyo nyumba kuwa chafu ndiyo inatosha kuwa ni ushahidi kuwa mie hiyo nyumba sio yangu?
 
What premise and parameters are you using as your basic tenets?

"Unachokifanya wewe ni sawa na mfano mie niwe ninasema kuwa nina nyumba na kujisifu kuwa mimi ni msafi. Halafu siku nikakupeleka kwn nyumba na kukwambia hii ndiyo ile nyumba yangu.Lakini nyumba yenyewe ukaikuta ni chafu halafu et kwa sababu umeikuta nyumba chafu ndiyo iwe hoja ya kusema kuwa hiyo nyumba si yangu kwa sababu mie nilisema ni msafi."

Ulipaelewa hapo?
 
Back
Top Bottom