COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Ni kweli kuna vitu sivijui wala hujakosea

Inawezekana siwezi kumjua Mungu kwasababu sina uwezo huo,lakini naweza kujua mambo ambayo yanaweza kunionesha kwamba yupo lakini pia najua mambo yanayomhusu Mungu ambayo yameniongoza kujibu maswali yako yote

Sijapata kukujibu hivyo mahali popote,labda uwe unaota ....

Nishakuambia kwamba sikatai kwamba kuna vitu sijui nashangaa unaendela tu kulalama
Hatujampachika Mungu majibu rahisi labda huyo Mungu ni wa kwako wewe na sio ninaemjua mimi kwasababu hakuna mwenye uwezo huo

Sikupi na sina haja ya kufanya hivyo kwasababu nilishafanya hivyo zaidi ya mara tano na haikusaidia,tena hili nilianza kulifanya mwaka juzi huko kwenye uzi wa GAZETI na hukuelewa,kitu gani kikufanye uelewe leo?

Denial itakumaliza wewe ....

CC: Ishmael .....!!
Kiongozi, umemshika pabaya sana huyu.
1. Kwanza yeye hajui kuwa hajui anacho bisha na hana ushahidi wa asicho kijua.
2. Kamwe hawezi kukupa ushahid wa anacho jua kuwa Mungu hayupo.
3. Kama anajua Mungu hayupo, kwanini hakupi ushahidi wewe usie jua kuwa hakuna Mungu?
 
Kitu ambacho mpaka sasa hujaelewa au hutaki kuelewa ni kwamba, mimi sio kwamba nataka mungu angeumba ulimwengu kama ninavyotaka mimi.

La hasha. Ukisema hivyo unathibitisha madai yangu kwamba huelewi hoja yangu.

Hoja yangu si kwamba mungu hajaumba ulimwengu ninaotaka mimi.

Hoja yangu ni kwamba huyo mnayemsema kuwa mungu hajaumba ulimwengu ambao unafanana na sifa zake.

Swali ni.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote (sifa zote hizi zinamtaka aumbe ulimwengu ambao hauwezwkaniki kiwa na mabaya) kaensa kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Huu si ulimwengu ambao ninautaka mimi, ni ulimwengubunaotakiwa kuwepo kimantiki kwa sifa za huyo mungu wenu mwenyewe.

Sasa mbona ulimwengu ulioumbwa na huyu mungu unapingana na sifa zake huyu mungu?

Hoja yako dhaifu.
 
Kiongozi, umemshika pabaya sana huyu.
1. Kwanza yeye hajui kuwa hajui anacho bisha na hana ushahidi wa asicho kijua.
2. Kamwe hawezi kukupa ushahid wa anacho jua kuwa Mungu hayupo.
3. Kama anajua Mungu hayupo, kwanini hakupi ushahidi wewe usie jua kuwa hakuna Mungu?
Mkuu huyu jamaa anachosha kabisa,hana mpya!
 
Kiongozi, wewe endelea kumuomba akupe ushahidi wa anachojuwa kuwa Hakuna Mungu. Kama hawezi basi mpe dawa yake ya kuwa yeye ni mfuata mkumbo.
 
First thing first elewa naongelea uwezekano wa mabaya kufanyika, sio tu mungu kuumba mabaya.

Hata ukisema mungu hakuumba mabaya, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kufanyika?

Chukulia muda. From our perspective, hatuwezi kurudi nyuma kwenye muda. Tunaenda mbele tu.

Mnaoamini mungu mnaamuni kwamba hivyo ndivyo mungu alivyouumba ulimwengu.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama ambavyo hatuwezi kurudi nyuma katika muda?

Mkuu Kiranga kwanza nashangaa kwa mtu mwenye akili tumamu, mwenye afya kutosha ya Mwili na Akili,(kwa kweli chizi hawezi kuandika yote haya) Kupinga uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa hoja kama hizi...!!!

Kwa uelewa wako wewe, kabla ya Mwanadamu wa kwanza kilikuwapo nini? Na nini msingi mkuu wa huyu Mwanadamu wa kwanza? Na huo msingi wa Mwanadamu wa awali ulijengwa/tokana na nini? Mean nini source ya Ulimwengu na vyote vilivyomo? (Naomba majibu Mujarabu kwa hoja hizi tafadhari)

Kwa hoja zako hapo juu, juu ya Mungu kuumba dunia yenye uwezekano wa kutokea ama kufanyika mabaya......, Mimi kwa uelewa wangu (kutokana na mafunzo ya dini yangu ya Kikristu) naweza kukujibu kama ifuatavyo...

Mungu hakuumba mabaya wala uwezekano wa kufanyika hayo ktk ulimwengu huu na ndiomaana ktk maandiko tunasoma "Na tazama kila alichokiumba ni chema sana" Naam kila kilichoumbwa na Mungu ni chema..!!

Kwanini basi ktk wema huo yanatokea mabaya??

Naam ni UASI WA MWANADAMU. Mungu alipomuumba Mwanadamu (Adam) na kumweka ktk bustani ya Eden na kisha kumpatia msaidizi (HAWA) Lengo lilikuwa aishi milele na kuifurahia dunia na vyote vilivyomo..!!! (Hakika asingekutana na Mabaya) Ila kutokana na Uasi alioufanya Adam kupitia kwa Mkewe akidanganywa na Nyoka, Ghadhabu ya Mungu ikawaka juu ya Mwanadamu. Na ndipo Biblia inasema Mungu kwa kutambua kwamba huyu Mwanadamu kasha Asi (Kwa kula tunda alilokatazwa na Mungu) na hivyo kujitambua ndipo sa akampa adhabu ya kwanza (kumtoa nje ya Bustani) Na kisha akamwambia "Kwa jasho utakula na mkewe apewa adhabu kama ilivyo kwa Mumewe akasema kwa uchungu utazaa...!!!

Tangu enzi za Adam mpaka kwa wanae (Kaini na Abel) dunia imekuwa ya uasi uasi Dunia imejaa maovu si kutokana na Kuumbwa na Mungu bali kutokana na Dhambi iliyofanywa tangu mwanzo na wazazi wetu (Uasi) Tinashukuru Mungu mwingi wa rehema baada ya maasi kuzidi duniani akamtuma mwanae wa pekee (Yesu Kristu) aje atukomboe sisi na dhambi zetu (Naam kwa kupigwa kwake sisi tumepona)

Kwahiyo pamoja na kwamba mengi yanayotokea hapa duniani si kwa mapenzi yetu sisi wanadamu, Ila lililowazi ni kwamba UASI KWA MUNGU wetu ndiyo chanzo cha yote haya na si kusindws kwa Mungu kuyazuia haya...!!! Mungu kakuleta duniani ili umtumikie,Umpende na hatimaye uweze kufika kwake Mbinguni. Ni kwa kumpenda na kumtumikia Mungu huwezi Kumwibia Mwenzako,Huwezi kumuua mwenzako,Huwezi kumdanganya kwa hila lengo likiwa kujipatia Mali,afya,ajira na vitu vinavyofanan na hivyo. NI KWASABABU HAYA YOTE MUNGU KATUKATALIA. Ila kutokana na kuendelea kumuasi Mungu wetu ndiomaana mpaka leo unaona Maovu yanaendelea kutokea duniani.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

Hoja zako zinakosha nguvu ukitazama vitu viwili.

Kwanza kabisa, kutokujua mwanadamu kaanzaje si kuthibitisha kwamba mungu yupo. Mimi siwezi kisema najua chanzo cha mwanadamu, lakini haiyumkiniki mwanadamu akawa kaumbwa na huyo mungu mnayemsema. Kwa sababu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na yoendo wote hawezi kutengeneza kiumbe anaye produce so much waste na asiye energy efficient.

Pili ukisema kila kilicho intelligent na complex kimeumbwa na kukicho intelligent na complex zaidi, utahikuta unaingia katika mtego wa jutaka mungu wako naye awe kaumbwa na mungu, na mungu wake awe kaumbwa ba mungu. Hivyo hivyo bila mwisho. Mungu wako anakuwa kigurudumu kidogo katika madhine isiyo mwisho, anakosa uungu, anakuwa kidudu tu mwenye moungu wasio hesabu.

Kuhusu habari ya mungu kutoruhusu uwezekano wa kufanyika mabaya, ukisema mungu hajaumba mabaya wala kuruhusu mabaya kufanyika, ila yamewezekana na yakafanyika na binadamu, hapo unatuambia kwamba mungu hana final control na ulimwengu. Wanadamu na shetani wanajifanyia tu tofauti na alivyoruhusu yeye na wanafanikiwa.

Huyo so mungu muweza yote, huyo ni katuni tu.
 
Last edited by a moderator:
In context, using set theory and venn diagrams if possible.

Kama mungu mnasema anapenda kuwapa watu uhuru, na mimi ningependa kuwa na uhuru wa kirudi nyuma katika muda, nikiuliza kama kweli mungu anapenda kuwapa watu uhuru mbona hajanipa mimi uhuru wa kirudi nyuma katika muda kama njia ya kuhoji habari yenu kwa kutumia "immanent critique" utasema namlazimisha mungu aumbe ulimwengu ninaoutaka mimi?

Matakwa yangu yakiwa ni subset ya sifa ya mungu ya kupenda watu wawe huru kuamua watakayo, na mimi nikisema nataka uhuru wa kurudi nyuma katika muda utasema nampangua mungu kuumba ulimwengu ninaoutaka mimi?

Baba yako akikwambia ana shilingi laki mbili za kukuwezesha wewe kufanya shopping yoyote utakayo, ukisema unataka kununua viatu kwa hela hiyo, utakuwa umemlazimisha baba yako kufanya chochote wakati alishasema anakupa uhuru wa kuamua tayari?

hata baba yako alikupa uhuru ufanye utakalo..je unaweza kuingia kulala chumbani kwake?
 
Hoja zako zinakosha nguvu ukitazama vitu viwili.

Kwanza kabisa, kutokujua mwanadamu kaanzaje si kuthibitisha kwamba mungu yupo. Mimi siwezi kisema najua chanzo cha mwanadamu, lakini haiyumkiniki mwanadamu akawa kaumbwa na huyo mungu mnayemsema. Kwa sababu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na yoendo wote hawezi kutengeneza kiumbe anaye produce so much waste na asiye energy efficient.

Pili ukisema kila kilicho intelligent na complex kimeumbwa na kukicho intelligent na complex zaidi, utahikuta unaingia katika mtego wa jutaka mungu wako naye awe kaumbwa na mungu, na mungu wake awe kaumbwa ba mungu. Hivyo hivyo bila mwisho. Mungu wako anakuwa kigurudumu kidogo katika madhine isiyo mwisho, anakosa uungu, anakuwa kidudu tu mwenye moungu wasio hesabu.

Kuhusu habari ya mungu kutoruhusu uwezekano wa kufanyika mabaya, ukisema mungu hajaumba mabaya wala kuruhusu mabaya kufanyika, ila yamewezekana na yakafanyika na binadamu, hapo unatuambia kwamba mungu hana final control na ulimwengu. Wanadamu na shetani wanajifanyia tu tofauti na alivyoruhusu yeye na wanafanikiwa.

Huyo so mungu muweza yote, huyo ni katuni tu.

hizo porojo zote zinathibitisha wapi MUNGU hayupo?
 
Ukweli kwamba hujajibu nilichoandika na umeamua kuziita kwa jumla tu "porojo" unaonesha huna majibu kwa hoja zangu.

Kilichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, kwa sababu hakipo ili kuweza kuthibitishwa.

Kilichopo ndicho kinathibitishika.

Ndiyo maana polisi wakienda nyumbani kwa mtu anayetuhumiwa kuwa na madawa ya kulevya hawamtaki athibitishe kwamba hana madawa ya kulevya, hakuna uthibitisho kama huo. Wao polisi wanaosema kuna madawa ya kulevya ndio wanaotakiwa kuthibitisha yapo kea kufanya search mpaka kuyapata.

Vivyo hivyo, huwezi kuniuliza mimi nithibitishe kwamba mungu hayupo, utakuwa kama polisi anayemtaka mtuhumiwa athibitishe kwamba hana madawa ya kulevya nyumbani kwake.

The onus of proof is on the one who says there is something, not the one opposing that.

The one opposing that has to only question the theory.

The trouble with you is that you are way out of your depth.

Kwa msingi huu, wewe ndiye unatakiwa kutoa uthibitisho kwamba mungu yupo.
 
hata baba yako alikupa uhuru ufanye utakalo..je unaweza kuingia kulala chumbani kwake?

Baba yangu alinipa uhuru nifanye nitakalo wapi?

Baba yangu anawezaje kunipa uhuru nifanye nitakalo wakati yeye mwenyewe hana uhuru wa kufanya atakalo?

Mungu wako analala na mkewe kama baba yangu?
 
Yako ambayo hata haijaonesha udhaifu wa yangu dhaifu uko wapi ni dhaifu zaidi.

Kwa maana imeshindwa hata kuonyesha udhaifu wa hoja dhaifu uko wapi.

Nimeshakuonesha udhaifu wa hoja yako kwa kukupa sifa zengine za Mungu ambazo zinafanya hoja yako kuwa haina maana kabisa.

Kwa sababu mungu ana sifa zake nyingi tu pamoja na huo upendo na uwezo wote.Sasa unapokuja na Mtazamo wako wa ulimwengu ambao wewe unaona ungeendana na sifa ya upendo aliyonayo mungu,ndiyo hapo hoja yako inapokuwa haina maana kwa sababu huo mtazamo wako(aina ya ulimwengu ambao ungetaraji uwe kwa sababu ya upendo wa mungu) utakuwa unapingana na sifa zengine za mungu.

Mungu ameshaeleza kuwa yeye ndiyo mwenye kukipa uhai kiumbe na yeye ndiyo mwenye kukitoa uhai kiumbe,hakuna mwengine mwenye sifa hiyo. Sasa ukija kulalama kwanini watu tunakufa et halafu mungu amesema anaupendo, Mi ndiyo napokushangaa.
 
Sifa zingine zipo ambazo zitapingana na mtazamo wangu?

Na kama sifa hizo zitapingana na huo unaousema kiwa ni mtazamo wangu, ambao kiukweli si mtazamo wangu bali ni mtazamo unaotokana na sifa za mungu, huoni kwamba mungu huyu atakuwa na sifa zinazopingana?

Huku tunaambiwa ana upendo wote, huku tunaambiwa atawapatiliza waliomkosea kizazi hata kizazi.

Huku tunaambiwa ni mungu wa haki, huku tunaambiwa atawahukumu wana kwa makosa ya baba na babu zao.

Huku tunaambiwa ana upendo wote, huku tunaambiwa kwamba atawachoma moto viumbe wake aliowaumba yeye mwenyewe bula kuombwa, kwa milele na milele.

Hii si ndiyo habari ninayoisema kila siku? Kwamba mungu wenu hawezi kuwepo kwa sababu yeye mwenyewe, kabla hatujataka kumpinga, kashaanza kujipinga mwenyewe!
 
Kwanza kabisa kumbuka tunamzungumzia Mungu,sasa huko kujipinga unakosema wewe ni kwa kutumia vipimo vya kibinadamu kusema mungu kajipinga? Sie binadamu tunatofautiana ktk vipimo vya jambo jema na ovu,sasa kwa udhaifu huu kweli ndiyo tunaweza tukatumia kumpimia na mungu?
 
Binadamu anaweza kumpima mungu au hawezi?

Maana isije kuwa unasema binadamu hawezi kumpima mungu nikiongelea mungu anavyojipinga tu, huku vitabu vya dini vimejaa maandishi ya binadamu wakimsifu mungu kwa mazuri, wale waliomsifu mungu kwa mazuri hawajampima mungu?

Pia, kabla ya kusema sana kuhusu mungu, unapaswa kuhibitisha kwamba yupo. Utathibitishaje kwamba mungu yupo kama binadamu hawezi kumpima mungu?

Unaposema kwamba mungu yupo unasemaje hivyo bila kumpima?

Unaposema kwamba mungu yupo na hapo hapo ukasema kwamba binadamu hawezi kumpima mungu unajuaje kwamba habari nzima ya mungu kuwepo si hadithi ya mapokeo tu isiyo na uhalisi?
 
hahhaa, kwa hiyo kukutana wewe na jirani yako kukutana barabarani kunathibitishaje uwapo wa mungu? hilo bichwa lako linashindwa hata kutafakari na kutafiti ni kwa nini mnatoka muda mmoja kuelekea kwenye mihangaiko yenu? halafu nilivyokuwa naandika hii reply nimejamba, lazima mungu atakuwepo.:lol:

Jf bwana ni haichoshi
 
Binadamu anaweza kumpima mungu au hawezi?

Maana isije kuwa unasema binadamu hawezi kumpima mungu nikiongelea mungu anavyojipinga tu, huku vitabu vya dini vimejaa maandishi ya binadamu wakimsifu mungu kwa mazuri, wale waliomsifu mungu kwa mazuri hawajampima mungu?

Pia, kabla ya kusema sana kuhusu mungu, unapaswa kuhibitisha kwamba yupo. Utathibitishaje kwamba mungu yupo kama binadamu hawezi kumpima mungu?

Unaposema kwamba mungu yupo unasemaje hivyo bila kumpima?

Unaposema kwamba mungu yupo na hapo hapo ukasema kwamba binadamu hawezi kumpima mungu unajuaje kwamba habari nzima ya mungu kuwepo si hadithi ya mapokeo tu isiyo na uhalisi?

Nimesema huwezi kumpima mungu kwa vipimo vyetu vya kibinadamu. Na nikasema kwamba sie binadamu hutofautiana kwenye kipimo cha kutizama ni lipi jambo jema na lipi jambo ovu,ndiyo maana nikasema ktk hali kama hii tutawezaje kumpima mungu!

Na maana ya "kumpima mungu" hapo nimemaanisha huko kusema kuwa amejipinga au kuona amekosea.Mfano mzuri kama hiyo sifa ya uweza wote, haujaipima sifa hiyo ktk kipimo cha kibinadamu.

Tatizo unapotaka kulazimisha kuwa mungu kajipinga ili ndiyo iwe ushahidi wa kutokuwepo kwa mungu Hapo ndiyo unapokwama.
Hoja yako utaitumia kupingia mungu ila haiwezi kuwa ndiyo ushahidi wa kuwa hakuna mungu kwa hoja hiyo,bado sijaona hoja ya kuonesha kuwa hakuna mungu.
 
interesting....kwani ni lazima umpime ndipo ujue kuwa yupo....unaamini kuwa una akili au brain?
umeshawahi kuipima akili yako au brain yako?
how hard is it to believe Something you can not see or measure exists if you believe una akili and your head has brain while you have never seen your own brain or measured your own akili?
 
Ndio kwanza natua mjengoni, Wadau wote, wana JF wote na wengine wote poleni kwa kazi ndefu ya kuelimisha jamii. Kwa kweli nimejua mengi na kujifunza nisiyo yajua kutoka kwenu, Hii nikutokana na kujituma kwenu kwa dhati kwa nia ya kuelimisha uma, kwa yale yasiyo fahamika. lengo hasa la kuandika hivi, nikutaka kusema kuwa Jitihada zenu za dhati ndio zitaweza kuelimisha wana taifa. Mwisho kabisa naamini kuwa hakuna umbali katika kuombeana hali njema, afya njema ili tuzidi kusimama imara na kutetea mambo ya busara na yakweli..
 
Nimesema huwezi kumpima mungu kwa vipimo vyetu vya kibinadamu. Na nikasema kwamba sie binadamu hutofautiana kwenye kipimo cha kutizama ni lipi jambo jema na lipi jambo ovu,ndiyo maana nikasema ktk hali kama hii tutawezaje kumpima mungu!

Na maana ya "kumpima mungu" hapo nimemaanisha huko kusema kuwa amejipinga au kuona amekosea.Mfano mzuri kama hiyo sifa ya uweza wote, haujaipima sifa hiyo ktk kipimo cha kibinadamu.

Tatizo unapotaka kulazimisha kuwa mungu kajipinga ili ndiyo iwe ushahidi wa kutokuwepo kwa mungu Hapo ndiyo unapokwama.
Hoja yako utaitumia kupingia mungu ila haiwezi kuwa ndiyo ushahidi wa kuwa hakuna mungu kwa hoja hiyo,bado sijaona hoja ya kuonesha kuwa hakuna mungu.

Binadamu hawezi kumpima mungu kwa vipimo vya kibunadamu, wewe unampima mungu jwa vipimo gani?

Na wewe kama binadamu unaweza vipi kuhakikisha kwamba hutumii vipimo vya kibinadamu kumpima huyo mungu hata pale ambapo unafikiri humpimi huyo mungu kwa vipimo vya kibinadamu?
 
Back
Top Bottom