Hapana,upendo wa binadamu haujashinda upendo wa Mungu
Kwanza fahamu kwamba kumpa kila mmoja kile ambacho anataka ni upendo
Mungu aliumba ulimwengu ambao kila kiumbe kitapata kinachotaka,kwa maana hiyo huo ni upendo,Mungu alipomuumba binadamu na kumuweka duniani alimuambia kwanza ubaya wa kutotii na wema wa kutii,lakini hiyo haikuondoa ukweli kwamba angechagua vinginevyo japokuwa vina madhara kwake angevipata tu kwasababu hivyo ndivyo alivyovitaka basi ni haki yake kupewa kwasababu huo ndio msingi wa upendo
Leo binadamu tunatafuta dawa baada ya kujua ukweli wa maonyo ya Mungu hapo mwanzo ambapo tayari tulikuwa tumeyakaidi,lakini pamoja na kukaidi bado huyu Mungu aliendelea kutafuta namna ya kuturudisha kwenye maisha yale ambayo yeye aliyapanga tangu mwanzo,lakini kwa hiyari bado [upendo mkuu],kwakuwa alishasema atamuadhibu kila mtenda dhambi kwakuwa hiyo ni haki yake kwasababu alikosea kwa kudhamiria na alionywa,Mungu ametengeneza mpango wa kutokumuadhiobu binadamu huyu huyu kwa yeye kuamua kuadhibiwa kwa niaba ya huyu huyu binadamu ambae alionywa kwanza kabla ya kukosea lakini akakaidi na kukosea tena makusudi[bado anaendelea kuonesha upendo mkuu sana]
Kwa maana hiyo,Mungu angeumba ulimwengu ambao kuna mambo hayawezekaniki isingereflect uwezo wake,lakini pia usingekuwa upendo kwasababu kuna watu ambao wasingepata wanachokihitaji na isingekuwa ni upendo kwasababu angewalazimisha wengine kufuata mambo ambayo hawayataki,lakini pamoja na hili usisahau kuwa unapochagua jambo ambalo ni baya madhara yatakupata na utaadhibiwa kwasababu adhabu ni haki yako,hivyo adhabu kwa hawa wanaochagua haya bado ni haki yao kwasababu wamekosea
Mungu ni upendo mkuu sana!