Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Yaani mtu uko hoi kitandani na yeye anajua kabisa kuwa u mgonjwa uliye hoi (na supposedly ana uwezo wa kukuponya) lakini anasubiri hadi umwambie kuwa unataka kupona ndo akuponye?
Kama ni hivyo basi moral compass yangu ni bora kuliko ya huyo mungu.
Aiseeeee :lol::lol::lol::lol::lol::lol:!!!!
Tatizo unadhani kila unachoona kizuri au kinachoonekana kizuri ni kizuri kwa kila mtu au kwa idadi kubwa ya watu,ngoja nikupe tukio lililotokea wala sio siku nyingi ....
Mahali ambapo nimepanga kwa maana ya kuishi kuna jamaa aliwahi kukaa siku mbili bila kula wala kutoka nje,kabla ya kutimiza siku mbili akiwa ndani,kuna jamaa yetu ambae tunaishi nae hapa nyumbani alikwenda kumuuliza kulikoni baada ya kumuona siku moja nzima hajatoka nje na kufanya mambo yake kama alivyozoeleka
Jamaa huyu alikwenda na kumuuliza kulikoni lakini jamaa alimuambia "ana mambo yake tu" hivyo hakuna tatizo lolote,alimuuliza kama hajala jamaa akamuambia kwamba hajala,jamaa alitoka na kwenda kumletea chakula,lakini jamaa aliekjuwa ndani akamuuliza kama amemuambia kama anahitaji chakula,alieleta chakula akamuambia kwamba amemuambia kwamba hajala tangu jana hivyo atajidhuru kwa kukaa muda mrefu bila chakula
Kisha akampa chakula,jamaa alikipokea na kumwagia chakula yule aliemletea na kumuambia asimsumbue tena
Mfano wa tukio hilo unaweza tu kuona kwamba sio kila chekundu ni red na ukifikiri kwa makabala huo ni hatari sana na ndio maana Mungu akaweka free will,kama unahitaji kuponywa mwambie,kwa Munmgu kujua tu kwamba wewe unaumwa na unahitaji kuponywa sio tiketi ya kukuponya kwasababu unaweza kusema na ukaponywa
Lakini pia unapaswa kujua kwamba hata maradhi ambayo mtu anaweza kuugua au anaugua ni matokeo ya uchaguzi wake mwenyewe na anajua kabisa ni mabaya,sasa mtu ulichagua mwenyewe,unatakaje tena uponywe tu bila kusema hitaji lako?