Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,319
Lazima uone nakusumbua sana tu. Nakuuliza maswali ambayo huna majibu yake na hutaki kukubali kwamba huna majibu hayo.
Tukienda na mfano wako kama unavyotaka, tutaona kwamba umeutoa bila kufikiri kwa kina.
Kwani, badala ya kukusaidia kujenga hoja yako, mfano wako unazidi kuibomoa.
Hoja hiyo ya jipu inahusiana na mtu ambaye hana control ya majipu. Jipu linatokea bila ya yeye kuwa na uwezo wa kulizuia, anaanzia hapo kutatua tatizo la jipu kwa kulikamua.
Mungu ambaye ame plan kila kitu kuanzia mwanzo, pamoja na kupanga kama aumbe ulimwengu ambao majipu yanawezekana au hayawezekani, kwa nini kaumba ulimwengu ambao majipu yanawezekana halafu amtoe mwana wake kama njia ya kuyakamua hayo majipu?
Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao majipu hayawezekani kabisa in the first place?
Hoja ni upendo na sio jipu. Nimekuuliza ni utaalamu gani wa kimantiki umetumia kutambua kwamba kuna mkanganyiko Kati ya Mungu na Ulimwengu uliopo.
Au umeota tu.