Mbona unakuwa mkali mkuu ukiulizwa kilichokufanya kuwa atheist?unatoa hadi mipasho.
Halafu suala la contradiction maelezo yangu ya mwisho yalikuwa ni haya:
"Kupinga ni suala rahisi sana kila mara narudia haya maneno.Umekariri kuwa hoja yenu haiwezi kujibiwa na ndiyo maana unahaha. Kumbuka umesha ambiwa kwanini huu ulimwengu upo hivi na kuelezwa kusudio la Mungu, ila wewe unasema mungu hawezi kuumba ulimwengu huu kwa sababu ya sifa yake ya upendo, uwezo wote na ujuzi. Nikakuuliza je,mungu angeumba ulimwengu ambao hauna tabu yeyote ndiyo ingekuwa hajajipinga? Ukajibu ndiyo, nikakwambia je, vp akitokea mtu na kudai kuwa ulimwengu huo utapingana na sifa ya mungu "adh-dhaaru"?? Ukasema ndiyo maana unasema mungu hawezi kuwepo kwa sababu sifa zake zinajipinga.
Mpaka hapo ilikuwa tumefikia
kwamba kumbe hata kama mungu angeumba ulimwengu wenye raha tupu bila tabu yeyote pia ingeonekana anajipinga na sifa zake nyengine pia,kwahiyo hoja hapa si kwanini kaumba ulimwengu huu,maana (kwa vigezo ulivyotumia kusema
ulimwengu huu unamfanya
anajipinga) hata angeumba
ulimwengu unaoona wewe ndiyo ungekuwa unafaa bado pia ingeonekana kuna contradiction.
Ndiyo maana unaambiwa
umemtengeneza mungu ktk kichwa chako,kwa sababu unataka kujua uwepo wa mungu kwa kuchagua baadhi ya sifa,kubali sifa zote hizo maana ndiyo sifa zake hizo."