UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Kinachokushangaza na kukustaajabusha ni nini?
Hapa kama kuna mtu anapost si kwa kutaka kueleweka basi ni wewe.
Maana sehemu ya kusema "nimeshangazwa na majibu yako kwa kuwa hujajibu hiki na huki, na nilitegemea hivi na vile..." umeacha sintofahamu kwa kunitaka nisome tena kitu ambacho hata baada ya kusoma mara mia siwezi kuingia kichwani mwako na kuona inachofikiri wewe.
Hapo sasa ambaye hataki kueleweka kati yako wewe usiyetaka kueleza unachofikiri na mimi ambaye siwezi kuingia kichwani mwako ni nani?
Bado hujathibitisha kwamba mungu yupo.
Hujaeleza imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
"Unajuaje kwamba wewe fikra zako za kwamba ama ulimwengu umeumbwa na mungu ama kutokea wenyewe si fikra za kufuata kitu kama line ya reli
inayoweza kwenda mbele na nyuma tu bila kujua kwamba kuna juu na chini?"
Maelezo yako hayo ndiyo maana mie nikatika unipe japo mfano tu(si kwamba unielezo ulimwengu umepatikana vp)