Nasikia maghorofa ya Chang'ombe (pale kwenye mafundi wa fenicha) yanakarabatiwa soon. Huenda wapangaji hawajaambiwa lakini tetesi zinadai pataboreshwa na hata hao mafundi wa fenicha ambao wameingia hadi milangoni watahamishwa (panaweza kuchimbika kiasi chake) lakini baadae huenda wakajengwa Furniture Mall eneo hilo hilo.Nashauri pia wayaangalie na majengo yaliyopo yanakarabatiwa ili yadumu. Wataalam watumike majengo yasijeanguka tena
Mi nataka tuanze kuongea kisomi mkuu wangu, hujanikwaza. Ni challenge ambayo tunayo kwa sasa kama taifa. Sasa, tukomae tujue status za miradi hii na kama fedha kwa ajili ya miradi hii zipo. Tunaweza kuanza kutembea vifua mbele (hata kama hatuna stake katika projects zenyewe) endapo hii miradi itafanikishwa bila kuvurugwa.
Ikitokea huu ukafanikiwa, wa Kigamboni ukafanikiwa na mingine zaidi, basi kuna afueni tutaiona angalau ukilinganisha na majirani zetu
Adamjee alipewa eneo la kiwanda tu, eneo jingine lipo chin ya kiwanda mfu cha TP ambacho ni mali ya Serikali. Hadi leo waliokuwa wafanyakazi wa TP wapo kwenye nyumba za TP hawajalipwa mafao yao. Kimsingi ni kama wametelekezwa, so nadhan ujio wa picha hizi utaibua hisia mbalimbali kwa washahafishwa wale.
Shukrani kwa serikali ya awamu ya nne. Stay tuned! Mambo mazuri yanakuja na yataendelea kuja chini ya serikali ya CCM.
Kama hutaki maendeleo wewe utakuwa ni mchawi na ukatafute nchi ya kuishi.
Unaonekana kama nawe ni miongoni mwao...
Mkuu,
Si ndoto. Na nikufahamishe ni kuwa tayari eneo la Kawe pale Tanganyika Peckers pamesharejeshwa ardhi kwa asilimia nadhani zaidi ya 50.
FYI, kuna project nyingine inakuja. Tanzanite Mall na itakuwa inaonekana kama inavyoonekana hapa chini (nimefuatilia Brela, naona kuna kampuni imesajili 2011 inaitwa "Tanzanite Mall Ltd" nahisi ndio wenye hii project):
Sasa umesema mwenyewe New Kawe City na picha umeweka kwa upembuzi wako yakinifu..Mwisho unauliza tena kwa anayejua progress hiyo....Pa warum[/QUOTE
Huyu ni CEO wa NHC aliyeweka huu Mchoro. Maana aliingia na Gia ya kudanganyaya watu kuwa angejenga huo mradi Mwaka jana. Sasa baada kuchemsha kwenye jingo lililoporomoka ameanza kudanganya watu na Mchoro wake huo.
Nchi yetu imejaa wezi sana, naona sasa umezuka ufisadi wa aina mpya wa kutuchorea picha/city plans na kupiga hela za walipa kodi. Ukiuliza ni TZS ngap zimetumika katika kudevelop hiyo plan unaweza ukazimia. Kama kweli serikali imedhamiria kuendeleza nchi, kwanini isimalize plan ambayo tayari ipo???? Au kigamboni project imeshaisha???? Pia hiyo ni mbinu tu ya kutuibia lile eneo maana bila mapichapicha ya hivi pale hapaingiliki.
Kama nguvu ya kuendeleza eneo hilo ipo, pls tumalizieni kwanza Kigamboni project kisha tuamie Kawe. Hizi ni namna ya kutuibia hela kwa kujifanya wamelipa mabilioni kwa hao wanaodevelop hizo plan. Wiiiiizi mtupu. Hii serikali ilishajitoaga kwenye uwekezaji, kiherehere tena cha nn kwenye kugharamia maplan ya mabilion haya??? Wapelekeeni madawa na maendeleo bibi zangu vijijini.