kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,105
Yaani huyu jamaa alichosema kinaweza kuwa ni kitu cha msingi lakini hoja yake inaweza kukosa mantiki kwani ametumia MANTIKI kukosoa misingi ya MANTIKI. sasa je ataweza kubaini udhaifu wa misingi ya MANTIKI kwa kutumia misingi hiyohiyo ya MANTIKI anayoikosoa??Nimegundua wewe jamaa una akili sana, Kiranga japo huwa ni vigumu kumshinda katika mijadala kama hii, lakini kwako lazima ajipange vizuri kama akitaka akushinde Kwa hoja.
Ninachoshauri huyu jamaa kama anaona kuna uwezekana wa walioweka misingi walikosea na wakaendelea kuamini mambo katika hiyo misingi basi na atuthibitishie.
Pia katika kujadili hili naomba aweke pembeni REASONING kama kitu kinachoipa hoja LEGITIMACY ya kuwa madhubuti ili akwepe kutumia misingi ya MANTIKI ambayo anaona inaweza kuwa ina walakini. Aje na mtindojenzi wa hoja tofauti na huu wa misingi iliyokosewa na hapo ndipo tutaanza kujadili vizuri.
Kiranga asipojibu swali kuna uwezekano wa mambo kadhaa yanayomkwamisha. Tunapotoka moja kwa moja na kusema amekimbia hoja ya mjadili mwenzake. Tusipende kuhitimisha mambo bila kuyapitisha ktk mchakato.
Sent using Jamii Forums mobile app