Congo DRC, imekuwa kubwa jinga, Tanzania tusijiingize!

Congo DRC, imekuwa kubwa jinga, Tanzania tusijiingize!

Wakongo wanaoongea Kiswahili wameanza kushikwa huko Kinshasa inawabidi waongee Lingala Kongo inaenda kugawanyika vipande viwili. West vs East.
 
A weak DRC means business kwa washindani wetu.Kenya na Rwanda wanataka kuibypass Tz SGR.Rwanda akiimiliki EASTERN CONGO the game is over!!!Soko lote la BURUNDI NA DRC LITAANGUKIA KWA KENYA,UGANGA NA RWANDA.
📌📌📌Tz ilitakiwa iwe imeshaplani kusimika kibaraka wetu hapo DRC.Na kuwa ready kulitetea soko la CONGO at any cost.
Viongozi wetu Hawa wanaolia mama, mama, mamaa Kila siku unadhani kuna wanachoelewa?
 
Rwanda washaanza kutumia mpaka silaha mpya za kivita kama drones na air defence system.Nyie mmekalia PROPAGANDA za enzi ya IDD AMIN ambapo kwa sasa mambo yamebadilika sana.Proxy wars ndio kila kitu mmejipangaje wazee😄😄
Hao akili zao wanadhani Yale makopo kuukuu wayopitisha uhuru ni silaha za kisasa, yaani sisi ni weupe sana hamna kitu, nchi Haina hata MRAP Moja.

Jeshi letu limekaa kizamani sana,
 
View attachment 3243715
Congo DRC wamekuwa kubwa jinga kwa muda mrefu.
Nchi haina umoja
Nchi ni tajiri sana
Nchi haina jeshi hata la watu laki moja
Na majenerali wa Congo ni wa kukata viuno tu, hawawezi hata kujitetea mbele ya vita.
Nchi nzima hii wao ni mayenu tu na kukata viuno

Cha ajabu huyu Rais wao Tsishekedi hajui aanzie wapi kukabiliana na wapinzani wake toka Rwanda.
PK anamnyanyasa kubwa jinga, DRC -Congo.
Hili kubwa jinga limebaki kulia lia kuomba msaada wa kijeshi toka kokote duniane, wao furaha yao ni mayenu tu.

DRC Congo inakera, tena sana.
Ingekuwa ni hapa Tz , hata mimi na umri wangu ningeenda fronti, kama miaka ya kumg'oa Nduli Idi Amin.

Kweli nchi bila umoja inanyanyasika.
kila nikimkumbuka rafiki yangu Mammadou Ndala, nahisi dunia uwanja wa fujo, ni mkongo pekee ambae kama angefanikiwa angeiokoa DRC, bahati mbaya wakamuwahi rafiki yangu😭
 
Wewe unafikiri kuonyesha kisu chako hadharani ni ujanja?
Niambie vita ambayo drones zimeteka nchi!
Urusi yenyewe inapigana man to man kuteka maeneo Ukraine.
Principles za vita, kama hujui, hazijawahi kubadilika!
Hiyo man to man unadhani wanapigana na hayo magole yenu ya mwaka 1940? Hiyo vita ya ukraine hujaona kwa kiasi kikubwa drone zimetumika kuliko vita yoyote?. Jeshi letu linunue silaha za kisasa waachane na Yale makopo ya kizamani.
 
Hao akili zao wanadhani Yale makopo kuukuu wayopitisha uhuru ni silaha za kisasa, yaani sisi ni weupe sana hamna kitu, nchi Haina hata MRAP Moja.

Jeshi letu limekaa kizamani sana,
😄😄😄😄tatizo hawataki kuchalenjiwa na kuambiwa ukweli.Military drills za maana hakuna yaani sisi tukisema tuingie vitani uchumi utasagika ungaunga kama sembe😄😄😄🙌🙌🙌
 
Hiyo man to man unadhani wanapigana na hayo magole yenu ya mwaka 1940? Hiyo vita ya ukraine hujaona kwa kiasi kikubwa drone zimetumika kuliko vita yoyote?. Jeshi letu linunue silaha za kisasa waachane na Yale makopo ya kizamani.
Hakuna maana kubishana na viGnZ ambavyo hata gobole havijui ni nini!
 
Bila Congo hiyo reli inaenda wapi? Rwanda viherehere tunaweza kupeleka reli bado wakatusumbua. Burundi uchumi mdogo. Utulivu wa congo ni muhimu sana kwetu. Congo ni muhimu kwetu kuliko sisi kwao
Reli ya SGR itatumika tu, liwepo Kubwa Jinga au la!
 
Mbinu zenu hizo za zama za kale za mawe🤣🤣🤣 hakuna anayewajali kwa sasa. Wenzenu wanafanya kweli nyie mmebaki na PROPAGANDA na stori za kusadikika😆😆😆
Mkuu mbona unajibaraguza?
Wewe fanya kujikuna, uone moto!
 
Mkuu Tresor Mandala hivi Jean Pierre Bemba ambae ni kiongozi katika serikali hii mbona kimya sana...?? Au ndio hawa wana sabotage harakat za serikali maana wao ni wazee wa misituni by history!!.. nilifikiri wangeweza kuwa msaada au ndio waajiriwa na middle men wa vikundi vya uasi??
 
DRC is a failed state.

Utawala uliopo huko upo dhaifu Sana.
Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo pia lipo dhaifu Sana kupita kiasi.

Jeshi la DRC lipo uchi wa mnyama kwa Utawala wa Rwanda.
Kuna uasi wa chini chini usiokwisha ndani ya Jeshi la DRC.

Wanajeshi wengi sana wa DRC pia ni Wapiganaji wa Siri wa M23.

Viongozi wengi wa Serikali ya DRC pia ni Mawakala wa Siri wa Utawala wa Rwanda na Vikosi vya Waasi wa M23.

Try to imagine: General Kabarebe aliwahi kuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) wa nchi hiyo ya DRC, lakini baadaye Mwanajeshi huyo alihama nchi na kwenda kuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) wa nchi ya Rwanda.
Sahihi kabisa..
 
Ardhi ya congo imelaaniwa...damu nyingi sana ya watu wasio na hatia imemwagika congo....hiyo damu itaendelea kuwalilia mpaka kuhama
 
Wakongo wanaoongea Kiswahili wameanza kushikwa huko Kinshasa inawabidi waongee Lingala Kongo inaenda kugawanyika vipande viwili. West vs East.
Kama jambo hilo litaleta Kutengamaa kwa Amani nchini Congo DRC bora iwe hivyo.
 
Congo DRC ni wateja wazuri wa bandari salama. Tusipojiingiza kwenye migogoro yao basi, machafuko yakakithiri, kukawa hakuingiliki basi tegemea yafuatayo:
1. Wamiliki wa malori wengi watashindwa lipa mikopo yao.
2. Bei za malori ndani ya nchi zitashuka as malori mengi yanayoenda nje ya nchi yatakuwa forced kufanya shughuli za ndani.
3. Madereva wengi na wasaidizi wao watakosa ajira, mnyororo wao ni mrefu sana.
4. Bandali salama itakosa mapato ya mizigo ya Congo DRC.
5. Clearing and Fowarding agents watakosa deals za kuwaweka mjini.
6. Madereva wa transit watakosa ajira.
7. Sekta ya ujenzi itadorora sana, hardwoods tunategemea sana toka Congo DRC.
Etc
Mleta mada anaongea kama mtoto mdogo asiyejua kitu, analaumu mayenu!

Tanzania ina maslahi mapana DRC, kuiacha Kinshasa ianguke kuna madhara makubwa ya kiuchumi kwetu.
 
Niliona katika video moja jamaa kawatatufa waganga na waganguzi na kawaleta pale Ikulu ili wamsaidie katika kupigana hiyo vita. Kama akina Kinjekitile wanatoa uaguzi wao kwamba watashinda vita hiyo. Katika Karne ya 21 bado watu, tena wakubwa, wana Imani za risasi kugeuka maji!
 
Back
Top Bottom