Congo DRC, imekuwa kubwa jinga, Tanzania tusijiingize!

Mweee alifanya kama Nebkadineza? 🤣🤣🤣
 
Ilianza na wazo la East African Community, Organisation of African Unity .....etc
Siyo kuunganisha nchi na kuwa taifa moja,watu walipinga united States of africa Ili walinde madaraka yao,maana wasingekua marais

US of Africa ni ndoto na wazo la kufikirika tu halina uhalisia hata kidogo.

Africa nchi nyingi bado ni nchi (countries) wala si mataifa (nations). There's a significant difference btn the two. Nchi nyingi bado haziwezi kujitawala zenyewe internally leo ziunganishwe itakua ni kupika bomu kubwa zaidi.

Kuna sababu za kiusalama na kiuchumi ambazo hazisapoti unification of Africa. Unaunganisha vp nchi kama Somalia, Congo, Sudan, Nigeria, Mali, Niger, Libya etc kuwa nchi moja? Congo tu hapo rais anaishi Kinshasa hajui kinachoendelea Goma wala Lubumbashi utadhani sio ndani ya mipaka ya Congo. Hata lugha wanazoongea ni tofauti.

Africa is so diverse with different cultures, traditions, languages, values haiwezekani kuunda nchi moja kwenye bara lenye utofauti mpana kiasi hiki. Tunaweza tumia hizi tofauti kuboresha umoja wetu ila sio kuwa nchi moja (Strength in diversity).
 
Wakati Anaingia walimsifia sana, wakasema Kabila hataki kuondoka madarakani, Kanisa katoliki wakamlilia sana huyu, sasa kaingia hata ajulikani ni rais au mwanamuziki?
 
Shida yetu ni kudhurumiana wenyewe kwa wenyewe,haiwezekani nifanye kazi nilipwe kiduchu. Harafu hakuna soko la bidhaa limekaa vizuri,ni Bora hao vita Iko wazi lakini sisi vita ya dhurma.inatia laana mpaka nchi imedumaa
 
Wachoweza wa congo kukata viuno na kupaka Carolite
 
Kongo wamekwama sababu ya corruption na nepotism, haya ni miongoni mwa mambo yanayoondoa umoja kwenye taifa.

Kelele zinazosikika nchini kila siku mara abdul, mara mama nani, tusipobadili mwelekeo kama taifa tutajikuta tumekwama sawa na Kongo.
Acha kuchomekea upumbavu wako kafanye siasa majukwaani
 
U Umeandika utumbo bora ungekaa kimya
 
Stori za kijiweni
 
Nasaport 100%
 
Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa sababu kubwa iliyopeleea DRC kufika hapo walipo ni mgawanyiko wa wao kwa wao ndani ya nchi ukichagizwa na mataifa ya nje.
Kiukweli nachelea kusema hata sisi tusipokuwa waangalifu tunaelekea huko.
Mgawanyiko unaofukuta kati ya wanaotaka mabadikiko na wale ambao hawataki mabadiliko unaweza kutufikisha pabaya.
Tufahamu pia kwamba mataifa ya nje yakishaona kuna hali ya mgawanyiko ndio nayo yanachochea zaidi hali hiyo kwa maslahi yao.
Hapo ndo wagogo wanasema ni point of no return kwa maana Mambo yanakuwa tayari yameharibika.
Cha kufanya kwa Sasa ni kuondoa hizi tofauti zetu kwa amani.
Shida Mimi ninayoiona ni nani atakubali kulegeza msimamo kati ya haya Makundi.
Nadhani kuna haja ya Kila kundi kuja na sababu thabiti ni kwa nini linasimamia linachokiamini na kuwaeleza wananchi Ili mwisho wa siku tuwe wamoja kwa kukubaliana la kufanya kama nchi.
Ni swala gumu ambalo linahitaji kujibiwa na hoja nzito na si hoja nyepesi nyepesi tu zinazolenga kufanikisha makengo ya kisiasa ya kundi hili au lile, Bali ziwe hoja zinazolenga kuleta mstakabali wa kuweka nchi pamoja.
 
Mleta mada anaongea kama mtoto mdogo asiyejua kitu, analaumu mayenu!

Tanzania ina maslahi mapana DRC, kuiacha Kinshasa ianguke kuna madhara makubwa ya kiuchumi kwetu.
Sasa wewe ulitaka sisi tufanye nini, wakati rais wao Kubwa Jinga analia lia tu badala ya kupigana vita.
 
Vijana wa 2000 hawatakuelwa kuwa hili lilitokea miaka ya mwanzoni mwa 60s
 
Walidhihirisha UBINAFSI wa asili wa mtu mweusi.Leo wote hao hawapo wapo mavumbini huko wanaliwa na funza.Hakuna kitu wameondoka nacho zaidi ya suti zao😀😀😀

Uafrika ni laaanaaa.Afrika imelaaaniwaaaaa!!!!
 
Sasa wewe ulitaka sisi tufanye nini, wakati rais wao Kubwa Jinga analia lia tu badala ya kupigana vita.
Kipindi cha Kikwete tulifanya nini?

JK alituma special force iliyoweka rekodi ya Afrika hadi leo(you can google, ''Tanzania Special forces in the Congo'' ).

M23 hawakutoboa, ndani ya wiki moja walishavuka mpaka na kukimbilia kwa boss wao Kigali.

We can again do the same, na safari hii tukishawafurusha, tuingie mkataba na serikali ya DRC majeshi yetu yabakie huko kuwazuia wasirudi tena, huku tukipata percent ya madini yaliyoko Goma.
 
Sasa wewe ulitaka sisi tufanye nini, wakati rais wao Kubwa Jinga analia lia tu badala ya kupigana vita.
Kwenye hali kama hiyo iliyopo hapo DRC; hata ungekuwa ni ww hungekuwa na la kufanya. Ukizingatia huyo Kubwa Jinga alishindwa kuzisoma alama za nyakati anakabiliwa na makundi 120+ yenye silaha dhidi yake. Na kama hilo halitoshi yupo Mkubwa mmoja wa nchi (Bwn. Tolu) na mwenzake mwingine wanatoa misaada ya hali na mali kwa baadhi ya vikundi hivyo.
 
Kubwa Jinga badala ya kujitajirisha, angeorganise jeshi lenye mafunzo idadi ya laki moja tu, PK asingemnyanyasa kama anavyofanywa sasa.
Tatizo waCongo starehe nyingi na hawako serious na kitu chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…