Congo: Wachawi wafanya tamasha la hadhara kuonyesha nguvu walizo nazo za kufanya miujiza. Waazimia kuutumia uchawi kukuza uchumi na maendeleo

Congo: Wachawi wafanya tamasha la hadhara kuonyesha nguvu walizo nazo za kufanya miujiza. Waazimia kuutumia uchawi kukuza uchumi na maendeleo

Uchawi ndio umewafukarisha waafrika wengi kwa kuwaamisha uwongo kwamba unaweza pata maendeleo kupitia ndumba
IMG-20220127-WA0017.jpg
IMG-20220127-WA0014.jpg
IMG-20220127-WA0013.jpg
IMG-20220127-WA0011.jpg
IMG-20220127-WA0007.jpg
IMG-20220127-WA0008.jpg
 
Uchawi ndio umewafukarisha waafrika wengi kwa kuwaamisha uwongo kwamba unaweza pata maendeleo kupitia ndumba
Si kweli, umedanganywa mambo mengi na mkoloni.
  • Huyu mtu mweusi ndiye mgunduzi wa zana za mawe.
  • Ndiye mgunduzi wa moto
  • Ndiye mgunduzi wa zana za muziki
  • Ndiye mgunduzi wa chuma na ndiye mtumiaji wa awali kabisa wa zana za chuma.
Alipokuja mzungu wahunzi wote na uzao wao aliwauawa na wengine kuwakata viganja vya mikono yao.

Walieneza dini yao kwa makali ya upanga.
 
Wachawi nchini Congo [emoji1078] DR wamefanya tamasha la wazi lenye nia ya kuonyesha nguvu na uwezo waluo nao.

Wachawi hao kutoka majimbo 12 walikuwa wamevalia mavazi yenye rangi kali na waliweza kuonyesha shughuli zao mbalimbali ambapo waliiomba serikali ya nchi hiyo iwapatoe leseni ili waweze kuzifanya kazi zao kibiashara na kukuza uchumi.

Mshana Jr, wenzetu wameanza kuutumia uchawi kimaendeleo, sisi tunakwama wapi?

Naunga mkono mapinduzi ya teknolojia, kamwe hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea teknolojoa mtumba.

Uchawi ukitumika vyema utakuwa chachu ya mabadiliko ya kisayansi na teknolojoa.

Ili nchi iendelee, inahitaji teknolojia yake yenyewe tofauti na sass ambapo tuna teknolojia mtumba na elimu wanayosoma vijana wetu imeshindwa kutoa matokeo chanya ndio maana hata waliosoma sayansi wanataka wawe wanasiasa

ningepata clip ninheinjoy
 
Si kweli, umedanganywa mambo mengi na mkoloni.
  • Huyu mtu mweusi ndiye mgunduzi wa zana za mawe.
  • Ndiye mgunduzi wa moto
  • Ndiye mgunduzi wa zana za muziki
  • Ndiye mgunduzi wa chuma na ndiye mtumiaji wa awali kabisa wa zana za chuma.
Alipokuja mzungu wahunzi wote na uzao wao aliwauawa na wengine kuwakata viganja vya mikono yao.

Walieneza dini yao kwa makali ya upanga.

Hio ni historia ya chuki isiyo na ushahidi,Mzungu akufika maeneo yote afrika wengine walikaa maporini Mzungu asifike hata kesho,huo utaalamu umeenda wapi.
Vipi zile nchi ambazo hazikuwahi tawaliwa na Mzungu wao utaalamu wao uliuliwa na nani.
 
Huwa najiuliza Sana jibu sipati. Hivi kwann mwafrika hakutumia uchawi Ili asichukuliwe utumwani au kutawaliwa na mkoloni.
Historia tunaypijua na kuisoma imechakachuliwa,kumbuka hata uchawi pia ni sanaa na haipo afrika tu hata waarabu na wazungu wanao uchawi wao kuna mambo ya kuzidiana na weledi ktk fani!
 
Waliyafanya haya kama njia ya kuwatisha watu kuwajengea uoga au kuuwa fikra zao.
Kama wafanyavyo magaidi kuuwa watu au kufanya ukatili Ili waogopeke.
Kwann sasa tusingewamaliza kwa uchawi hawa weupe,huoni kwamba uchawi ni technology duni Sana kama ilishindwa kumzuia mwafrika asiathiriwe na ukoloni ikiwemo tamaduni za kigeni huoni ni kitu kisicho na faida.
 
Historia tunaypijua na kuisoma imechakachuliwa,kumbuka hata uchawi pia ni sanaa na haipo afrika tu hata waarabu na wazungu wanao uchawi wao kuna mambo ya kuzidiana na weledi ktk fani!
Kwenye nyanda za uharibifu na sio ujenzi.
 
Back
Top Bottom