Copa America 2024 in USA

Copa America 2024 in USA

USA vs Bolivia saa 7 usiku

Uruguay vs Panama saa 10 usiku.

Hawa jamaa naona waliamua kutoangalia pande zingine za dunia.
Hata hii euro, na mechi nyingi za ligi epl,na ndugu zake kuna watu wanazicheki mida mibovu kama hiyo na wengine unakuta mtu saa 2 asubuhi anatakiwa acheki mpira, next worldcup tunaenda kuadhibiwa, mimi hii copa america ntacheki fainali. Na mechi nyingine labda argentina na brazil wakikutana kati hapo nayo ntacheki
 
USA nao wameanza vizuri kwa kupata ushindi wa 2 bila dhidi ya Bolivia

Uruguay nao pia wakishinda 3 kwa moja dhidi ya panama
 
Alfajiri ya kesho tarehe 26/june Argentina atakipiga na Chile kwenye michuano ya Copa America inayoendelea huko Marekani kwenye uwanja wa Metlife huko New Jersey.

Cha kusisimua zaidi kwenye huu mtanange ni kumbu kumbu iliyopo kwenye michuano ya Copa America iliyofanyika mwaka 2016.

Timu hizi mbili zilikutana kwenye fainali ya 2016 ambapo Chile alokuwa ni bingwa mtetezi mnamo tarehe 27/june katika uwanja huu huu wa Metlife na majira yale yale ya saa 10 alfajiri.... ni fainali ambayo iliamuliwa kwa mikwaju ya penalty na Messi akiwa ni moja ya wachezaji walikosa penalty kwa upande wa Argentina na muacha na maumivu makali mno mpaka kumpelekea kustaafu kabla hajatengua maamuzi yake.

Kesho timu hizi zinakutana huku Argentina akiwa ni bingwa mtetezi kama ilivyokuwa kwa Chile kipindi kile.

Ngoja tusibiri nini kitatokea, ila itkuwa ni mechi ya kukata na Mundu.
 
Chile tutampiga kama amelala vile, Argentina all the time ni ya moto, basi hawanaga tu bahati
 
Back
Top Bottom