Corona: Dar es Salaam Wananchi wafanya kweli. Hongereni sana

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na Mabwana hapa ni Dar katika mapambano dhidi ya Corona.

Kwa hakika hawa wameonyesha njia kwani hizi ni jitihada binafsi baada ya kutambua ugonjwa huu upo na biashara ni asubuhi.

Kama vifaranga vya kuku vile kwa hakika hawa wana chakura kivyao kivyao:

Your browser is not able to display this video.


Wa mikoa mingine zingatieni. Mkisubiri kupatiwa maelekezo kwa mwendo uliopo yanaweza yasipatikane:

Your browser is not able to display this video.


Dar wameonyesha njia katika namna ambayo kama wangekuwa kwenye kile kikao na yule mkurugenzi, wasingekubali kuamrishwa kuzivua.

Kongole kwenu wanaume na wanawake wa Dar. Kwa hakika mu wa kupigiwa mfano.

Ninawasilisha.
 
Wafuasi wa CHAMA CHA MAZEZETA wanaendelea kusisitiza HAMNA COVID-19, kunyweni juice ya tangawizi inaua virusi.
Wanasayansi wa kweli wako maabara yanatafuta chanjo na tiba ya kuaminika.

Maprofesa wetu na madaktari wetu wao wako busy na trip za sokoni, jikoni wakisaga chuisi ya pilipili,malimao, tangawizi na vitunguu saumu.

Dona kantreee.
Au nadanganya ndugu zangu?
 
Nilihudhuria mazishi K’Njaro watu wote zaidi ya 1500 walikuwa kwenye barakoa. Ifike mahali tumwondoe dikteta.
 

Mwenye macho haambiwi tazama

Mwenye masikio na asikie
 
Mbona sielewi mnazungumzia Dar ipi?

I'm little bit confused [emoji848]
 
Tangu maambukizi ya Kwanza kabisa Hadi leo hakuna tamko lolote la Serikali kuzuia watu kuchukua hatua za kujilinda na Corona

Tamko lao rasmi hili hapa:

Corona haipo, corona ilikwisha, aaaah aah ipo kidogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…