UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Unataka ujibiwe Mungu yupi wa kweli wakati hata hakujajibiwa kama kweli huyo Mungu yupo? Mie nimeuliza swali sijazuia swali lako watu kulijibu yote mawili yanahitaji majibu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka ujibiwe Mungu yupi wa kweli wakati hata hakujajibiwa kama kweli huyo Mungu yupo? Mie nimeuliza swali sijazuia swali lako watu kulijibu yote mawili yanahitaji majibu.
Maada nyingine mnapokuwa mnajadili kuweni makin sana maana mnaweza kumkosea Muumbaji wa yote . Haya yote yalishatabiriwa katika vitabu vitakatifu na sasa yanatimia hapo ndo utambue kwamba mwisho wa sayari yetu umekaribia kikubwa ni kurekebisha matendo yetu kabla ya kiama . Mungu hapimwi ndugu
Ila matendo ya wachungaji wa leo sio uthibitisho wa uwepo wa Mungu ama laaa! Imani yako ndo itakuponya wala sio wachungaji asanten wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Na mpaka sasa kipindi cha pili na dakika za nyogeza bado dini haijafanikisha kumpata huyo munguScars,
DINI ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, imeumbua dini nyinginna ndio maana kua dini moja kubwa wakaamua kufunga misa zao, wakafuata wale wa MECCA sasa WOKOVU ambao uliletwa na YESU ndio umebaki na ndio mpango wa Mungu kuwakomboa wanadamu na dhaambi zao, hawa watu wa wokovu wanadamu
Ningependa kuongopewa basi ungeniona nikishoboka na hizi diniNa tatizo la watanzania mnapenda sana KUONGOPEWA KULIKO UKWELI.
viongozi wa dini NI watu kama sisi. Hawana mamlaka yoyote au nguvu zozote za kuzuia au kuponesha magonjwa.
Ila leo akitokea kiongozi wa dini anasema anatibu corona.
MTAKIMBILIA HUKO.
sababu mnapenda kudanganywa.
NA WAO WANAJUA. Scars,
Sent using Jamii Forums mobile app
Roho mtakatifu ni hadithi ambayo inazungumzika vitabuni na makanisani tu lakini kiuhalisia haipolaiti kweli wangekua wanaroho mtakatifu anaewapa maono, nadhani wangekua msaada mkubwa sana yanapokuja majanga kama haya maana wangeomba kuoneshwa dawa watu wakapona bt na wao wamejawa na hofu na wanawasubiri madaktari kama waamuz wa hili na si mungu anaewapa maono
Hua wanamaanisha nini Wanavyosema yesu ni dawa, allah ni muweza wa yote anaponya kila gonjwa na hakuna asichoshindwa, mara ombeni nanyi mtapewa?
It's Scars
Ningependa kuongopewa basi ungeniona nikishoboka na hizi dini
Sipendwi kuongopewa na ndo maana nikiuliza maswali ambayo wao walitaka kupotosha kupitia dhana ya imani naambiwa nakufuru
It's Scars
Ukiwaza kidogo lazima uje na fikra ndogo kama hizi, I'm sorry for that
Kama kweli watu wa dini wanaweza kuuondoa huu ugonjwa kwa maombi basi serikali isingepiga marufuku na hata wao walikua na haki ya msingi kikatiba kujijeteta
Serikali imegundua kua maombi si chochote na ndo maana hata wao wenyewe wadini hawajaweka pingamizi
Kama kweli maombi yanafanya kazi sana kwanini tunawaona wanavaa mask huku wakihamasisha na wangine wavae kama kweli maombi yanafanya kazi?
Mfano katika nchi kama ya saudia arabia wale serikali yao yote inafata misingi ya dini lakini kwanini wamekua mstari wa mbele kukataza watu kutoka mataifa mengine wasiende mekka kama kweli power ya maombi inafanya kazi kama tunavyoaminishwa?
It's Scars
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Kwanza hakuna watu waoga kufa kama watu wadini. Lakini ukiwakuta madhabahuni wanavyohubiri utasikia "ukiwa na yesu au roho mtakatifu basi kifo sio tishio kwako"Kumekuwa na mbwembwe nyingi za wachungaji, mitume na manabii kukitokea matatizo yoyote katika jamii wakijinasibu kuyamaliza kwa uwezo waliopewa.
Mara nyingi wao hutunga vitu na kusisitiza wameoneshwa na Mungu na kutamka kuviondoa. Wakijinasibu wakati mwingine hata kusema wanawaponya watu walioathirika na virusi vya UKIMWI.
Naomba niseme kati ya watu wamekuwa wasanii ni hao manabii pamoja na waumini wao wasio na uelewa ambao huacha kufanya kazi na kuwaita baba zao.
Sasa nasema Corona hii hapa, iondosheni Tanzania. Au yatatueni machangamoto ya ndoa zenu huko nyumbani kwenu. Jihadharini na kudanganya watu kujifanya mnaponya kumbe mnatumia wasanii.
Nachukia wanaoigiza
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa watasema kile kipindi walikua kwenye trial version mungu alikua akiwajaribu ila kwa uwezo wa roho mtakatifu jaribu lile walilishindaWakati wa janga la njaa miaka mitatu na nusu watu walipokula mavi ya njiwa vipi hapakuwa na nabii au wakati Israel wametekwa kwenda Babeli hapakuwa na nabii?
Wewe huamini mungu?Baba Swalehe,
Wakati wewe unataka kujua Mungu yupi ni wa wakweli kuna wengine wanataka kujua kama huyo Mungu kweli yupo?
Wewe unaweza kujibu hilo swali kuwa kweli Mungu yupo?
Scars,
Kwa maana nyengine ni kwamba kumbe tunaweza kuaminishwa jambo la kisayansi na kumbe jambo hilo lisiwe kweli.
Kwenye sayansi tunaambiwa kunafanyika tafiti na sio imani,ila mbona kuna utata wengine wanasema kuna virusi vya ukimwi na wengine wanasema hakuna virusi vya ukimwi? Na wote ni wanasayansi wenye kutofautiana hivyo na wana ushahidi wao wa kisayansi.
Kama mambo ya imani ni magumu utajuaje kua imani yako sahihi kuliko ya mwingine?Mambo ya imani ni magumu.
Usitegemee mara zote uombe na Mungu akujibu on the sport.
Hata Mfalme Daudi kuna wakati alikosea Mungu akawapiga tauni ya siku tatu taifa lilikaribia kuisha.
Hata wana wa Israeli walikuwa wakimkosea Mungu anawapiga au na vita au na maradhi hadi watubu.
Hao watumishi wa leo nao ni watu kama wewe wengi wao wana makandokando kibao. Mungu anawatazama kwanza watubu warejee kwake.
Hata hivyo tuamini tu kuwa wapo wachache wanaoomba na Mungu anasikia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upotoshaji kijana
Imani ingekua inaponya kama wewe unavyotuaminisha hapa basi tusingeona vatican na mekka wakipiga marufuku watu kwenda kuhiji kwao kwa kuogopa corona wakati wakijua kabisa kua ukiwa na imani unapona
It's Scars