Mleta mada ngoja nikufungue macho kidogo tu.
MUNGU maana yake ni NGUVU (POWER)
NGUVU (POWER) unaweza ukaendelea kuifafanua katika pande mbili
1.NGUVU Hasi (NEGATIVE POWER)
2.NGUVU Chanya (POSITIVE POWER)
zote mbili zinatengeneza jina MUNGU(POWER)
Nguvu hizi zote ni za manufaa kwa mwanadamu.
Zinashuka kutokana na matendo na Imani yako.
Kwanza ulitakiwa ufafaune hiyo nguvu chanya ina sifa za uwezo, wote, ujuzi wote na upendo wote au ni kinyume chake?
Kama hiyo nguvu chanya ni mungu basi pia ulitakiwa kufafanua hiyo nguvu hasi imetokana na nini, yaani nini chanzo cha hiyo nguvu hasi mpaka ikawepo?
Kama nguvu hasi (shetani) imeumbwa na mungu wako (nguvu chanya) mwenye utimilifu wa hizo sifa nilizozitaja hapo juu inatakiwa uthibitishe ni kivipi mungu mwenye uwezo wote aumbe kiumbe chenye uovu?
NGUVU hizi ni jumuiko la nguvu zote ulizowai kujua au kusikia Mfano,nguvu ya kusikia,nguvu ya kunena,nguvu ya uumbaji,nguvu ya kufufua,nguvu ya kifo na nyingine nyingi sana.
Imani na matendo yako yakiwa mema,huitaji hata kuubiriwa NGUVU CHANYA itakushukia , hutaona mateso yoyote kwa sababu ya kutawaliwa na Positive Power ambayo sehemu yake ni Amani,Afya na Mafanikio.
Imani ni nini?
Pili matendo mema unayapimaje?
Mfano mdogo waislamu kwao kuoa wake wanne kwao ni tendo jema, lakini ukija kwa wakristo jambo hilo sio jema.
Sasa ikatokea mtu amefanya jambo hilo utatumia dhana gani kuhalalisha au kubatilisha kua ni jema au sio jema?
Upi mzani sahihi kupima jema au lisilo jema?
Imani na Matendo yako yakiwa ni ya giza,huitaji tena kuubiriwa,NGUVU hasi itashuka tu na matokeo yake ndio yatakufungua ufahamu kwamba uligusa kwa imani na matendo sehemu inayovuta nguvu hasi.
Skiliza wewe
Hayo matendo ya giza kimsingi wa dini yenu siwezi nikayafanya bila kushawishiwa na huyo shetani. Infact ni kua kila jambo baya linapotendeka basi kwa namna yeyote ile shetani lazima ahusike.
Vile vile mungu akitaka mimi nisifanye hayo mambo ya giza anaweza kwasababu uwezo wote anao na sababu yakufanya hiyo anayo kwasababu yeye ni mwenye upendo wote.
Lakini hata hivyo ukiangalia hiyo kazi ya shetani kama ni kosa ambalo linamchukiza mungu basi tutahitimisha kwa kusema mungu ni mnafki. Kivipi? Kwasababu kabla hajamuumba shetani, huyu mungu kwa uwezo na ujuzi wake wote aliweza kujua impact itakayofanywa na huyi shetani siku za usoni. Inamaana mpaka anafikia hatua anamkamilisha kumuumba shetani, mungu alikwisha jua shetani atachoenda kukifanya.
Sasa huyu mungu kujilalamisha kwamba hapendi matendo anayoyafanya shetani huoni kwamba kunamfanya mungu aonekane mnafiki?
Haya tuseme kwamba ni kweli anachukizwa na uovu wa shetani, sasa anachukua uamuzi upi ku-fix hilo tatizo? Mbona uwezo wote anao kulikua na haja ya yeye hata ku-delay?
Kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote anaishia kunung'unika tu pasipo kufanya chochote kivipi ategemee sisi tumuepuke shetani?
Kwa kutafakari Nguvu zilizoundwa na Mwanadamu,Nguvu ya umeme imegawanyika hivyohivyo,kutoka na jinsi utakavyoitumia.Ukiutumia umeme kwa kufuata masharti na vyombo husika utafurahia nguvu chanya ya umeme,ukienda kwenye nyaya na kutaka kuutumia bila vifaa maalumu utafurahia nguvu chanya.
Nguvu ya umeme uliotengenezwa na binadamu bado sio efficiently kwasababu malengo yao hayaendi kama wanavyotaka kwasababu hawana uwezo wote.
Aliyetengeneza umeme alikua hana uwezo wote wa kuufanya umeme usiweze kudhuru watu au miundombinu ya watu.
Huyu mungu ambaye anasifa ya "neno" yani akitamkacho ndicho kinachoenda kufanyika alikua na uwezo wa kusema "uovu usiwepo" na ikawa kweli uovu ukatokomea. Kwasababu kila kitu kipo chini yake
Corona na Magonjwa mengine ni matokeo ya imani na matendo hasi ya mwanadamu.
Na mataokeo hasi yamesababishwa na mungu kwa kosa alilolifanya kumuumba shetani ambaye anatushinikiza sisi kufanya uovu.
Utagundua baada ya nguvu hii kushuka,Matendo hasi yamezimwa kwa muda ingawa ni kwa kutumia sheria lakini pia watu wamejua kuna MUNGU.Juudi za kipindi kifupi za kuzima uhasi,zimeanza kuvuta Nguvu Chanya,amani na utulivu baadhi ya miji imeanza kurejea.
Hakuna muda sahihi wa mungu kudhihirisha ukuu wake kama kipindi hiki cha matatizo.
Hiki kipindi ndio kipindi ambacho mungu angeibuka warrior, lakini imekua tofauti yani kipindi hiki tumegundua ni namna gani hizi dini zimekua zikituongopea kuhusu mungu
Kwanini umtolee sadaka halafu kwenye matatizo kama haya akuache?
Mekka na vatican wanapiga hela za kuhiji lakini kipindi hiki wote wamefunga milango hawawataki muende.
Shetani hajawai kuumba nguvu yoyote japo yeye anatafasiriwa kama ndio Nguvu Hasi.Shetani ni matokeo ya nguvu ya uumbaji kama ilivyo kwa mwanadamu.Tofauti yake ni kwamba ndani yake amewekewa nguvu fulani zilizo nje ya uwezo wa mwanadamu na hajapewa mwili kama mwanadamu kabaki katika roho kitu kinachompa uwezo mkubwa wa kutumia nguvu ndogo iliyowekwa ndani yake ya ushawishi,na kujigeuza na kujigawanya.
Kwanini ubaya wa shetani alaimiwe shetani na sio mungu aliyemuumba shetani huku akijua kua atakuja kufanya ubaya?
Shetani yeye anatafuta kujiumba ili aitwe NGUVU lakini ameshindwa.Kwa kutumia ushawishi wake ambao ndio furaha yake,ameweza kushawishi wanadamu kugusa kwa imani na matendo sehemu zinazovuta NGUVU hasi.Kumbuka ukishawishiwa kushika nyaya za umeme utavuta kifo,fuata maelekezo utafurahia umeme.
Shetani kushindwa kufanya matakwa yake ni sawa kwasababu aliyemuumba hakumpa uwezo wote.
Sasa mungu muweza wa yote lakini bado ulimwengu umezagaa uovu inakuaje anashindwa kudhibiti haya mabaya?
Kazi ya wachungaji na Dini ni kukutadharisha usiguse nyaya za umeme .
Ndio maana wanatuhamasisha kuvaa mask
Nguvu ya kifo ikishuka kwa majina tofauti tofauti kama Corona,tuangalie imani na matendo yetu kama yapo sawa.Uzuri nguvu hasi ikishuka kama hii ya Corona inaweza kukusanya na wale ambao matendo yao na imani yao ni nzuri ila kwa sababu ulimwengu huu si makao yetu ilo halisumbui kwa sababu Nguvu ya ufufuko itafanya kazi yake ambayo itaelekeza ni nani wa kufufuka na kuendelea kuwa na nguvu ya Uzima na ninani wa kufa milele.
Watu wote wangejua kwa hakika kua huu ulimwengu sio makao yetu. Na kuna maisha baada ya hapa ambayo ni mazuri kuliko haya ya hapa, basi tusingeona maka na vatican wakipiga marufuku watu kwenda kwao kwa hofu ya kufa kwa corona
Hivyo ni kukumbushe mleta mada upo jinsi ulivyo kwa sababu kuna nguvu imekufunika,angalia imani yako na matendo yako yasivute Nguvu hasi, hakuna Dini wala mbadala wa Dini utakaokuokoa bali imani yako na matendo yako katika njia iliyofafanuliwa na vitabu vitakatifu.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Vitabu vitakatifu wewe unajuaje kua vimesema ukweli?
It's Scars