Mleta mada ngoja nikufungue macho kidogo tu.
MUNGU maana yake ni NGUVU (POWER)
NGUVU (POWER) unaweza ukaendelea kuifafanua katika pande mbili
1.NGUVU Hasi (NEGATIVE POWER)
2.NGUVU Chanya (POSITIVE POWER)
zote mbili zinatengeneza jina MUNGU(POWER)
Nguvu hizi zote ni za manufaa kwa mwanadamu.
Zinashuka kutokana na matendo na Imani yako.
NGUVU hizi ni jumuiko la nguvu zote ulizowai kujua au kusikia Mfano,nguvu ya kusikia,nguvu ya kunena,nguvu ya uumbaji,nguvu ya kufufua,nguvu ya kifo na nyingine nyingi sana.
Imani na matendo yako yakiwa mema,huitaji hata kuubiriwa NGUVU CHANYA itakushukia , hutaona mateso yoyote kwa sababu ya kutawaliwa na Positive Power ambayo sehemu yake ni Amani,Afya na Mafanikio.
Imani na Matendo yako yakiwa ni ya giza,huitaji tena kuubiriwa,NGUVU hasi itashuka tu na matokeo yake ndio yatakufungua ufahamu kwamba uligusa kwa imani na matendo sehemu inayovuta nguvu hasi.
Kwa kutafakari Nguvu zilizoundwa na Mwanadamu,Nguvu ya umeme imegawanyika hivyohivyo,kutoka na jinsi utakavyoitumia.Ukiutumia umeme kwa kufuata masharti na vyombo husika utafurahia nguvu chanya ya umeme,ukienda kwenye nyaya na kutaka kuutumia bila vifaa maalumu utafurahia nguvu chanya.
Corona na Magonjwa mengine ni matokeo ya imani na matendo hasi ya mwanadamu.
Utagundua baada ya nguvu hii kushuka,Matendo hasi yamezimwa kwa muda ingawa ni kwa kutumia sheria lakini pia watu wamejua kuna MUNGU.Juudi za kipindi kifupi za kuzima uhasi,zimeanza kuvuta Nguvu Chanya,amani na utulivu baadhi ya miji imeanza kurejea.
Shetani hajawai kuumba nguvu yoyote japo yeye anatafasiriwa kama ndio Nguvu Hasi.Shetani ni matokeo ya nguvu ya uumbaji kama ilivyo kwa mwanadamu.Tofauti yake ni kwamba ndani yake amewekewa nguvu fulani zilizo nje ya uwezo wa mwanadamu na hajapewa mwili kama mwanadamu kabaki katika roho kitu kinachompa uwezo mkubwa wa kutumia nguvu ndogo iliyowekwa ndani yake ya ushawishi,na kujigeuza na kujigawanya.
Shetani yeye anatafuta kujiumba ili aitwe NGUVU lakini ameshindwa.Kwa kutumia ushawishi wake ambao ndio furaha yake,ameweza kushawishi wanadamu kugusa kwa imani na matendo sehemu zinazovuta NGUVU hasi.Kumbuka ukishawishiwa kushika nyaya za umeme utavuta kifo,fuata maelekezo utafurahia umeme.
Kazi ya wachungaji na Dini ni kukutadharisha usiguse nyaya za umeme .
Nguvu ya kifo ikishuka kwa majina tofauti tofauti kama Corona,tuangalie imani na matendo yetu kama yapo sawa.Uzuri nguvu hasi ikishuka kama hii ya Corona inaweza kukusanya na wale ambao matendo yao na imani yao ni nzuri ila kwa sababu ulimwengu huu si makao yetu ilo halisumbui kwa sababu Nguvu ya ufufuko itafanya kazi yake ambayo itaelekeza ni nani wa kufufuka na kuendelea kuwa na nguvu ya Uzima na ninani wa kufa milele.
Hivyo ni kukumbushe mleta mada upo jinsi ulivyo kwa sababu kuna nguvu imekufunika,angalia imani yako na matendo yako yasivute Nguvu hasi, hakuna Dini wala mbadala wa Dini utakaokuokoa bali imani yako na matendo yako katika njia iliyofafanuliwa na vitabu vitakatifu.
Sent using
Jamii Forums mobile app