Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Kila kitu kina utaratibu wake,Daktari hawezi kutibu bila kuwa na vitendea kazi,kuwa na mtu wa maabara,na mtu wa maabara bila vitendea kazi,hapati vipimo sahihi.Na yapo maradhi, ambayo wanasayansi,hawayajui,hawana dawa ya kuyatibu.Hapo ujuwe ipo nguvu nje ya uwezo wa wanasayansi,na si nyingine,ila ni Mungu,muweza wa yote.
Kwa hiyo dini,pia ina taratibu zake.Uislamu unahimiza kujitibu,sio kuomba dua tu peke yake.Na vile vile kujikinga kwa ugonjwa ni amri katika uislamu.Kuweka karantini pia ni amri katika uislamu. kwa
Hua wanamaanisha nini Wanavyosema yesu ni dawa, allah ni muweza wa yote anaponya kila gonjwa na hakuna asichoshindwa, mara ombeni nanyi mtapewa?

It's Scars

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwepo kwa utata katika sayansi ambayo inafanywa na watu ambao hawana uwezo wote wala ujuzi wote, wala sio jambo la kustaajabisha.

Tutasema tu kua probably kwasababu ya udhaifu wao ndio maana hayo yanatokea na wao hawakua na namna ya kuweza kuepuka kufanya hivyo kwasababu hawakua na uwezo wote wala ujuzi wote wa kufanya bila kukosea.

Sasa kwa mungu mwenye sifa hizo za ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote huoni mungu huyo kuumba huu ulimwengu ambao umejaa magonjwa na mabalaa ya kila rangi bado ni utata?

It's Scars
Kwani uliambiwa huu ulimwengu una mabalaa na magonjwa kwa sababu Mungu kasema kashindwa kuyaondoa au kwamba kashindwa kuumba ulimwengu ambako hakuna magonjwa?

Point ni kwamba hata kwenye masuala ya sayansi kuna waumini,kwamba tunaamini tunayoambiwa na wanasayansi kuhusu masuala ya kisayansi na wakati mwengine hutokea tuliyoaminishwa kuwa si ya kweli pamoja na sifa za sayansi tunazoipa.
 
BS
Janga mulitafute wenyewe,halafu,lawama mpeleke kwa Mungu.
Mugu alishaleta maelekezo ya jinsi ya kuishi,kupitia vitabu,Mitume,Manabii.Vitabu vyake,vina maelekezo yote ya maisha,kipi ufanye,na kipi uwache.Kipi ule na kipi usile.Mnakula popo,nyoka,majongoo,konokono nk.Halafu mkiumwa mwalamika kwa aliyewapa tahadhari.
Ni sawa na kumlaumu,aliyetengeneza gari au machine,wakati ameshakupa maelekezo kupitia vitabu na mafundi,jinsi kuitunza machine,kwa kuifanyia service,kila ukifika mda fulani,wewe huifanyii service,halafu wamlaumu mtengeneza magari.Au gari la petrol,unakwenda weka diesel,halafu unamlamu aliyetengeneza gari,likikataa kufanyakazi.






Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu kina utaratibu wake,Daktari hawezi kutibu bila kuwa na vitendea kazi,kuwa na mtu wa maabara,na mtu wa maabara bila vitendea kazi,hapati vipimo sahihi.Na yapo maradhi, ambayo wanasayansi,hawayajui,hawana dawa ya kuyatibu.Hapo ujuwe ipo nguvu nje ya uwezo wa wanasayansi,na si nyingine,ila ni Mungu,muweza wa yote.
Kwa hiyo dini,pia ina taratibu zake.Uislamu unahimiza kujitibu,sio kuomba dua tu peke yake.Na vile vile kujikinga kwa ugonjwa ni amri katika uislamu.Kuweka karantini pia ni amri katika uislamu. kwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanasayansi kukosa majibu katika tafiti zao za kitabibu hakuoneshi kwamba kuna nguvu yenye uwezo wote na upendo wote ipo.

Kuwezekanika tu kuwepo kwa hayo maradhi ambayo wanasayansi wamekua wakikesha kuyatafutia tiba kunathibitisha hakuna nguvu yenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote yenye kutunusuru na haya maradhi

Unakubali kabisa kua kuna magonjwa ambayo hayana chanjo wala tiba halafu at the same time unasema kuna nguvu ipo yenye uwezo wote, hivi haujishtukii tu kua unajichanganya mwenyewe?



It's Scars
 
Kwani uliambiwa huu ulimwengu una mabalaa na magonjwa kwa sababu Mungu kasema kashindwa kuyaondoa au kwamba kashindwa kuumba ulimwengu ambako hakuna magonjwa?
Kwanini kuwe na haja ya kuambiwa ilihali hali halisi inajionesha?

Dhana ya "mungu kasema kashindwa kuyaondoa" kwangu bado inatatiza kwasababu nitakudai uthibitisho wa kauli hiyo

katika yale magonjwa ambayo yametafutiwa suluhu na ambayo bado hayajatafutiwa suluhu, unaweza kuthibitisha mungu kabla ya ya chanjo kupatikana mungu alisema kua atayaondoa au kutoyaondoa hayo magonjwa?

Kuna nukuu yeyote ambayo unaweza kunipa ikionesha mungu amesema anaweza kuuondoa ukimwi ambao unazaidi ya mika 30 hapa duniani?



Point ni kwamba hata kwenye masuala ya sayansi kuna waumini,kwamba tunaamini tunayoambiwa na wanasayansi kuhusu masuala ya kisayansi na wakati mwengine hutokea tuliyoaminishwa kuwa si ya kweli pamoja na sifa za sayansi tunazoipa.

Point nyingine ni kwamba uwepo wa waumini katika sayansi haimaanishi kua wanatumia dini katika kutekeleza majukumu yao ya kisayansi.

Ingekua kweli maombi ya watu wadini hufanya kazi kwa namna ambavyo wamekua wakihubiri madhabahuni. Basi hata hao wanasayansi wasinge thubutu kuhangaika kutafuta chanjo ya magonjwa. Kwasababu mambo yangekua rahisi tu kama ukiomba dawa inapatikana kwa muujiza wa mungu



It's Scars
 
Mleta mada ngoja nikufungue macho kidogo tu.
MUNGU maana yake ni NGUVU (POWER)
NGUVU (POWER) unaweza ukaendelea kuifafanua katika pande mbili
1.NGUVU Hasi (NEGATIVE POWER)
2.NGUVU Chanya (POSITIVE POWER)
zote mbili zinatengeneza jina MUNGU(POWER)
Nguvu hizi zote ni za manufaa kwa mwanadamu.
Zinashuka kutokana na matendo na Imani yako.
NGUVU hizi ni jumuiko la nguvu zote ulizowai kujua au kusikia Mfano,nguvu ya kusikia,nguvu ya kunena,nguvu ya uumbaji,nguvu ya kufufua,nguvu ya kifo na nyingine nyingi sana.

Imani na matendo yako yakiwa mema,huitaji hata kuubiriwa NGUVU CHANYA itakushukia , hutaona mateso yoyote kwa sababu ya kutawaliwa na Positive Power ambayo sehemu yake ni Amani,Afya na Mafanikio.

Imani na Matendo yako yakiwa ni ya giza,huitaji tena kuubiriwa,NGUVU hasi itashuka tu na matokeo yake ndio yatakufungua ufahamu kwamba uligusa kwa imani na matendo sehemu inayovuta nguvu hasi.

Kwa kutafakari Nguvu zilizoundwa na Mwanadamu,Nguvu ya umeme imegawanyika hivyohivyo,kutoka na jinsi utakavyoitumia.Ukiutumia umeme kwa kufuata masharti na vyombo husika utafurahia nguvu chanya ya umeme,ukienda kwenye nyaya na kutaka kuutumia bila vifaa maalumu utafurahia nguvu chanya.

Corona na Magonjwa mengine ni matokeo ya imani na matendo hasi ya mwanadamu.

Utagundua baada ya nguvu hii kushuka,Matendo hasi yamezimwa kwa muda ingawa ni kwa kutumia sheria lakini pia watu wamejua kuna MUNGU.Juudi za kipindi kifupi za kuzima uhasi,zimeanza kuvuta Nguvu Chanya,amani na utulivu baadhi ya miji imeanza kurejea.

Shetani hajawai kuumba nguvu yoyote japo yeye anatafasiriwa kama ndio Nguvu Hasi.Shetani ni matokeo ya nguvu ya uumbaji kama ilivyo kwa mwanadamu.Tofauti yake ni kwamba ndani yake amewekewa nguvu fulani zilizo nje ya uwezo wa mwanadamu na hajapewa mwili kama mwanadamu kabaki katika roho kitu kinachompa uwezo mkubwa wa kutumia nguvu ndogo iliyowekwa ndani yake ya ushawishi,na kujigeuza na kujigawanya.

Shetani yeye anatafuta kujiumba ili aitwe NGUVU lakini ameshindwa.Kwa kutumia ushawishi wake ambao ndio furaha yake,ameweza kushawishi wanadamu kugusa kwa imani na matendo sehemu zinazovuta NGUVU hasi.Kumbuka ukishawishiwa kushika nyaya za umeme utavuta kifo,fuata maelekezo utafurahia umeme.

Kazi ya wachungaji na Dini ni kukutadharisha usiguse nyaya za umeme .

Nguvu ya kifo ikishuka kwa majina tofauti tofauti kama Corona,tuangalie imani na matendo yetu kama yapo sawa.Uzuri nguvu hasi ikishuka kama hii ya Corona inaweza kukusanya na wale ambao matendo yao na imani yao ni nzuri ila kwa sababu ulimwengu huu si makao yetu ilo halisumbui kwa sababu Nguvu ya ufufuko itafanya kazi yake ambayo itaelekeza ni nani wa kufufuka na kuendelea kuwa na nguvu ya Uzima na ninani wa kufa milele.

Hivyo ni kukumbushe mleta mada upo jinsi ulivyo kwa sababu kuna nguvu imekufunika,angalia imani yako na matendo yako yasivute Nguvu hasi, hakuna Dini wala mbadala wa Dini utakaokuokoa bali imani yako na matendo yako katika njia iliyofafanuliwa na vitabu vitakatifu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mpaka sasa kipindi cha pili na dakika za nyogeza bado dini haijafanikisha kumpata huyo mungu

It's Scars
Mungu haonekani kwa macho, "nyie wapaganinndio mnasema mara kamtokea fatima, mara yupo chanika, mara kamtokea sijui babu mtakatifu nani? yupo na alikuwepo na ataendelea kuwako
 
Back
Top Bottom