Corona imekuja kuumbua uongo wa dini


Acha upotoshaji kijana

Imani ingekua inaponya kama wewe unavyotuaminisha hapa basi tusingeona vatican na mekka wakipiga marufuku watu kwenda kuhiji kwao kwa kuogopa corona wakati wakijua kabisa kua ukiwa na imani unapona

It's Scars
 
Na mpaka sasa kipindi cha pili na dakika za nyogeza bado dini haijafanikisha kumpata huyo mungu

It's Scars
 
Ningependa kuongopewa basi ungeniona nikishoboka na hizi dini

Sipendwi kuongopewa na ndo maana nikiuliza maswali ambayo wao walitaka kupotosha kupitia dhana ya imani naambiwa nakufuru

It's Scars
 
Ninachotambua nikuwa MUNGU yupo.... (Majaribu haya budi kuja)
Binadamu anamkumbuka Mola wake wakati wa taabu, tena anataka ajibu maombi yake haraka sana kiasi cha mate aliyotema chini yasikauke.

Asante Mungu
 
Roho mtakatifu ni hadithi ambayo inazungumzika vitabuni na makanisani tu lakini kiuhalisia haipo

It's Scars
 
Na ndo maana viongozi wa dini wamekaa kimya.
SABABU WAMEJUA KUWA HAKUNA MAOMBI YATAKAYO TIBU CORONA.
sasa NINYI MNALAZIMISHA MTAPELIWE.
akina gwajima wanawacheki tu.
Wanatafuta njia ZA KUJA KUWATAPELI.
Maana HAMSIKIII.
Ningependa kuongopewa basi ungeniona nikishoboka na hizi dini

Sipendwi kuongopewa na ndo maana nikiuliza maswali ambayo wao walitaka kupotosha kupitia dhana ya imani naambiwa nakufuru

It's Scars

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Waislam unawaone bure kabisa, wao hawana mambo ya kusema wanaponesha wagonjwa kwa miujiza.

Hii ishu tuwaulize moja kwa moja wakristo ambao kila siku tunaona wanaponesha wagonjwa,viwete wanatembea, wenye kansa wanapona...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hautakiwi kuleta hoja kujadili kitu usichokiamini kama huamini katika dini ni bora kukaa kimya.
 

Mkuu Scars nimeziona hoja zako. Naomba mkuu ujue kwamba huu ugonjwa unaweza kuwa ni kidole cha Mungu kuunyeyekeza ulimwengu na ni vyema ukajua kwamba kupitia ugonjwa huu wengi wanaweza kumrudia Mungu. Mkuu Scars mbali na ulichoandika hapo juu, nakuhakikishia hata wewe ukiona ndugu kadhaa wa familia yako wameondoka kwa huu ugonjwa utaanza kuwaza kumtafuta Mungu. Sasa hili la watu waliotarajiwa kutuongoza kuelekea kutumia Imani kuonyesha kutokuwa na Imani wao wenyewe ni udhaifu wa kibinadamu tu.

Hili la kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya kuhusu Corona na haliondoi lile hitaji ya watu kuendelea kumtumaini Mungu kwa Maombi.

Ahsante
 
Kwanza hakuna watu waoga kufa kama watu wadini. Lakini ukiwakuta madhabahuni wanavyohubiri utasikia "ukiwa na yesu au roho mtakatifu basi kifo sio tishio kwako"


Kwanini wanaogopa kufa wakati sisi ndugu zetu wakifa mapadre na masheikh wakati wa ibada za maziko wamekua wakisema "sisi tulimpenda ila mungu alimpenda zaidi" na kuna muda wanaenda mbali kabisa na kusema kua kifo ni mpango wa mungu

Kama kweli mtu akifa mungu anakua amempenda zaidi kwanini wao wajikinge na mask au kukataza watu wasiende kuhiji kwa kuogopa kufa kwa maambukizi ya korona?



It's Scars
 
Wakati wa janga la njaa miaka mitatu na nusu watu walipokula mavi ya njiwa vipi hapakuwa na nabii au wakati Israel wametekwa kwenda Babeli hapakuwa na nabii?
Hahahaa watasema kile kipindi walikua kwenye trial version mungu alikua akiwajaribu ila kwa uwezo wa roho mtakatifu jaribu lile walilishinda

It's Scars
 

Kuwepo kwa utata katika sayansi ambayo inafanywa na watu ambao hawana uwezo wote wala ujuzi wote, wala sio jambo la kustaajabisha.

Tutasema tu kua probably kwasababu ya udhaifu wao ndio maana hayo yanatokea na wao hawakua na namna ya kuweza kuepuka kufanya hivyo kwasababu hawakua na uwezo wote wala ujuzi wote wa kufanya bila kukosea.

Sasa kwa mungu mwenye sifa hizo za ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote huoni mungu huyo kuumba huu ulimwengu ambao umejaa magonjwa na mabalaa ya kila rangi bado ni utata?

It's Scars
 
Kama mambo ya imani ni magumu utajuaje kua imani yako sahihi kuliko ya mwingine?

It's Scars
 
Imani ina taratibu zake,sio kama unavyotaka wewe.Hata sayansi ina taratibu zake,ili iwe ni sayansi,sivyo unavyotaka wewe.Kwa mfano,unataka kufanya jaribio lolote la sayansi,ni lazima uende maabara, maalumu iliyojemgwa kwa kazi hiyo,huwezi kwenda sokoni ukafanya jaribio la sayansi ukapata majibu sahihi.Vile vile ukitaka kupiga picha ya X Ray,huwezi kupiga nje kwenye mwanga wa jua,kuna chumba maalumu,kilichojengwa kwa ajili ya X Ray's.Nk.
Kwa hiyo imani ina taratibu zake,na sayansi ina taratibu zake.
Acha upotoshaji kijana

Imani ingekua inaponya kama wewe unavyotuaminisha hapa basi tusingeona vatican na mekka wakipiga marufuku watu kwenda kuhiji kwao kwa kuogopa corona wakati wakijua kabisa kua ukiwa na imani unapona

It's Scars

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…