Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Wewe jamaa bhana!!?
Unavyo mchukulia MUNGU ndivyo naye atakavyo kuchukulia ukimchukulia kwa uzito na yeye atakuchukulia kwa uzito ukimchukulia kikawaida basi ivyoivyo atakuchukulia wewe

Nauhakika na hili
Mungu naye kumbe ana double standards kama sisi?

Ye mbona kwenye vitabu amesema wivu ni dhambi halafu yeye huyo huyo anasema usiabudu miungu wengine maana yeye ni mungu mwenye wivu?

Leo hii mimi nikiwa na wivu na mungu naye awe na wivu hiyo si inamaana kama dhambi wote tunayo na kama sio dhambi basi wote hatuna. Sasa kwanini mimi niwe nayo halafu yeye asiwe nayo wakati wote tuna wivu?
 
Dini imekataza kula pop, bundi na wanyama sasa wachina wakala na haya ndo matokeo yake
Dini yako ndo imekataza ya kwake huenda imeruhusu, sasa unataka watu wote waishi kwa kufata sheria za dini yako? We mbona hauli pop kwasababu dini zingine zimeruhusu

Na nyie wadigo ambao hamli popo imekuaje imewapata?
 
Mungu naye kumbe ana double standards kama sisi?

Ye mbona kwenye vitabu amesema wivu ni dhambi halafu yeye huyo huyo anasema usiabudu miungu wengine maana yeye ni mungu mwenye wivu?

Leo hii mimi nikiwa na wivu na mungu naye awe na wivu hiyo si inamaana kama dhambi wote tunayo na kama sio dhambi basi wote hatuna. Sasa kwanini mimi niwe nayo halafu yeye asiwe nayo wakati wote tuna wivu?
Kwa upande wako your right
 
2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
8 Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu.
9 Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.
10 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;
11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
15 Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani. Neema na iwe pamoja nanyi nyote.

'Tito 3:2-15'


Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
'Waebrania 11:6-8

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

'Yuda 1:3-4'


Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
'Waebrania 11:6-8

Sent using Jamii Forums mobile app
Hso waebrania ulio wanukuu unahakika gani kama wamesema ukweli?

Unafikiri mapadre huko vatican hawajaona kua kuna nukuu za waebrania mpaka wameamua kupiga marufuku msiende?
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
=============================

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Wewe jamaa bhana
Kama hii ndio hoja yako basi unaweza kusema kila jambo limekuja kuumbua uongo wa dini.

Kwa nini hukusema kutafuta riziki kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kukaandani na kuomba dua halafu chakula kikamshukia.
Au kwanini hukusema kusoma kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kwenda msikitini kuomba dua kisha tayari akawa professor. Na hivyo hivyo mambo mengine.

We jamaa mwenyezimungu aliweka nidhamu/kanuni katika ulimwengu na mambo hayaendi vile unavyo fikiri wewe.
 
Dunia yote imesalander! Hakuna mwenye nguvu, hakuna mwenye utaalamu, hakuna tajiri, hakuna teknolojia, hakuna silaha kali, hakuna usalama wa taifa, hakuna hakuna hakuna chochote. Kila nchi inalilia hali yake. Kila nchi inafunga mipaka yake, haijulikani tena nani anamfungia nani. Hakuna nchi inayohurumia nchi nyengine, kila moja inapambana kivyake... yote yamesababishwa na kidudu kidogo-virus.. wala hakionekani kwa macho! Unahitaji nini kukubali kuwa Mungu yupo?

Ambaye akitaka lake hakuna nguvu yeyote inayoweza kulizuia?
Ameleta corona akitaka ataiondoa hakutaka ataiacha iendelee kutia adabu watu. Hapangiwi ampe nani na nani ni maamuzi yake tu!!! Watu wa dini yeye ndo anawajua zaidi kuliko wewe kama ni wa kweli au waongo!

Sisi tunaomuamini uwepo wake na nguvu zake tunamuomba atunusuru na hili lkn hatuna haki ya kumlazimisha. Tunaomba, anaweza akatukubalia au akatukatalia! Hakuna mwenye guarantee ya maamuzi ya Mungu!
 
Back
Top Bottom