Haya sasa ndiyo madhara ya kuchanganya DINI, SIASA, UTAPELI, SAYANSI, HALF-KNOWLDGE na PREJUDICE.
Katika ukristu, sote tunajua kuna matepeli wengi, wanaotumia jina la Yesu kuishi mjini, kuwafanya wengine mazoba ili wao wapige dili, na hawa wameuumiza ukristu kwa sehem kubwa. Wanapaswa kulaumiwa sababu hawamuhubiri Yesu wa msalaba ila Yesu wa Harusini kana, wao ukristu ni kupata utajari, kupona magonjwa yote, kuishi kama uko peponi ilihali uko duniani.
Jibu rahisi tu ni kwamba hata Yesu mwenyewe, hakuponya wagonjwa wote aliokutana nao, aliponya wale tu ambao uponyaji wao unahusika moja kwa moja na lengo lake kuja duniani, ambalo ni kuokoa roho (na mwili akitaka Yesu, ila sio kwa kuamrishwa na mwanadamu)
Lengo la Yesu na Ukristu, sio kumfanya mwanadamu astarehe duniani, bali mwanadamu atambue maisha ya duniani kama matayarisho ya maisha ya umilele, hili ndilo lililomleta Yesu duniani, na ndiyo kwa mfano kanisa katoliki linafundisha.
Unadhani kwa nini wamisionari walikuja na dini mkono wa kulia na shule/hospitali mkono wa kushoto? je kuna wamisonari wa kikatoliki walikuja na kusema acheni hospitali njooni tuwaombee mpone?
Mungu anasikia kilio chetu na anaweza kutuponya kwa muujiza Corona endapo akitaka, sisi tunafunga na kusali kumuonesha haja na hitaji letu, japo analijua lakini ameshasema OMBENI NANYI MTAPEWA, BISHENI NANYI MTAFUNGULIWA....hakusema simama mlangoni, nitafungua kwa kuwa ninajua unataka kuingia!!!!
Tutumie utashi wetu wa kibinadamu, ambao ni zawadi ya Mungu, kukwepa corona, na tumuombe Mungu atuepushe na Corona kwa namna zile ambazo ziko nje ya uwezo wetu kama wanadamu, ila tusatake kumfanya Mungu shemeji yetu kuwa aje sasa aponeshe Corona ndo awe Mungu kweli.
Nawaambia hivi, hata Mungu akishuka leo hii akaponesha Corona dunia nzima, hamtamwamini, sababu Corona sio kipimo cha uwezo na mamlaka ya Mungu, Mungu hapimwi kwa uwezo wake wa kuponya Corona