Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Unajibu dhaifu mno

Kwanza mimi sijazungumzia kua hakutakua na maisha baada ya corona

Pili hayo magonjwa yaliyopita na kuua watu hadi ikafikia hatua dawa imepatikana ebu elezea ni kwa namna gani dawa ilipatikana? Ni Kwa njia ya maombi?

Tatu, hiyo dawa ya maleria ilipatikana kwa maombi na jitihada za waumini ndi zilifanya mpaka mseto ukashushwa kutoka juu?

Kama majibu ya hayo maswali yatakua ni negative basi huna haki ya kusema huoni sababu ya mimi kukashfu dini.

It's Scars
Embu tupe maana yako ya neno "maombi" maana naona hayo ndo yanakutoa povu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwe unawaza kidogo.
Serikali ndo imekataza hayo mambo.
kwanini kiongozi wa dini aje kupinga?
Wewe kama hauamini kwenye dini endelea kutokuamini.
USIANZE KASHFA KWA VIONGOZI WETU WA DINI...
watu wameachwa kuingia na kutoka alafu leo ugonjwa unaingia utawalaumu viongozi wa dini au MUNGU?
TUPAMBANE NA HALI ZETU.wachawi ni sisi wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiwaza kidogo lazima uje na fikra ndogo kama hizi, I'm sorry for that

Kama kweli watu wa dini wanaweza kuuondoa huu ugonjwa kwa maombi basi serikali isingepiga marufuku na hata wao walikua na haki ya msingi kikatiba kujijeteta

Serikali imegundua kua maombi si chochote na ndo maana hata wao wenyewe wadini hawajaweka pingamizi

Kama kweli maombi yanafanya kazi sana kwanini tunawaona wanavaa mask huku wakihamasisha na wangine wavae kama kweli maombi yanafanya kazi?

Mfano katika nchi kama ya saudia arabia wale serikali yao yote inafata misingi ya dini lakini kwanini wamekua mstari wa mbele kukataza watu kutoka mataifa mengine wasiende mekka kama kweli power ya maombi inafanya kazi kama tunavyoaminishwa?

It's Scars
 
Janga mulitafute wenyewe,halafu,lawama mpeleke kwa Mungu.
Mugu alishaleta maelekezo ya jinsi ya kuishi,kupitia vitabu,Mitume,Manabii.Vitabu vyake,vina maelekezo yote ya maisha,kipi ufanye,na kipi uwache.Kipi ule na kipi usile.Mnakula popo,nyoka,majongoo,konokono nk.Halafu mkiumwa mwalamika kwa aliyewapa tahadhari.
Ni sawa na kumlaumu,aliyetengeneza gari au machine,wakati ameshakupa maelekezo kupitia vitabu na mafundi,jinsi kuitunza machine,kwa kuifanyia service,kila ukifika mda fulani,wewe huifanyii service,halafu wamlaumu mtengeneza magari.Au gari la petrol,unakwenda weka diesel,halafu unamlamu aliyetengeneza gari,likikataa kufanyakazi.

Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiambiwa dawa ya corona imepatikana na ili ukubali kua inafanya kazi kweli inabidi uamini

Halafu ukaletewa cyanide hapo kua inabidi uamini kwanza kabla haujanywa utakubali?

Je kuamini kwako kutabadilisha chochote kwenye cyanide kua kinga ya corona?

It's Scars
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Kutengeneza dawa sio swala la kiimani ni kitu ambacho lazima ukifanyie majaribio
so huwez kulinganisha kumwamini Mungu na swala la kutengeneza dawa coz Mungu wetu hajaribiwi.ndio maana huwez kwenda kwa Mungu na kusema "nipe dawa ili niamin kama upo" na ukapata Majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
J2 hii naskia kina ibada ya kuvunja corna kanisani kwa mbunge mama rwakatare.
Mmealikwa kwa wingi muhudhurie.
Thubutu

Nani atahudhuria?

Hizo bible zenyewe japokua zinanadiwa kua ni vitabu vya mungu lakini katika kipindi hichi watu watazikwepa kama daftari la mchango

It's Scars
 
Kama hili linajulikana kiujumla inamaana unataka kutuaminisha kua watu wadini ni wanafki?

Unafiki ni nini na unaingiaje katika hili ? Sijajua kwanini umewaita Wanafiki.
Kama mungu yeye ndio ameamua watu wafe kwa korona na jambo hilo linatambulika kidini kwanini watu wadini wanafanya maombi ili wasalimike?

Ulitakiwa uwaulize watu wa dini hiyo husika. Ila kwa kukusaidia tu kwa mujibu wa dini yangu Uislamu, tuna ambiwa yafuatayo :

"Kuchukua tahadhari katika juu ya jambo fulani ni kuitendea kazi dini yaani kuyafanyia kazi mafundisho ya dini, na kutochukua tahadhari na kufanya sababu ni kuitia dosari DINI (Yaani kuitia dosari Tawheed, ile hali ya kumpwekesha Mola katika uwezo wake)"

Watu wa dini wanachukua tahadhari sababu yote yanatoka kwake na hakuna anae jua amepangiwa nini juu ya janga hili.

Mathalani katika hadithi iliyopokelewa na Imaam Muslim, inayosimuliwa na swahaba Uthmani bin Affan, inaweka wazi muongozo juu ya magonjwa ya mlipuko yakiingia katika mji. Mtume wetu alifundisha ya kuwa "Panapo ingia magonjwa ya mlipuko (Tauni) basi watu waliopo katika mji husika wasitoke katika mji huo na wale ambao wako nje ya mji huo wasiingie katika mji huo"

Kwahiyo hii yote ni tahadhari na utaratibu huu umetoka kwa yule ambaye ameuleta ugonjwa huo, Mola anatautaka tuzifanyie kazi akili zetu na tuyafanyie kazi mafundisho yake. Mifano iko mingi juu ya hili, ila kwa sasa tosheka na maelezo haya mafupi.
Halafu kama point ya mungu ni kuwadhuru watu kwa corona kwanini vatican na mekka wakataze watu wasiende kuhiji makwao kwa kuogopa kudhurika na ugonjwa?

Hakuna aliye sema lengo la Mola ni kuwadhuru, bali nilisema ametaka ugonjwa utudhuru. Sababu kubwa ya ugonjwa au kudhihiri kwa majanga ni kutukumbusha waja wapi tukipo kosea na kurudi katika njia ya sawa. Kwahiyo kudhurika ni matokeo na si lengo.

Lakini, Allah ameweka utaratibu wake wa kuwa akileta janga sehemj halichagui yupi mkosaji na yupi si mkosaji, wote mnaingia na siku ya hesabu tutahesabiwa kwa haki.

Mathalani watu wa Makka (Nazungumzia dini hangu, na watu wa Vatican watazungumzia dini yao) hao wamefanyis kazi mafundisho ya mtume na hilo limetoka kwa Allah kwahiyo, hatutakiwi kubweta kubweteka si katika maagizo ya Allah, na kuchukua tahadhari na kutafuta sababu ndio amri ya Allah aliye juu.
Huoni kwa kuwazuia watu wasiende huko maana yake ni kuzuia watu wasidhurike jambo ambalo wanakua wanaenda kinyume na matakwa ya mungu?

Allah aliye juu akitaka jambo likufike popote ulipo linakufika, ila ukichukua tahadhari ni njia ya kutii amri yake, na kwa kutii amri yake hukuepusha na jambo hilo.

Kwahiyo huko hawajaenda kinyume a matakwa bali wametii maagizo ya Allah aliye juu.
Unaelewa kwa mujibu wako hao waliozuia nyinyi msiende huko wamefanya dhambi maana wanawanyima haki ya kusambaza ugonjwa ili watu wadhurike kama alivyokusudia mungu wenu??

Hili umeliona wapi toka kwangu mpaka useme kwa mujibi wangu ?

Kisha soma kwa umakini nilichokiandika ili ujue ya kuwa unae mzungumzia (Allah) hukuwahi kumjua na wala hukuwahi kupatia katika kumzungumzia.

Ahsante.
 
Janga mulitafute wenyewe,halafu,lawama mpeleke kwa Mungu.
Mugu alishaleta maelekezo ya jinsi ya kuishi,kupitia vitabu,Mitume,Manabii.Vitabu vyake,vina maelekezo yote ya maisha,kipi ufanye,na kipi uwache.Kipi ule na kipi usile.Mnakula popo,nyoka,majongoo,konokono nk.Halafu mkiumwa mwalamika kwa aliyewapa tahadhari.
Ni sawa na kumlaumu,aliyetengeneza gari au machine,wakati ameshakupa maelekezo kupitia vitabu na mafundi,jinsi kuitunza machine,kwa kuifanyia service,kila ukifika mda fulani,wewe huifanyii service,halafu wamlaumu mtengeneza magari.Au gari la petrol,unakwenda weka diesel,halafu unamlamu aliyetengeneza gari,likikataa kufanyakazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wote walioumwa corona wamekula popo na nyoka?

Mbona hatujahabarishwa kua wala nyoka na popo ndio victim wa hili gonjwa?

It's Scars
 
Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.

Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".
 
Hakuna dini,inayoruhusu kula hivyo,bila mpangilio wa chakula.Ni sawa na kusema,kuna kampuni za magari,nyingine zimeruhusu gari zao kutofanyiwa service.Dini zote,zimeweka utaratibu wa maisha,kuanzia usafi,chakula,kujifunza,kujitibu nk.
Unaposema,mpaka wa dini nyingine wamepata maambukizi,hawa wamepata kupitiya kwa ambao hawakufuata usalama wa maisha,kufuata maagizo ya dini,sawa na barabarani,asiyefanya service ya gari yake,atamsababishia ajali,pia anayefanya service,kama kufeli break,atamgonga na kusababisha ya ajali ya wengi,kwa uzembe wa mtu mmoja.
Dini yako ndo imekataza ya kwake huenda imeruhusu, sasa unataka watu wote waishi kwa kufata sheria za dini yako? We mbona hauli pop kwasababu dini zingine zimeruhusu

Na nyie wadigo imekuaje imewapata?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokua sahihi wakati nikizungumzia mungu ambaye si sahihi ni sahihi pia

Ushatanguliza kutokuwa sahihi kisha ukawa hauko sahihi katika jambo ambalo ni sahihi ni kujichagulia kukosea na kutokuwa sahihi.

Halafu siku ikatokea wanasayansi wamegundua dawa utamskia "si nilikuambia kua mungu atafanya muujiza basi ule muda ambao mungu aliupanga kujibu maombi yangu ndio huu"

Naposema humjui Allah unatakiwa uelewe yaani humjui kweli.

Allah ndio anawawezesha waja wake wafanye mambo wanayo yafanya, kwahiyo ukiona jambo limefanikiwa ujue ni kwa uwezo wa Allah amewazesha watu husika na ametaka jambo lifanikiwe na kinyume chake haliwezi kutokea wala kufanikiwa.

Hakuna kinachotoka nje ya milki yake, ndio maana wanao mkana wote ni Wagonjwa wa akili na wanafikiria kitoto sana na kwa upande mmoja.
 
Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.

Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".
Katika watu wajinga na mazwa zwa hapa duniani sijaona wa kuwazidi watu wa aina ya mtoa mada.

Nasema hivi hakuna wakuwazidi,mfano mzuri ni huu tu wa mtoa mada, yaani hamjui Mola halafu ajabu anamzungumzia kwa kutoa kasoro. Vichekesho hivi.
 
Unafiki ni nini na unaingiaje katika hili ? Sijajua kwanini umewaita Wanafiki.

Ulitakiwa uwaulize watu wa dini hiyo husika. Ila kwa kukusaidia tu kwa mujibu wa dini yangu Uislamu, tuna ambiwa yafuatayo :

"Kuchukua tahadhari katika juu ya jambo fulani ni kuitendea kazi dini yaani kuyafanyia kazi mafundisho ya dini, na kutochukua tahadhari na kufanya sababu ni kuitia dosari DINI (Yaani kuitia dosari Tawheed, ile hali ya kumpwekesha Mola katika uwezo wake)"

Watu wa dini wanachukua tahadhari sababu yote yanatoka kwake na hakuna anae jua amepangiwa nini juu ya janga hili.

Mathalani katika hadithi iliyopokelewa na Imaam Muslim, inayosimuliwa na swahaba Uthmani bin Affan, inaweka wazi muongozo juu ya magonjwa ya mlipuko yakiingia katika mji. Mtume wetu alifundisha ya kuwa "Panapo ingia magonjwa ya mlipuko (Tauni) basi watu waliopo katika mji husika wasitoke katika mji huo na wale ambao wako nje ya mji huo wasiingie katika mji huo"

Kwahiyo hii yote ni tahadhari na utaratibu huu umetoka kwa yule ambaye ameuleta ugonjwa huo, Mola anatautaka tuzifanyie kazi akili zetu na tuyafanyie kazi mafundisho yake. Mifano iko mingi juu ya hili, ila kwa sasa tosheka na maelezo haya mafupi.

Hakuna aliye sema lengo la Mola ni kuwadhuru, bali nilisema ametaka ugonjwa utudhuru. Sababu kubwa ya ugonjwa au kudhihiri kwa majanga ni kutukumbusha waja wapi tukipo kosea na kurudi katika njia ya sawa. Kwahiyo kudhurika ni matokeo na si lengo.

Lakini, Allah ameweka utaratibu wake wa kuwa akileta janga sehemj halichagui yupi mkosaji na yupi si mkosaji, wote mnaingia na siku ya hesabu tutahesabiwa kwa haki.

Mathalani watu wa Makka (Nazungumzia dini hangu, na watu wa Vatican watazungumzia dini yao) hao wamefanyis kazi mafundisho ya mtume na hilo limetoka kwa Allah kwahiyo, hatutakiwi kubweta kubweteka si katika maagizo ya Allah, na kuchukua tahadhari na kutafuta sababu ndio amri ya Allah aliye juu.

Allah aliye juu akitaka jambo likufike popote ulipo linakufika, ila ukichukua tahadhari ni njia ya kutii amri yake, na kwa kutii amri yake hukuepusha na jambo hilo.

Kwahiyo huko hawajaenda kinyume a matakwa bali wametii maagizo ya Allah aliye juu.

Hili umeliona wapi toka kwangu mpaka useme kwa mujibi wangu ?

Kisha soma kwa umakini nilichokiandika ili ujue ya kuwa unae mzungumzia (Allah) hukuwahi kumjua na wala hukuwahi kupatia katika kumzungumzia.

Ahsante.
Yani uchukue tahadhari kwa lengo lipi?

Mi navyojua tahadhari inachukuliwa kwa lengo la kujiepusha na kitu fulani. (unaweza kunikosoa hapa kama siko sahihi)

Sasa kakuumbia ugonjwa ili ukudhuru sasa huoni kuchukua kwako tahadhari kunaonesha unapingana na matakwa ya mungu?

Mungu angetaka wewe usidhurike asingekuletea ugonjwa, sasa mungu amependezewa wewe udhurike halafu wewe unam-challenge mungu kwa kuchukua tahadhari huoni kwamba hapo unashindana naye?

Huoni kwamba kuchukua tahadhari ili kuepuka hatari ambayo mungu kakuwekea ni kufanya dhambi?

It's Scars
 
Infact ni kwamba hakuna sector yeyote ambayo muafrika anafanya kwa weledi bila kukosea kama sector ya ujinga

Muafrika kwenye ujinga ndo anaplay part vizuri kuliko sector yeyote unayoijua wewe
Siungi mkono hoja ,,,hapo kwenye ujinga andika "upumbaavuu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.

Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".

Nimeweka wazi sio kwenye maombi tu bali kwenye dhana nzima ya uongo kupitia dini

It's Scars
 
Mungu yupo, Yesu kristo pia yupo. Ila Mungu hakai na wanafki. Wanachohubiri na wanachokifanya ni vitu viwili totauti. Mengi Kati ya wanayohubiri na kuyafanya ni machukizo kwa Mungu wetu wa kweli.
 
Unajua tatizo si dini hapo ila tatizo ni jinsi wanavyolichukulia tatzo la COVID19, hasa ilikuwa ni kutoa elimu kwa wananch kwa jinsi ya kuuepuka ugonjwa na si kuzuia watu kwenda kwenye maeneo ya ibada. Kwan hakuna jambo gumu kama kukikimbia kitu usichokiona, hivyo swala la corona na imani bado mahusian yake hayalerate kabsa. Na dini ni imani hivy ukiwa na iman juu ya kile unachokiomba kufanikiwa ni lazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom