Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 40,466
- 88,695
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
=============================
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Kwa kweli mkuu hii imekuwa kama danganya toto tuu!Wote wako chaka wanaskilizia madaktari watoe jibu la hitimisho maana wao tayari wamejipanga na majibu yao mfukoni mwao
Ikitokea madaktari wametoa dawa, tutawaskia wakisema maombi yao ndio yamewezesha wanasayansi kupata dawa.
Na ikitokea hakuna dawa iliyotengenezwa na wanasayansi watasema kua mungu katupa corona ili kutujaribu na kutupima imani au watasema mungu hujibu maombi kwa wakati wake
Wewe jamaa bhana
Kama hii ndio hoja yako basi unaweza kusema kila jambo limekuja kuumbua uongo wa dini.
Kwa nini hukusema kutafuta riziki kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kukaandani na kuomba dua halafu chakula kikamshukia.
Au kwanini hukusema kusoma kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kwenda msikitini kuomba dua kisha tayari akawa professor. Na hivyo hivyo mambo mengine.
We jamaa mwenyezimungu aliweka nidhamu/kanuni katika ulimwengu na mambo hayaendi vile unavyo fikiri wewe.
Kama Mungu aliweka nidhamu katika ulimwengu sasa kwanini corona inasumbua watu halafu tunaona wachamungu wakijihami kwa maombi wakati huu ugonjwa ni sehemu ya matokeo yanayotokana na nidhamu ya ulimwengu aliyoiweka mungu?Wewe jamaa bhana
Kama hii ndio hoja yako basi unaweza kusema kila jambo limekuja kuumbua uongo wa dini.
Kwa nini hukusema kutafuta riziki kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kukaandani na kuomba dua halafu chakula kikamshukia.
Au kwanini hukusema kusoma kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kwenda msikitini kuomba dua kisha tayari akawa professor. Na hivyo hivyo mambo mengine.
We jamaa mwenyezimungu aliweka nidhamu/kanuni katika ulimwengu na mambo hayaendi vile unavyo fikiri wewe.
Na hakuna mahali nimeandika kua mvunjike moyo msiaminiPamoja yote uliyoandika, huwezi kuvunja watu moyo wa kuamini.
Inaonyesha hujui neno maombi maana yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ona sasa mwingine huyuDunia yote imesalander! Hakuna mwenye nguvu, hakuna mwenye utaalamu, hakuna tajiri, hakuna teknolojia, hakuna silaha kali, hakuna usalama wa taifa, hakuna hakuna hakuna chochote. Kila nchi inalilia hali yake. Kila nchi inafunga mipaka yake, haijulikani tena nani anamfungia nani. Hakuna nchi inayohurumia nchi nyengine, kila moja inapambana kivyake... yote yamesababishwa na kidudu kidogo-virus.. wala hakionekani kwa macho!!!! Unahitaji nini kukubali kuwa Mungu yupo? ambaye akitaka lake hakuna nguvu yeyote inayoweza kulizuia?!!
Ameleta corona akitaka ataiondoa hakutaka ataiacha iendelee kutia adabu watu. Hapangiwi ampe nani na nani ni maamuzi yake tu!!! Watu wa dini yeye ndo anawajua zaidi kuliko wewe kama ni wa kweli au waongo! Sisi tunaomuamini uwepo wake na nguvu zake tunamuomba atunusuru na hili lkn hatuna haki ya kumlazimisha. Tunaomba, anaweza akatukubalia au akatukatalia! Hakuna mwenye guarantee ya maamuzi ya Mungu!
Sasa nani amekwambia amewaachia Madaktari,wakati yeye ndio ameruhusu ugonjwa huo uwepo na uwadhuru watu.
Yeye ndio ameuleta na yeye ndio wakuuondoa,hakuna mwanadamu mwenye kuweza kuuondoa ugonjwa wala kuleta ugonjwa.
Maelezo yako yote yanaonyesha ni kwa namna gani humjui Mola muumba wa mbingu na ardhi.
Inafurahisha mtu ambaye humwamin Mungu kutaka kuhakikishiwa kama yupo .hicho ni kituko kwa sababu step ya kwanza unatakiwa umwamin Mungu yupo nje ya hapo huwez kumwamin wala kumwelewaHso waebrania ulio wanukuu unahakika gani kama wamesema ukweli?
Unafikiri mapadre huko vatican hawajaona kua kuna nukuu za waebrania mpaka wameamua kupiga marufuku msiende?
Kutokua sahihi wakati nikizungumzia mungu ambaye si sahihi ni sahihi piaSahihi "ajabu" sio "hajabu" .
Sikujui kweli ila najadili ujinga wako juu ya jambo hili, kwa vile umeudhihirisha.