Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Kujikinga na kufata maagizo ya Mola muumba.

Swadaktaa huku tukiwa hatujui kama litatufika au halitotufika.

Sasa ukiona umechukua tahadhari na jambo limekufika ujue Allah ametaka likufike na huo unakuwa ni mtihani kwako kulingana chumo la mikono yako au anakuzindua juu ya jambo fulani.

Inanekana husomi ninacho kiandika, unaposema "ili" wakati lengo si akudhuru wewe unakuwa muongo, kudhurika ni matokeo ila lengo ni lile nililo litaja huko juu.

Sasa jitahidi kusoma na ukaelewa ili kuepusha kuuliza maswali ambayo yameshajibiwa katika maelezo yaliyo tangulia.

Ameleta ugonjwa na akitaka unakudhuru na asipotaka haukudhuru. Kwahiyo yote yapo kwake.

Unashindana nae vipi wakati unatii agizo lake mzee. Huelewi wapi ?

Hakuna dhambi hiyo kijana katika mafundisho ya dini, yaani huo ni utiifu na ukifanha hivyo unalipwa thawabu na unakuwa umefanya jema mzee.

Ukiwa haujui kivipi wakati huko juu umekiri kua mungu ndiye aliyeleta huu ugonjwa?

Inamaana saizi unataka kukana kua hujui kua mungu ndiye akiyeleta hili gonjwa kwa lengo la kuwadhuru?

It's Scars
 
Wewe jamaa bhana!!?
Unavyo mchukulia MUNGU ndivyo naye atakavyo kuchukulia ukimchukulia kwa uzito na yeye atakuchukulia kwa uzito ukimchukulia kikawaida basi ivyoivyo atakuchukulia wewe

Nauhakika na hili
Jibu hoja wewe acha povu... swali moja kati ya mengi ni je mungu anapenda sadaka na matoleo halafu wakati wa shida za watoa sadaka anajichimbia?
 
Dini na Imani ni vitu vya ajabu sana, utatukanwa hapa balaa kisa umegusa Imani na dini za watu. Watu wenye Imani zao huwa hawana reasoning kabisa, wao watakuambia "utalaaniwa".
 
Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.

Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".
Jibu zuri sana.
 
Ushatanguliza kutokuwa sahihi kisha ukawa hauko sahihi katika jambo ambalo ni sahihi ni kujichagulia kukosea na kutokuwa sahihi.

Naposema humjui Allah unatakiwa uelewe yaani humjui kweli.

Allah ndio anawawezesha waja wake wafanye mambo wanayo yafanya, kwahiyo ukiona jambo limefanikiwa ujue ni kwa uwezo wa Allah amewazesha watu husika na ametaka jambo lifanikiwe na kinyume chake haliwezi kutokea wala kufanikiwa.

Hakuna kinachotoka nje ya milki yake, ndio maana wanao mkana wote ni Wagonjwa wa akili na wanafikiria kitoto sana na kwa upande mmoja.
Dada uko na akiri sana na hoja anazoandika jamaa nazisoma najitathmini nakujiona mtu mwenye Reasoning sana...kweli kama huamini mungu hata reasoning inashuka.

Mfano hoja yake anasema hivi
“Eti mwanasayansi akigundua dawa hapo watu wa dini wameumbuka kwasababu dawa ijaletwa na maombi”

Imagine hoja kama hii yaani ameUbongo unaoamini kwamba wanaofanya maombi wanajibiwa jkwa kishushiwa dawa kutoka mbinguni na kudondoka ajui kwamba huko madaktari kufanikisha kupata dawa ndio maombi ya watu wa dini yamejibiwa.

Simply sichanfiagi uzi kama hizi maana naonaga hoja nyengine mpaka nauzika nakaushaga tu nisikufuru ila umejibu hoja zote kwa weredi kama ujaelewa achana nae.
 
Jibu zuri sana.
Jibu zuri sana wapi nawe shirikisha hata ubongo basi sio kila kitu kwako ni yes

Biblia yenyewe wanayoifata inasema ombeni nanyi mtapewa hakuna mahali imesema ombeni ila sio lazima kupewa

Na pia kwa imani unaweza kufanya kila kitu ikiwemo kuamisha milima vile vile umepewa mamlaka ya kukanyaga n'ge na nyoka bila kudhurika.

Saaa ungekua mpembuzi nilitegemea ungefika angle hii uanze kufanya hata comparison na nilichokiandika halafu ungekuja ku relate.

Kupitia imani zao na mamlaka waliyopewa mbona hawakuweza kuutokomeza ukimwi ambao unamiaka zaidi ya thelasini hapa nchini??

Kupitia maombi yao ambayo wameambiwa ombeni nanyi mtapewa mbona wameshindwa kuudhibiti huu ugonjwa usiingie hapa nchini?

Kama maombi na imani vimeshindwa kuzuia korona usiingie unadhani maombi ya sasa yataweza kuleta impact yeyote kuitokomeza??

It's Scars
 
Kipindi Cha nuhu watu walikebehi hivyo hivyo na wakaangamia ila elewa Mungu anataka tutubu ili atuondolee hizi balaa Kama tukikataa tutaisha. Dunia imejaa dhuruma, mauaji, unyanyasaji kwa wanyonge jamani tukubali kwamba uovu wa Sasa hivi ni zaidi ya ule wa sodoma na gomola

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu hoja wewe acha povu... swali moja kati ya mengi ni je mungu anapenda sadaka na matoleo halafu wakati wa shida za watoa sadaka anajichimbia?
Kuna mahali ulishaenda ukalazimishwa kutoa sadaka ????sadaka ni maamuzi yako ww kutoa na unatakiwa utoe kwa sababu fulani .sio kwa kuambiwa na mtu toa sadaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajabu ni kwamba hadi mkata kodi akifika church kuna ten percent anaiacha tena hapewi hata risiti
We jamaa umenchekesha [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ila kwa kifupi maswala ya Imani n ngumu kuyaelezea na kufikia muafaka kikubwa n kuheshimu Iman ya mtu

One love
 
Ukiwa haujui kivipi wakati huko juu umekiri kua mungu ndiye aliyeleta huu ugonjwa?

Inamaana saizi unataka kukana kua hujui kua mungu ndiye akiyeleta hili gonjwa kwa lengo la kuwadhuru?

It's Scars
Wewe jamaa uwe unasoma hoja sio kukimbillia kuandika maana Dada wawatu amelijibu ilo swali ×2 still unauliza swali lilelile.
 
nimejifunza biblia na mashaidi wa yehiva wana majibu ya haya yote..kuwa ni dini bandia za kujizalishia mali...wana maandiko ya kutosha miujiza ishakoma tokq enzi hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea unaamini nini. Haikufanya msafi kufanya kazi kiwanda cha sabuni, mpaka uichukue na kuitumia.

Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
 
Jibu zuri sana wapi nawe shirikisha hata ubongo basi sio kila kitu kwako ni yes

Biblia yenyewe wanayoifata inasema ombeni nanyi mtapewa hakuna mahali imesema ombeni ila sio lazima kupewa

Na pia kwa imani unaweza kufanya kila kitu ikiwemo kuamisha milima vile vile umepewa mamlaka ya kukanyaga n'ge na nyoka bila kudhurika.

Saaa ungekua mpembuzi nilitegemea ungefika angle hii uanze kufanya hata comparison na nilichokiandika halafu ungekuja ku relate.

Kupitia imani zao na mamlaka waliyopewa mbona hawakuweza kuutokomeza ukimwi ambao unamiaka zaidi ya thelasini hapa nchini??

Kupitia maombi yao ambayo wameambiwa ombeni nanyi mtapewa mbona wameshindwa kuudhibiti huu ugonjwa usiingie hapa nchini?

Kama maombi na imani vimeshindwa kuzuia korona usiingie unadhani maombi ya sasa yataweza kuleta impact yeyote kuitokomeza??

It's Scars
Hapana sikujibu kitu, maana majibu yangu yangekuwa kama Zurri tu, ila nikiangalia naona ujamakinika na majibu yake ili uelimike badala yake unauliza ×tatutatu ikiwa kitu ushajibiwa kwa makini.

Siwezi l.
 
Dada uko na akiri sana na hoja anazoandika jamaa nazisoma najitathmini nakujiona mtu mwenye Reasoning sana...kweli kama huamini mungu hata reasoning inashuka.

Mfano hoja yake anasema hivi
“Eti mwanasayansi akigundua dawa hapo watu wa dini wameumbuka kwasababu dawa ijaletwa na maombi”

Imagine hoja kama hii yaani ameUbongo unaoamini kwamba wanaofanya maombi wanajibiwa jkwa kishushiwa dawa kutoka mbinguni na kudondoka ajui kwamba huko madaktari kufanikisha kupata dawa ndio maombi ya watu wa dini yamejibiwa.

Simply sichanfiagi uzi kama hizi maana naonaga hoja nyengine mpaka nauzika nakaushaga tu nisikufuru ila umejibu hoja zote kwa weredi kama ujaelewa achana nae.

Ona sasa umefikia hatua unasifia mpaka unakosea unamuita mwenzako dada.

Kwanza inaonekana hujasoma vizuri ukalewa bandiko langu

Hapo juu nimeweka mfano ukiwalenga watu wa dzain kama yenu ambo ni wavivu kushirikisha ubongo

Mfano wenyewe nimesema watu wa dini tayari wameshajitengenezea self defense ili kuwapumbaza watu ambao sio wadadisi

Watubwa dini mpaka muda huu wanatembea na dhana mbili (positive na negative)

Kivipi, ikiwa watabibu wamefanikisha kupata dawa, watu wa dini watakuja na dhana ya (positive) watajinadi kua dawa hiyo imepatikana kwasababu ya maombi yao yamejibiwa na mungu ni hapa ndipo ule msemo wa god works in mysterious ways unapopata nafasi

Ila ikitokea hakuna dawa iliyopatikana, hapa watakuja na ile dhana ya (negative) kua mungu hujibu maombi kwa wakati wake au watasema hili ni jaribu ambalo mungu ametupa ili kutupima imani

Sasa nakuona nawewe umedondokea kwenye mifano hiyo hiyo hapo kua mungu atafanya muujiza kupitia madaktari

Nimesema vipi kama wote tukiungana kuomba kusiwepo na madaktari wa kuhangaikia tiba je maombi yetu yatafanya chochote?

It's Scars
 
Kipindi Cha nuhu watu walikebehi hivyo hivyo na wakaangamia ila elewa Mungu anataka tutubu ili atuondolee hizi balaa Kama tukikataa tutaisha. Dunia imejaa dhuruma, mauaji, unyanyasaji kwa wanyonge jamani tukubali kwamba uovu wa Sasa hivi ni zaidi ya ule wa sodoma na gomola

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hicho kipindi cha nuhu mungu ali respond haraka tofauti na sasa?

It's Scars
 
Back
Top Bottom