Kama ndo hivyo basi hakuna kipimo sahihi cha kujua ukweli
Kwasababu hata mimi naweza kusema spiderman yupo kweli kwasababu akili yangu imeniambia hivyo. Na kwasababu jibu umepata baada ya kutumia akili basi nitakua sahihi kusema hivyo
Na atakayepinga kua spiderman hayupo kihalisia naye atakua sahihi kwasababu katumia akili yake kufanya tathmini
Sasa wewe utajuaje kua habari za kuran ni kweli kwasababu akili yako imesema kua ni kweli, na sio kwamba akili yako imekupa majibu ya uongo kwasababu ni jambo ambalo halipo kihalisia?
It's Scars
Suala la kukubali kuwa kitu fulani ni sahihi au si sahihi inategemeana na hoja zako.
kukikubali kwa hoja au kupinga kwa hoja.
Sas ikiwa wewe unaipinga Quran kuwa si sahihi, lete hoja zako
ili akili ya mwenye kupima ichambue na kuthibitisha, lakini sijaona hata mahali pamoja katika uzi huu ulipoonesha kuwa Aya hii ni ya uongo.
Hata pale nilipo kutaka upinge hoja fulani ya Qur-an,ulikwepa na hukuonesha kuwa unacho cha kupinga makhsus bali unapinga kijumla jumla tuu.
Sasa niambie ni wapi katika Qur-an wewe umeona si sahihi?
Nakupa Aya za Mfano hapa chini kama kuna makosa ,onesha Makosa yake au kanusha.
Surat Yunus sura ya 10
3. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
4. Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walio amini na wakatenda mema. Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru.
5. Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua.
6. Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu.