Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Pili, onyesha nilipo jichanganya,kisha parekekebishe, ukiweza,hilo naacha kujadili huu mjadala.
Niparekebishe ili iweje?

Kukukosoa tu kumetosha na hii sio mara ya kwanza, kama unakumbuka vizuri makosa kama haya ndio yalikufanya ukakimbia mjadala hapo mwanzo

It's Scars
 
Mungu sio dhaifu na suala la Ayubu Mungu alijivunia uchaji wa Ayubu na imani ya Ayubu ndio maana aliruhusu mjaribu atende awezavyo na Ayubu alishinda na kurejeshewa maradufu alichopoteza,hivyo Mungu ameruhusu Corona kati yetu ilikupima imani yetu kwake kama dunia,taifa na MTU mmojammoja.
Nakama shingo zetu zitakuwa ngumu basi tutarajie baya zaidi kutukumba kama kwa Farao yaliyompata.
Mungu aliyeumba mbingu na dunia bado yupo kazi milele Amina.
 
Niparekebishe ili iweje?

Kukukosoa tu kumetosha na hii sio mara ya kwanza, kama unakumbuka vizuri makosa kama haya ndio yalikufanya ukakimbia mjadala hapo mwanzo

It's Scars
Kijana, wewe una dai kama umenikosoa au unanikosoa lakini kiuhalisia huna uwezo huo, ndio maana ili kuonye kwamba huwa una dai, nimekwambia onyesha hilo kisha rekebisha nilipo kosea, unaleta dibaji tena.

Nasubiri ujibu maswali niliyo kuuliza.

Ahsante.
 
utaumbuka wewe
 
Thibitisha mungu yupo kwanza

It's Scars
 

Sio kazi yangu

kukukosoa tu imetosha kuonesha ujinga wako ulipo

It's Scars
 
Thibitisha mungu yupo kwanza

It's Scars
Mtu anayetaka uthibitisho wa Mungu yupo au hayupo ni mtu jeuri kama Farao,mimi nakuombea kwa Mungu Mwenyewe ajithibitishe mwenyewe kwako kwa njia yeyote atakayoona inafaa kama kwa Farao na nina imani litatokea kwako
 
Sio kazi yangu

kukukosoa tu imetosha kuonesha ujinga wako ulipo

It's Scars
Huna uwezo huo kijana, ndio maana nikakupa fursa uonyeshe kosa kisha uusahihishe.

Mimi ninao uwezo wa kukuonyesha kosa na kukusahisha, kudai kila mtu anaweza, hata mjinga kama wewe unaweza kudai una elimu, ila tukikuomba uonyesha elimu uliyo nayo, ndio kama hivi una ruka ruka.

Ahsante.
 
Mtu anayetaka uthibitisho wa Mungu yupo au hayupo ni mtu jeuri kama Farao,mimi nakuombea kwa Mungu Mwenyewe ajithibitishe mwenyewe kwako kwa njia yeyote atakayoona inafaa kama kwa Farao na nina imani litatokea kwako

We Farao unamjua au ndio story za kusadikika?
 
Kweli kabisa.
Ila wale wana wa israel pale jangwani walijisababishia wenyewe kwa uukaidi wao
Mungu aliwambie waingie jerusalem na wawapige wakazi wake ,wao wakakataa wakamwambie Musa nenda wewe na Mungu wako kapigane sisi tunakusubiri,mukisha shinda ndo sisi tutakuja kuingia raha mustarehe.
Munngu aliwapa adhabu ya kuishi jangwani miaka 40.
Aliyekuambia nature inahitaji kuumbwa nani?
Ina mana unakubali kuwa Nature haihitaji kuumbwa,
Sas tuambie Nature ni nini?
Mbona si halisi,ni kitu tu cha kufikirika?
What is Nature?
 
Aliyekuambia nature inahitaji kuumbwa nani?
Sasa wewe Bw. ''Scars''
Wacha kubabaika na kuruka vihumzi ukiukwepa ukweli,Mwisho wa yote umeangukia kwenye Nature.Kisha unasema Nature haikuumbwa.
Ila Mimi nikikuambia kuwa Kuna Mungu Muumba wewe unaniambia Nithibitishe,wakati wewe huwezi kuithibitisha hii Nature.
Sasa Hapo ulipo ishia wewe Akili yako ,Ndipo Uungu unapoanzia,na unajikubalisha kuwa huna uwezo wa lolote mbele ya nature.
Soma Kidogo basi ujiongezee maarifa kama wewe ni mwenye kusikia na kufahamu.
Qur-an
Sura 42:

3. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyo kuletea ufunuo (Wahyi) wewe na walio kabla yako.
4. Ni vyake viliomo mbinguni, na viliomo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.

8. Na Mwenyezi Mungu angeli penda ange wafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi.

9. Au ( hawa watu wanaompinga Mungu ) wamechukua walinzi wengine badala yake (Mungu)! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi khasa. Na Yeye ndiye anaye huisha wafu. Na Yeye ndiye Mweza wa kila kitu.

11. Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama wa kufuga (hoa) dume na jike, anakuzidishieni namna hii (kwa kitendo cha kuzaana,baada ya dume kumpanda jike na kumpa mimba). Hapana kitu (kinachofanana naye) kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.

12. Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.

27. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia riziki waja wake (wote kuwa matajiri) , basi bila ya shaka wangeli panda kiburi katika dunia ( maisha yasingelikuwa na maana ya kutegemeana). Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho (kwa amtakaye). Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona .
 

Yaliyopo huko angani yanatosha kuonesha kuwa kuna nguvu kuu inayouendesha ulimwengu ikiwemo na dunia yenye wajinga wengi wenye kupinga hata uwepo wao wenyewe.
Wataalamu wa Sayansi takriban wote wanauona ufalme wa Mungu jinsi ulivyo mkuu.Mpaka wakati mwingine hudhania kuwa huenda Mungu asinge kuwa na muda wa kushughulika na kijisayari hiki kimoja kinachoitwa dunia na vilivyomo kwa jinsi alivyokuwa tajiri wa ukubwa wake na ufalme wake ulivyo danda waa.
Lakini ukweli ni kwamba Mungu hapitwi na hata jani linaloanguka juu ya mti ,ila elimu yake na hatima yake anayo.
Wewe endelea kuw mjinga kwa kuwa hukusoma Ulimwengu,umepata wanafalsafa wasiotaka kuzituma akili zao na kuandika mambo mengi ya Kubuni na kudhani kwa akili zao bila ya hata uthibitisho wa chochote. Wanajaribu kutumia Logic na umahiri wa akili walizopewa na Huyo Mungu mwenyewe,eti kisha watu wnamjadili Muumba na kumpangia lipi angalifanya na lipi asingelifanya.
 
Katika Ufalme huu wa Mungu wewe nani 'Scars' mpaka useme eti Thibitisha uwepo wake
Haya aliyoumba Mungu makuu huyaoni?
Basi hata wewe unapokwenda chooni na kubwaga mzigo kule ,jambo ambalo kimsingi binadamu halipendi,lakini inabidi huna namna,ia huwezi kuna udhaifu wako ,na Ukuu wa alikuumbia huo mfumo?
au usiku unaposinzia na kupoteza kabisa kumbu kumbu na kutojuwa nini kinaendelea ukiwa ume lala,huwezi kuona Uwezo wa liye kufanya uwepo?
Angelitaka angelikunyima huo usingizi ungeanza kukimbizana kwa madaktari kutafuta tiba,
Namuomba Mungu wangu Akupe Jaribio la kuonesha Uwezo wake japo kwa wiki moja hivi,Na asiuachie mpaka ukiri kuwe yeye ndiye Mungu na Muumba muweza ndo upate Releaf
 
Mtu anayetaka uthibitisho wa Mungu yupo au hayupo ni mtu jeuri kama Farao,mimi nakuombea kwa Mungu Mwenyewe ajithibitishe mwenyewe kwako kwa njia yeyote atakayoona inafaa kama kwa Farao na nina imani litatokea kwako
Hujaweza kuthibitisha mungu yupo, hivyo habari nzima ya maombi ni nonsense kama ilivyo maombi yaliyofanywa kwa ajili ya kudhibiti corona isiingie nchini halafu ikaingia

It's Scars
 
Quran inakunasihi Bw. 'scars'
30. Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi.
31. Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu.
35. Na ili wajue wanao jadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahala pa kukimbilia.
36. Basi vyote mlivyo pewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu kwa ajili ya walio amini, na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi,
48. Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyo yatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru.
49. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume,
 
Mpaka utakapo elewa. Usiwe na haraka.
Back to my questions

Umedai kua Allah asingeumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya asingekua muweza wa yote. Tunaona vitabu vinasema alipo yeye ni mahala patukufu hakuna ubaya wowote unaoweza kutendeka maana ni sehemu ambayo hakuna ubaya.


unakubali kwa hoja yako hiyo allah huyo sio muweza wa yote kwasababu huko mbinguni ambako yeye anaishi hakuna ubaya wowote?

Maswali yangu ambayo huko juu hujayajibu nayarudia hapa tena

Umesema Allah ni muweza wa yote na katika uwezo huo ni mjumuisho wa kufanya mabaya, refer kauli yako kua kungekua na mazuri peke yake asingekua mungu muweza wa yote kwasababu ameshindwa kuumba mabaya

Je kupitia uwezo huo allah anaweza kujiua?

Kupitia uwezo wote alionao, Allah anaweza kuumba jiwe zito ambalo hawezi kulibeba?



It's Scars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…