Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Point sio tiba tu, bali mechanism ya huo ugonjwa ambao wewe umedai kua ni mapepo na majini bado ni paradox. Kwasababu umeingiza dhana za kufikirika ambazo ukiambiwa uthibitishe uhalisia wake kama vitu hivyo vipo kweli, huwezi.

Umesema madaktari wenye taaluma za magonjwa mbali mbali wamesema hayo ni magonjwa ya akili tu na sio mapepo kama ambavyo misikitini na makanisani mnaaminishwa.

Sasa hao waliosema kua ugonjwa huo unasababishwa na mapepo na majini,, utawaamini vipi kua wakati siyo taaluma yao?

It's Scars
Unauliza nitawaamini vp wakati nakuelezea hapa kuwa wanatibu hilo tatizo na mtu anapona kabisa na hawapelekwi hospitali,mie sikulazimishi wewe uamini kuwa sababu ya hilo tatizo kuwa ni majini bali nakuelezea tiba ya hilo tatizo ambayo ni kweli na watu hupona. Sasa wewe ukiamini kuwa ni tatizo la magonjwa ya akili ni sawa tu ila kuhusu tiba ni kwa dua hutibu hilo tatizo na ndiyo point yetu hapa.
 
Kwasababu una relate na mungu, shetani allah, zombie na vitu vingine vya kufikirika

It's Scars
Kwahiyo umetaja spiderman kwa sababu spiderman ni kitu cha kufikirika ?

Sasa nani alikwambia kuwa Mungu ni kitu cha kufikirika tu kama spiderman? Mfanano hapo ni upi?
 
Yaaani mungu hapangiw nini cha kufanya maombi yanafanya kazi vizur tyu ila sasa kuja kwa corona kuna watu wamemrudia mungu mungu anaweza leta kity ambach kuna watu wataokoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi sio zama za kuamini, hizi ni zama za kujua

Imani ingekua ni njia sahihi ya kujua ukweli wa jambo basi dini ingekua moja

Au kila Miungu inayoabudiwa na dini yeyote ingekua niya kweli endapo tu watatumia imani kuabudu

It's Scars
Tunawaamini wanasayansi,madaktari n.k halafu wewe unasema hizi sio zama za kuamini? Au wewe huamini wanasayansi na madaktari?
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Nini maana ya neno "dini"?
 
Kuna mmoja alisema corona ni laana ya Mungu kwa wachina, juzijuzi naye akaupata, sasa sijui akipona atawaambia nini wafuasi wake.
Mbona unashindwa kumtaja na au kuweka link na sisi tunafahamu, Nani huyo na kayasema wapi hayo? Au mlikuwa wawili pekeenu alipokwambia hayo? Au unazuwa tu?
 
Mwenye haki huwa anaishi kwa Imani yake akisita-sita roho ya Mungu haina furaha nae.
Yaani katika vitu ambavyo kuna watu hawajui hata kama kipo duniani ni Corona
Huku Bush wanaendelea na mambo yao huo upuuzi wamewaachia mabrazamen wa mjini
Kumbuka sio kila tatizo unalolipotia wewe udhani kila mtu analipitia
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Mkuu Scars, tambua ya kwamba yapo majaribu kutoka kwa Mungu na mengine ni ya Ibilisi. Jaribu kutoka kwa kwa Mungu humfanya mtu mwenye imani akapate kuthibitika, bali jaribu la Ibilisi humfanya mtu kukufuru na hata kuangukia dhambini.

Hata siku moja kiongozi wa dini hawezi kutenda miujiza endapo jambo likija kwa makusudi yake. Jaribu litoke kwa Mungu ama Ibilisi, mwenye imani ya kweli tu ndiye atakayeweza kusimama.

Ona mwenyewe, viongozi wa kidini uliowataja, ijapokuwa hujitambulisha kwa vyeo vya kidini lakini hawana jinsi zaidi ya kuitegemea sayansi na teknolojia yake ilete majibu juu ya janga hili la COVID-19 badala ya kusimama ktk maombi yenye kuleta miujiza.

Amini, amini nakwambia, kama vile ambavyo dunia iliumbwa kwa Neno, mwanadamu akaumbwa kwa Neno, wafu hufufuliwa kwa Neno, wenye magonjwa na shida mbalimbali huponywa kwa Neno basi tambua janga hili si kitu chochote mbele za Mungu.

Kiinachokosekana ni watu sahihi wenye kulibeba Neno la kweli katika kipindi hiki cha sasa cha nyakati za kanisa. Kipindi ambacho kinaitwa Laodikia, kipindi chenye imani vuguvugu, si baridi wala si moto. Kwa uvuguvugu huo kwa hakika kimeshatapikwa kutoka kinywani kwa mwenye kulimiliki Neno (Ufunuo 3:14-18).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unashindwa kumtaja na au kuweka link na sisi tunafahamu, Nani huyo na kayasema wapi hayo? Au mlikuwa wawili pekeenu alipokwambia hayo? Au unazuwa tu?
Mkuu, sijataka kuanzisha mjadala katika hili ndiyo maana sijazungumza kwa kina. Kama hujasikia, dunia haiko kwenye giza bado. Unaweza kujitafutia taarifa mwenyewe.
 
Nachoamini Mimi mungu yupo na anamakusudi na sisi watu wake, hata kuja kwa corona ni mpango wa mungu vilevile kuna kitu mungu anataka tujifunze kupitia janga hili la corona,,, kwa uhai nilionao na pumzi ya bure nayofuta bila kulipia chochote naamini kuwa mungu yupo hai na anatenda,, tumshukuru mungu kwa kila jambo hata Kama ni magumu.
 
SHETANI MWENYEWE ANAJUA UWEPO WA MUNGU NA ANAMWOGOPA SEMBUSE WEWE SISIMIZI? NI WAKATI WAKO KUMJUA MUNGU NA KUTUBU SIKU YA HUKUMU YAJA.
 
Sema maswali niliyohoji yakijibiwa kiufasaha bila watu kuogopa yatahibitisha Mungu hayupo

Mambo ya dini magumu sana halafu hapo hapo unawataja muhammad na yesu ambao wamezungumziwa na dini, utajuaje kua ugumu huo sio pamoja na kuongopewa uwepo wa hao watu uliowataja?

It's Scars

Kijana swali gani au maswali gani hujajibiwa ?

Hii mada tulishaimaliza kitambo sana, nashangaa unaposema hujajibiwa maswali yako. Siku ukiamua kuwa mkweli ujinga ulio nao utaondoka.
 
Basi kaa kimya hata kuelezwa hufai subiri kifo chako tu na kuombea uzikwe kama kiroba bila dini yoyote

Wanacho nikera hawa watu ni kuwa hawamjui Mola lakini wanajitutumua kukosoa au kumkosoa, kinachowakuta ni kukosea kila nukta.

Kwanza wanakosea kuhoji kwa kuhoji na kupelekea maswali yao yote kuwa ya uongo, wanachotakiwa ni kurekebisha njis zao za kuhoji, iki wahoji kwa usahihi.
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Liwekwe kongamano la kukanyaga mafuta na mwamposa wetu mafuta ya [emoji535]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie watu watu mnaojifanya mnatenga dini na imani ya Mungu huwa mnanishangaza kwa sababu wengi wenu humu mmekulia katika hizi hizi dini na ndipo mlipojua kuhusu Mungu,hivyo hata huyo Mungu mnaemfikiria nyie pasina dini ndiye yule mliyemjulia kutoka kwenye dini.
Naamini Mungu yupo lakini hainizuii kuhoji

Mimi sio mtumwa wa dini kama wewe
That is the difference between me and you

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachoamini Mimi mungu yupo na anamakusudi na sisi watu wake, hata kuja kwa corona ni mpango wa mungu vilevile kuna kitu mungu anataka tujifunze kupitia janga hili la corona,,, kwa uhai nilionao na pumzi ya bure nayofuta bila kulipia chochote naamini kuwa mungu yupo hai na anatenda,, tumshukuru mungu kwa kila jambo hata Kama ni magumu.
Yaani Mungu anataka tujifunze kupitia mateso

Basi nasema Hivi Huyo Mungu wako ni mpumbavu

Mungu nayemwamini hayuko hivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Virusi vya corona vimekuja kuthibitisha wazi kua maombi hayana msaada wowote kwenye maisha ya binadamu na wala dini haiwezi kuwaokoa binadamu na janga lolote la asili hivyo kuabudu na kufanya maombi ni kazi bure.

Juzi niliona Italy wakitembeza msalaba na sanamu la maria mama wa yesu angani ili kuwaokoa, kilichofuatia ni vifo vingi zaidi vya watu.

Jana niliona video clip Gwajima akisihi watu kunawa mikono, nikajiuliza ameshindwa kuombea watu hili gonjwa lipite au mungu wake anachagua magonjwa ya kuponya na ya kuacha yaue watu maana mara nyingine hua wanadai wanaombea na kuponya ukimwi, kansa, nk, je corona mungu haiwezi?

Corona imevamia Italy hadi vatcan imeua mapadri, viongozi wakubwa wa kidini vatcan(petro alipojenga kanisa-mwamba)wanakufa kwa corona, mwamba unaenda kuanguka, siku corona ikimvaa papa ndio tutajua hatujui.

Haya mambo ya dini, maombi na sala ni ya watu, hayawezi kumsaidia binadamu kwa chochote. Mungu anaeshindwa kuzuia majanga na magonjwa ataweezaje kuyaondoa kwa maombi ya binadamu kama yeye na malaika wameshindwa kuzuia kabla?

Tuendelee kuomba ndugu zangu😀
 
Back
Top Bottom