Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Hapa tena umekubali

Sasa rudi kule mwanzo kajibu maswali yangu ambayo uliyakimbia

It's Scars
Haya ndio yale yale niliyo kwambia post ya 13 na 120 na majibu mengine, sasa unaposema nimekubali unatakiwa kuonyesha nimekubali nini na wapi ?

Kijana hapa hutoki.
 
Tatizo lako moja humakiniki

Hapo kwenye neno "mwanasayansi" unaweza kuweka jina lolote iwe mkulima au nani na bado ukawa kwenye duara lile lile ambalo nimelichora

It's Scars
Hebu muweke mkulima katika hilo duara tuone utakavyomuelezea.
 
Uzima ndio unaokupa kiburi.
Hata mtoto mpumbavu akiwa na kiburi anaweza akamwambia mama yake usinisumbue hata Mimi ningetangulia ningekuzaa.

Umewahi kujiuliza maswali haya :-
Kwa nini sio kila mtu ni Daktari?
Kwa nini sio kila MTU ni Mchawi ?
Kwa nini sio kila MTU ni mwanamziki au Mchezaji au Mwana Sarakasi ?
Kwa nini sio kila MTU ni Mwanamazingaumbwe?
Kwa nini kila MTU sio Mwanajeshi au kwa nini sio kila mwanajeshi ni Komandoo?
Kwa nini wote hatuna akili sawa?
Kwa nini wengine ni Magenius na wengine sio?

Huoni tu kuwa kuna Mwenye Maarifa makubwa aliyewaumba hawa watu na kuwapa vipaji kwa kazi na wakati wakati wake?

Kama binadam ametengeneza magari ya aina tofauti na kila moja na ubora wake kama vile Benz ,Toyota, Mitsubishi, Nissan, Land Rover n.k. Kichaa na mpumbavu ndiye anayeweza akasema hayo magari yamejitengeneza yenyewe.
Binadam wameumbwa na kupewa akili ya kujisimamia .

Engineer wa Umeme akishawasha umeme anaondoka zake umeme unaendelea kuwaka kwa kiwango alichoweka. Ukikatika hata vishoka wanaweza kuunga tena.

Mungu ana Mambo Mengi na kazi kubwa ya kupambana na muasi Shetani sio kuhangaika na Korona walizozitafuta wafuasi wa Shetani kwa tamaa zao za kutajirika na kumiliki uchumi na madaraka ya dunia.

Dawa zinatoka kwa Mungu kama haujui.
Ndugu yako Shetani amekua akidanganya watu sana lakini ujanja wote wa dawa unatoka kwa Mungu ndio maana hata alama ya tiba dunia nzima ni Nyoka aliyejisokota kwenye mti.

Waganga wote wa asili wanarithishwa kwa imani ya mizimu namna ya kutambua miti ya dawa. Hii pia ni dini.

Waitali wameasi na kukufuru sana mana Makanisa mengi wameyageuza kumbi za starehe na club za Pombe na kufanya kila aina ya ufuska kwenye majengo ya Makanisa. Sasa Mungu ameamua kuudhihirisha ulimwengu kuwa kazi za mikono yao haziwezi kuwaokoa bila kutii amri zake.

Bado wewe zamu yako inakuja. Utamheshimu Mungu tu kabla hujafa.
Mana kama sio Corona itakupiga Sukari na kama sio sukari itakupiga Presha,kama sio Presha utakupiga Ukimwi na kama sio ukimwi utapigwa na ajali na kama sio ajali utapigwa na Kansa na kama sio kansa utapigwa na Mpafu na kama sio mapafu utapigwa na vidonda vya tumbo.
Utamkumbuka tuu aliyekuumba na kukupa pumzi na akili na sasa unasema hayupo . Utakapokuwa unachungulia kaburi utawaza kuwa mada haiwezi kuharibiwa lakini inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine. Utaona unavyokaribia kubadilika kwenda kwenye hali usiyoijua ndipo utakapomkumbuka Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia mjadala mwanzo mwisho acha na mimi nichangie kdg.Kwa ujumla mtoa mada ana logic katika hoja zake. Binafsi mimi ni mkristo s.d.a na naamini Mungu yupo.Labda nianze tu kusema kuamini uwepo wa Mungu ni IMANI na kutokuamini uwepo wake ni IMANI vilevile. Ukweli ni kwamba kuprove uwepo wa Mungu physically ni vigumu but ni kama upepo kuna uwezekano wa kuprove uwepo wa upepo kwa effect zake.
Mimi binafsi pamoja na kukuwa na ku be influenced na family yangu juu ya uwepo wa Mungu lakn nilipokuwa na akili timamu niliamua kuamini uwepo wa Mungu kwa kujiulza maswali kadhaa e.g

Kuto amini hakuwezi kua imani

1. Kabla ya kuzaliwa nilikuwa wapi
Kabla ya kuzaliwa haukuwepo

2. Kuna mambo mengi yanayoendelea mwilini na nje ya mwili ambayo ni nje ya uwezo wako (hupangi wewe) involuntary hata ku exist kwako na hta hiyo reasoning power/ability uliyonayo ya kuchallenge hata uwepo wa Mungu
Hayo mambo ambayo yanaendelea bila wewe kuyapanga tafsiri yake huyajui yanafanyikaje na sio kwamba upendekeze jibu la mungu kua ndio liwe mbadala.

watu miaka ya nyuma waliona radi ikiunguruma waliamini kua ni sauti ya mungu amekasirika lakini leo hii radi inaelezewa vizuri bila dhana potofu kama hiyo.

Huenda miaka hiyo ungewaambia kua hiyo radi sio mungu bali ni msuguano wa mawingu watu wangekupiga mawe kua unakufuru

3.ukifa inakuaje

Ukifa unazikwa na habari inaishia hapo

Unataka kuwe na muendelezo baada ya hapo wakati umekufa na mwili wako utaoza?

Kukiwa kuna muendelezo baada ya kufa utakua ulikufa kweli au ulizimia?

4.nashuhudiaga mtu mwenye mapepo ukitaja jina la Mungu wanaongea kabsa kukiri uwepo wake kama ni mgonjwa wa akili tu awezi kugbu vile .
Hii ni drama hujui bongo movies hadi makanisani zipo?

Mapepo ni uzushi kutuibia sadaka zetu

Unafikiri kwanini wao mapasta wamekua wakisema wanayatoa badala ya kuyaua wakati wanajinadi kua wamepewa mamlaka makubwa na mungu?

Yani unatoa pepo ambalo litamuingia mtu mwingine halafu unasema kanisa la uponyaji? hao wanaponya au wanaamisha tatizo?

Mapepo ni hadithi tu

5.mfumo na utendekaji wa vitu duniani ambayo hta science inakubali kuwa hata kimoja kiki disobey hali itakuwa tofauti kabsa mfano hta kwa cku 1 tu dunia isi rotate e.t.c effect yake ni kubwa sna e.t.c
Kwanza ukifatilia hoja hii upande wa dini imezungumziaje utaona kuna contradiction hapo dini imepinga dunia kuzunguka

Lakini hata hivyo kwanini kuzunguka kwa dunia kuthibitishe mungu na sio kingine?

Kwanini kuzunguka kwa dunia kusithibitishe maajabu ya dunia na sio kutegemea jambo lingine?

6.Origin of life kwa kila kitu.
Kuna haja ya chanzo ili kitu kiwepo

Kama hakuna haja, basi hatuna chanzo

Kama kuna haja, basi mungu hayupo maana naye atahitaji chanzo kwasababu yupo na huyo aliyemsababisha mungu kuwepo atahitaji chanzo nk.

In general vitu hivi vichache tu kuacha viiingi vinaprove kuwa kuna nguvu nje ya ubinadamu inayo control each and everything ambayo wengi ndio wanaamua kuamini ndo MUNGU wake/wao. Coz ana influence na DESTINY yako .sasa mtu anaweza amua tu kuiamini au kutokuiamini.
Haya ni majibu ya kivivu yasiyozingatia misingi ya utafiti

Watu wasiopenda kudadisi huibuka na jibu kama lako kwasababu wakishindwa hawawezi kusema hatujui jibu bali hupendekeza nadharia yakufikirika

Mwisho kabsa hta ukiiamini na kuamua kufuata mafundsho ya dini fulani basi utaishi kwa imani hiyo kuliko asiye amini kabsa nahsi anaishi kwa hofu zaidi kwamba je nikimkuta yupo na nilimpinga itakuaje?
Watu wa dini ndio watu wanaoishi kwa hofu

Sina hofu kua nikila nguruwe ni dhambi, sina hofu kua nisipo muamini mungu ntaenda motoni

Watu wa dini wanaamini mungu kwa hofu ya kuchomwa moto ambao vitabu vyao vimesema.

Na ndio maana hata humu baadhi ya wadau wamenijia juu kua "huna hofu ya mungu ndio maama unamkufuru"

Inamaana kinachowafanya wao mpaka muda huu waendelee kuamini mungu wengi wao hawajapenda kwa hiari yao bali hofu ya kuogopa moto wa jehanamu ambao ni wakufikirika ndio sababu iliyopelekea wadumu kwenye dini na kuamini mungu yupo

Sasa ukiamua kuamini uwepo wake na dini fulani through hiyo dini tunaweza jadili sasa swali lako la msingi kwa nini Mungu mweza wa vyote hivo aruhusu vitu vibaya e.g Corona, magonjwa mbalimbali , njaa ,vifo ,shida mbalimbali etc ziwakumbe viumbe vyake ziwe ni binadamu kasababisha au yeye mwenyewe katoa pigo but ameruhusu itokee coz alikuwa anaweza kuizuia.
Kwanza siwezi set njia potofu kwa ajili ya kupata jibu sahihi

Kwanini swala la uwepo wa mungu ambaye yupo kila mahali lihitaji imani?

Lakn bila kukubaliana juu ya uwepo wa Mungu mada ya pili haitakuwa na Mwisho. Coz reference za Bible huziamini za Quran huziamini. So we umechagua imani hiyo na ss tumechagua imani ya kuamini Mungu yupo hamna haja ya kulumbana sna.
Ukitoa hoja zinazothibitisha mungu yupo mbona utakua umefanya jambo kunwa sana ambalo miaka mingi hakuna aliyewahi kufanya

Pengine kuweza kwako kuthibitisha mungu yupo kutakufanya utoke font page kwenye majarida ya kidunia

Ni sawa na Mzungu kumshangaa mswahili kuita mtoto "MTOTO" na mswahili amshangae mzungu kumta mtt "BABY" na kila mmoja kumtaka mwenzake abadilike amfuate.
Kwaiyo unathibitisha mungu yupo au unani-recommend niamini bila uthibitisho?

It's Scars
 
Sababu yeye ndio ameweka utaratibu huu.

Umethibitisha wapi hili ? Ukiweza naacha kutumia hii "Id"

Unajuaje kua yeye ndiye aliyeweka huo utaratibu?

Nimekuthibitishia hapa hapa

It's Scars
 
Unajuaje kama seli za binadamu zinaelekea kufa au kwa kipi ?

Seli hizo huchukua muda gani mpaka zina choka ?

Magonjwa yanathibitisha hilo

Hakuna muda maalumu wa seli kuchoka bali kulingana na mazingira yakiwa rafiki basi zitaweza kudumu bila kuchoka kwa kipindi kirefu lakini ikiwa kama si mazingira rafiki itakua ni kinyume

It's Scars
 
Nimesjajibu hilo swali.
Hujajibu ndio maana nalirudia kwa kuweka msisitizo

Hujajibu swali hili

Unajuaje kwamba waandishi wa dini hawakutumia spirit hiyo ili uongo wao kuhusu dhana ya uwepo wa mungu ufanikiwe?

It's Scars
 
Uzima ndio unaokupa kiburi.
Hata mtoto mpumbavu akiwa na kiburi anaweza akamwambia mama yake usinisumbue hata Mimi ningetangulia ningekuzaa.

Umewahi kujiuliza maswali haya :-
Kwa nini sio kila mtu ni Daktari?
Kwa nini sio kila MTU ni Mchawi ?
Kwa nini sio kila MTU ni mwanamziki au Mchezaji au Mwana Sarakasi ?
Kwa nini sio kila MTU ni Mwanamazingaumbwe?
Kwa nini kila MTU sio Mwanajeshi au kwa nini sio kila mwanajeshi ni Komandoo?
Kwa nini wote hatuna akili sawa?
Kwa nini wengine ni Magenius na wengine sio?

Huoni tu kuwa kuna Mwenye Maarifa makubwa aliyewaumba hawa watu na kuwapa vipaji kwa kazi na wakati wakati wake?

Kama binadam ametengeneza magari ya aina tofauti na kila moja na ubora wake kama vile Benz ,Toyota, Mitsubishi, Nissan, Land Rover n.k. Kichaa na mpumbavu ndiye anayeweza akasema hayo magari yamejitengeneza yenyewe.
Binadam wameumbwa na kupewa akili ya kujisimamia .

Engineer wa Umeme akishawasha umeme anaondoka zake umeme unaendelea kuwaka kwa kiwango alichoweka. Ukikatika hata vishoka wanaweza kuunga tena.

Mungu ana Mambo Mengi na kazi kubwa ya kupambana na muasi Shetani sio kuhangaika na Korona walizozitafuta wafuasi wa Shetani kwa tamaa zao za kutajirika na kumiliki uchumi na madaraka ya dunia.

Dawa zinatoka kwa Mungu kama haujui.
Ndugu yako Shetani amekua akidanganya watu sana lakini ujanja wote wa dawa unatoka kwa Mungu ndio maana hata alama ya tiba dunia nzima ni Nyoka aliyejisokota kwenye mti.

Waganga wote wa asili wanarithishwa kwa imani ya mizimu namna ya kutambua miti ya dawa. Hii pia ni dini.

Waitali wameasi na kukufuru sana mana Makanisa mengi wameyageuza kumbi za starehe na club za Pombe na kufanya kila aina ya ufuska kwenye majengo ya Makanisa. Sasa Mungu ameamua kuudhihirisha ulimwengu kuwa kazi za mikono yao haziwezi kuwaokoa bila kutii amri zake.

Bado wewe zamu yako inakuja. Utamheshimu Mungu tu kabla hujafa.
Mana kama sio Corona itakupiga Sukari na kama sio sukari itakupiga Presha,kama sio Presha utakupiga Ukimwi na kama sio ukimwi utapigwa na ajali na kama sio ajali utapigwa na Kansa na kama sio kansa utapigwa na Mpafu na kama sio mapafu utapigwa na vidonda vya tumbo.
Utamkumbuka tuu aliyekuumba na kukupa pumzi na akili na sasa unasema hayupo . Utakapokuwa unachungulia kaburi utawaza kuwa mada haiwezi kuharibiwa lakini inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine. Utaona unavyokaribia kubadilika kwenda kwenye hali usiyoijua ndipo utakapomkumbuka Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi wapenzi wa Mungu mnaruhusiwa na kutoa hukumu pia?
 
Asie jua wew muislamu nani, pita kushoto, endelea na upagani wako sasa
Roho mtakatifu kakuingiza chaka hebu msisitize kesho kukikucha huenda amekujibu jibu sio kwasababu ya hangover

It's Scars
 
Haya ndio yale yale niliyo kwambia post ya 13 na 120 na majibu mengine, sasa unaposema nimekubali unatakiwa kuonyesha nimekubali nini na wapi ?

Kijana hapa hutoki.
Aisee hii kasheshe

Kwaiyo hata ulichokikubali nacho hukijui?

It's Scars
 
Kaka hakuna Muislamu kilaza kama huyu mzee, muweke mahala anapostahili ila huku hastahili.
Kwanza siwezi kua muislamu bora vyenyewe umeweka wazi, huyo suriya nia yake ni kuona wote tuwe wajinga kama nyie

It's Scars
 
Nimepitia baadhi ya maneno yalioandikwa huku nimechekea sana watu wanavo defend vitabu vilivoletwa na Mashua kupitia bahari ya Hindi na kutua Kilwa Kivinje na Bagamoyo.

If you know your history well, you’ll know where your coming from.

Babu yako alieishi mwaka 1750 alikua dini gani?
 
Back
Top Bottom